Kwani kasimu anatoa hela zake kuihudumia namungo?ngoja nikupe faida kidg juu ya timu ya namungo
Kwanza ukae ukijua namungo ipo chini ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya elianje genesis ambao hawa hutoa kila kitu kwa timu ya namungo
Pili namungo pia ipo chini ya halmashauri ya wilaya ya ruangwa ambao wao kila inapofikia msimu wa mavuno hukata asilimia kadhaa ya pesa kutoka kwa wakulima kwaajili ya mchango wa timu ya namungo na wilaya ya ruangwa kwa mwaka ina misimu mitatu ya kilimo.ufuta mbaazi na korosho na pia kuna makampuni ambayo yapo ruangwa ya uchimbaji wa madini nayo huchangia juu ya uendeshaji wa timu hii
Kwa ufupi tu namungo tayari ilishatengenezewa mifumo imara ya uendeshaji wake na hivi sasa wapo kwenye ujenzi wa uwanja wao wa mazoezi