Mining Indaba Capetown, Kenya wasio na madini wana banda, Tanzania wenye madini hawana banda

Propaganda za CCM zimetukolea kweli kweli. Wamewaaminisha watanzania sisi pekee ndiyo tuna madini ili ile dhana yao ya uongo kuwa "tunaonewa wivu" ionekane ina mashiko!
Hii ni mbaya sana hii, na inabidi ipigwe vita ni sawa hili fukuto la Bima linalochekelewa sasa likishika moto watu watatafuta kwa kujificha
 
Hivi kweli jamani kuna nchi duniani ambayo haina madini aina yoyote ile?
 
Aliyekuambia Kenya haina madini ni nani?? Futa tongo tongo, huko magharibi mwa kenya kwa ndugu zetu waluhya dhahabu imevumbuliwa juzi tu hapa, wacha kujifungia
 
Mnpenda sana kusikiliza stori za uongo za Wakenya.

Aliyewaambia Kenya hakuna madini ni nani?

Yaani Tanzania kuwe na madini, Tarime halafu Kenya upande huo Migori kusiwe na madini???
Najuwa hata mchanga wa kujengea nao lazima uwe na leseni ya Idara ya Madini. Kweli Kenya wanayo madini lakini je ni valuable kama Gold, Cobalt au Tanzanite
 
Najuwa hata mchanga wa kujengea nao lazima uwe na leseni ya Idara ya Madini. Kweli Kenya wanayo madini lakini je ni valuable kama Gold, Cobalt au Tanzanite
Kila kikichopo Tanzania, na Kenya almost kipo.

Ingawa vingine siyo kwa wingi kama Tanzania.

Kinachofanya sekta ya madini isipige hatua Kenya, ni kwasababu ya sera yao ya aedhi, na uhuni wa wanasiasa na hivyo uchimbaji mwingi ni HARAM.

Dhahabu ipo kwa wingi sana Kenya, na kuna migodi kibao ya wachina wanachimba.
 
Na basically airport ya kwanza ilijengwa hapo pia
 
Hiyo ni peanut Bro!! Soma hapo chini ulinganishe na Tz:-

 
Wanafikiri tz pekee ndiyo kuna madini

Ova
Wana madini kiduchu ambayo mchango wake kwa pato la Taifa ni chini ya 1%. Huwezi kujihesabu una madini
 
Aliyekuambia Kenya haina madini ni nani?? Futa tongo tongo, huko magharibi mwa kenya kwa ndugu zetu waluhya dhahabu imevumbuliwa juzi tu hapa, wacha kujifungia
Peanut au kwa Kiswahili ni kiduchu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…