Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Wote hawana haki bali wanatakiwa kwenda mahakamani mali igawanywe kwa hao ndugu. Mahari aliyetoa alishafariki hivyo ndugu wa mume hawana haki ya kusingizia mahari,mjane harithiwi mkuu
kwa nini azikwe moshi na siyo morogoro?
 
Wachaga Wachaga Wachaga kila kona ya ugomvi wa mirathi hawana hata aibu. Kule Bagamoyo wameenda kuzika ndugu yao hata mke hayupo! Huku nako wameenda kumzika Mpogoro Moshi ili tu wajimilikishe mali. KLyn wa Mengi wanamsumbua kama hawamjui vile. Yaaani hizi mtu kwenye mali ni FISI maaaaamae zao
 
M
Mbona hiyo kesi ipo wazi Sana ! Ni kwamba huyo Mama mali kaziendeleza baada ya kuwa kapata mgao wake wa urithi kwa mmewe so ndugu wa mume hawana Chao kwani mirathi ya ndugu yao ilikwishagawanywa alipofariki kilichopo ni Cha ndugu wa mke!
 
Ndugu wa mume Wanatumia mantiki gani kudai Mali ni zao?
Mjane ni mwanamke single. Kuzikwa Moshi au Dar hakumfanyi kuwa mke wenu.

Wanadai Mtu kuolewa maana yake ni kuhamishwa ukoo.

Ile mahari waliyopokea maana yake ni mwanamke anahama ukoo wake na kuhamia ukoo wa mume.

Ndio maana hata mwili wake wameenda kuuzika moshi alipozikwa mume wake na mwanae.

Sasa kama mwili wake umzikwa kwenye makaburi ya ukoo wao. Na hata mali zake zisimamiwe na ukoo huo huo uliomzika
 
Hawa kwanini walikubali azikwe moshi wakati wanasema ni wakwao
 
mwanamke kama alilipiwa mahari hao ndugu wa mwanamke hawana wanachodai kwa upande huo alioolewa huyo mwanamke. wanachotaka kufanya hakina tofauti na wizi
Hapa bado hujatoa suluhu maana kama Mume alishafariki, nyumba imejengwa na sasa Mume, Mama na Mtoto wote hawapo..ni nani huwa ndio '"next of kin?"

Hapa kama Mama hajaacha maandishi hakika ni mtihani.
 
Hapa bado hujatoa suluhu maana kama Mume alishafariki, nyumba imejengwa na sasa Mume, Mama na Mtoto wote hawapo..ni nani huwa ndio '"next of kin?"

Hapa kama Mama hajaacha maandishi hakika ni mtihani.

Huyo mjane kazikwa wapi?
Alipozikwa mjane ndipo wenye mamlaka na Mali za marehemu
 
Wote hawana haki mkuu, win win situation apo ni mjengo tu uuzwe wagawane fungu ila umasikini ni mbaya sana aloo
Hapana mkuu wagawane kwa misingi ipi wakati unaambiwa nyumba alijenga huyo mwanamke na wakati anajenga mme wake alikuwa ameshafariki.
Hao ndugu wa mme ni njaa tu zinawasumbua mbona jambo liko wazi kabisa hata mtoto wa chekechea anaweza kusuluhisha hiyo kesi.
 
Hapo hakuna cha malezi wala mchango,nyumba ni ya mwanamke aliyefariki hao ndugu wa mme wanahusika vipi hapo?ndugu wa huyo mke aliyekufa ndio wenye mamlaka na hiyo nyumba very simple
 
Kiwanja kilikua cha mume lakin kwa msingi huo wana haki na jasho la ndugu yao
 
Wazazi wa huyo mama Marehemu bado wapo? Kama wapo hao ndiyo warithi halali wa mali hizo!
 

Kiwanja alinunua mume enzi za uhai wake. Na kwenye mirathi ya mume hiko kiwanja alipewa mtoto wa huyo mama ambae ni ukoo wao pia. Ameshafariki wamezika kwao.
 
Uhalali upo sababu mume alitoa mahari na pia mwanae kazikwa hapo. Mfumo mnaoutetea ulishapitwa na wakati.
Kama ishu ni mahari wadai hiyo mahari walipwe lakini si nyumba.
Hiyo nyumba haiwahusu kivyovyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…