Miradi mikubwa haikuanza kipindi cha Hayati Magufuli pekee

Labda kama huna unalolijua kuhusu ilo bwawa, ila unabyomuona Samia na Janauary wanaubunifu wowote? Just be neutral! Samia anavyomuona ni mtu ambae anasumbua kichwa chake kutafuta taarifa? Kubuni vitu?
Kubuni ndio Nini? Mambo yote yapo kwenye mpango wa taifa wa miaka mitano Kuna mpaka miradi ya umeme wa joto ardhi na upepo. Kuna masuala ya kununua meli za bahari kuu za kuvua samaki, Kuna mradi wa kuvuna gesi asilia, Kuna mpango wa kujenga Barabara nane till Morogoro and so on.

Hata JPM sio kama alibuni ni mpango ulishakuepo hata flyover ulikuwepo kwenye DMDP na kipengele Cha decongestion Dar Es Salaam kwenye mpango wa taifa wa miaka mitano 2011-2016!!!
 
How many times the efforts to ditch out the project have failed? Hakuna kitu kinachofanyika gizani kisijulikane mwangani. Mbwembwe za kubeza jina la JPM ndio linalofanya atamkwe sana kwa wema au ubaya.
When did they plan to ditch out the project? Acheni hearsay na speculation hakukua na mpango wa kuacha mradi ule ilikua kelele za Mitandaoni tu ila ujenzi uliendelea kwa Kasi Ile ile. Sasa mradi umeisha badala ya kumpongeza mama wameanza oooh bila JPM wasingeweza mara ooh walidhani bwawa halitajaa kisa miti kukatwa??

Ndio nashangaa kwamba kwani kama Kuna pesa na engineers kinachoshindikana ni Nini mpaka tuaminishwe ni JPM pekee anayeweza kujenga miradi.
 
Una matatizo wewe! Ilo Bwawa lilikuwa katika mpango wenu wa miaka mi5? Kuvuna gas ilo najua kwa Kikwete sawa lilikuwepo ila sio kufufua shirika la ndege, ujenzi wa bwawa la umeme rufiji, ujenzi wa meli ziwa victoria hivo wala havikuwepo kabisa
 
Miaka 10 huwezi kufanya na kumaliza kila kitu. That is not possible. What we miss as a country ni continuity. Tunafanya kama vile kila awamu ni private project ya watu fulani.
We are missing a point
Continuity ipo sana tu unless hausomi ilani za chaguzi na kuona mipango ya taifa then fuatilia vipaumbele vya bajeti. Aliyetaka kuharibu ni JPM kufanya manunuzi nje ya bajeti kinyume kabisa na mpango wa taifa na dira ya taifa. Mfano kujenga airport chato was irrelevant.
 
Nani kakuaminisha kitu? Kuamini ni project yako binafsi. Tuache kufanya project kubwa za nchi ni kitu personal. Tunafeli sana
 
Una matatizo wewe! Ilo Bwawa lilikuwa katika mpango wenu wa miaka mi5? Kuvuna gas ilo najua kwa Kikwete sawa lilikuwepo ila sio kufufua shirika la ndege, ujenzi wa bwawa la umeme rufiji, ujenzi wa meli ziwa victoria hivo wala havikuwepo kabisa
We ndio una matatizo Bwawa lilikuwepo kwenye makabrasha ya time ya mipango tokea mwaka 1974 Wala sio idea ya JPM
 
Hakuna continuity...Mfano mdogo tu...Mkapa alianzisha Mkurabita na Mkukuta. JK akaanzisha BIG Results Now. Halfu JPM akatelekeza vyote.
Ngoja tuendelee kula mtori. Nyama tutazikuta chini. Ila kina sisi ni wazuri sana wa kuja na misemo na kiswahili kingi
 
Ilani ya Uchaguzi 2015 haikuwa na mradi wa bwawa la rufiji ila aliekuja kufanya alifanya kwa utashi wake na ndiyo maana walipinga walikuwa ndan hukohuko
 
Kawadanganye wajinga. Mitambo ya Kinyerezi inapata gesi only 6% ya uwezo wake.
Kinyerezi one Mega Watt 210 na Kinyerezi two Mega Watt 240 jumla Mega Watt 450.

Nchi nzima tuna wastani wa Mega Watt 1800 hivi.

Je, Mega Watt 450 ni asilimia 6 ya umeme wote unaozalishwa Tanzania?
 
Mtaongea kila kitu awamu hii ila sisi nasi tunaona na tunajua nani kafanya nini.

Uongo wenu hautawasaidia.
 
Kuna mradi wa kuzalisha kizazi cha watanzania wengi wajinga wanaomaliza darasa la saba pasipo kujua kusoma na kuandika ila wamefaulu mtihani wa drs la saba, mradi huo ulianza wakati wa bwana kikwete.
 

Magufuli aliwabrainwash watu wazito wa kufikiri, na alifanikiwa kwa kudhibiti vyombo vya habari ili vitangaze yale aliyopenda tu kuyasikia. Na kwakuwa wajinga ni wengi basi aliwapata. Wengi waliamini ndio nchi imeanza miradi wakati wake, na hakuna uwezekano wa chochote kufanyika baada yake. Wakati wake ndio kulianza sifa za kijinga kuwa fedha za umma ni za rais, na fedha ikitolewa ya umma, basi hiyo ni hisani ya rais maana fedha ni zake!
 
Sawa mkuu we ongelea hiyo mingine sisi watanzania tumeamua kuongelea aliyoifanya mwamba Magufuli
 
When did they plan to ditch out the project? Acheni hearsay na speculation hakukua na mpango wa kuacha mradi ule ilikua kelele za Mitandaoni tu ila ujenzi uliendelea kwa Kasi Ile ile.

Kama si kelele za mtandaoni na maombi ya wamatumbi mradi ungesimama au kucheleweshwa kwa makusudi, ni hivi uwa mnajisahaulisha. Si humu humu ndani nyie madalali wa kisiasa mlikuwa mnawasakama sukuma gang kuwa huo mradi ni white elephant project.

siasa chafu kuhusu mradi ule unaita hearsay na speculation blah blah. Kuchelewesha mradi kukamilika kwa makusidi unaita sio mipango?
 
Ni ushamba tu wa yeye na genge lake hakuna cha ajabu. Hizo reli na bomba la mafuta sio ishu, Nyerere alijenga reli na bomba mafuta kutoka Dar hadi KapiriMposhi Zambia na hakukuwa na kelele zozote.
 
Msoga alitumia miaka mingapi na JPM kwa miaka mingapi.

Ukituliza akili utagundua JPM ni habari nyingine.
 
Umeongea pumba na uongo wa maskani. Bwawa la Nyerere lipo kwenye Ilani ya CCM, ambayo iliandikwa kabla hata hajateuliwa (utaniambia vingapi vinaandikwa havitekelezwi). Kwani mradi wa njia 8 hadi Bagamoyo umetumia kiasi gani? Hivi ingekuwa akili kweli kujenga njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha huku watanzania lazima wapitie Kenya kwenda Mwanza? Au kwenda Mtwara kutoka Songea kupitia Dar? Au usijenge Daraja la Kilombero ili kuopitisha mchele ufike sokoni? Au usijenge Malagarasi? Jiulize kama umeme wa gesi ni asilimia 60 ya umeme wote, hali ingekuwaje kama wasingejenga bomba la gesi na kujenga kinyerezi gas plants na badala yake kujenga njia 8 za Kibaha. JPM alitamka hadharani kuwa bila yeye miradi aliyoanzisha haitamalizwa, Mungu fundi kamchukua, je kuna mradi wake uliosimama?

Fuatilia historia ya Morogoro road ndio utaona kuwa Kimara -Kibaha sio "specialized case". Kila Rais kaijenga hiyo barabara kulingana na mahitaji ya wakati husika. Tunachosema hapa sio kwamba JPM hakufanya kitu, la hapana. Alifanya kama watangulizi wake pia walifanya ila kuiona kama Tanzania ilianza na yeye, huo ndo uzezeta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…