Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwa nini azikwe moshi na siyo morogoro?Wote hawana haki bali wanatakiwa kwenda mahakamani mali igawanywe kwa hao ndugu. Mahari aliyetoa alishafariki hivyo ndugu wa mume hawana haki ya kusingizia mahari,mjane harithiwi mkuu
kwa nini azikwe moshi na siyo morogoro?
Mbona hiyo kesi ipo wazi Sana ! Ni kwamba huyo Mama mali kaziendeleza baada ya kuwa kapata mgao wake wa urithi kwa mmewe so ndugu wa mume hawana Chao kwani mirathi ya ndugu yao ilikwishagawanywa alipofariki kilichopo ni Cha ndugu wa mke!Habari wadau.
Kama mnavyojua swala la mirathi linavyotolewa macho hapa Tanzania.
Jirani kwetu kuna mama amefariki na kuacha nyumba nzuri tu na hajaacha mtoto hata mmoja.
Historia ya huyu mama ( kabila mpogoro) mwaka 1991 aliolewa kwa ndoa ya kanisani na mume wake ( kabila mchaga)
Baada ya kufunga ndoa walinunua kiwanja na mume wake na kuzaa mtoto mmoja wa kiume.
Mwaka 1994 mume wa huyu mama alifariki na kumuacha mke na mtoto mmoja wakiwa hai.
Taratibu za mirathi ya mume wake zilifanyika baada ya msiba. Mama na huyo mwanae wakapewa hiko kiwanja maeneo ya tegeta kikiwa kitupu hakijaanzwa ujenzi wowote.
Maisha yakaendelea. Mama huyu hakuolewa tena . Aliendelea kuishi na mwanae kwa kupanga nyumba ya NHC keko. Na mdogo mdogo akaanza ujenzi wa nyumba katika kiwanja walichoachiwa na mumewe.
Alijenga nyumba nzuri tu ya kisasa. Na zingine ndogo ndogo pembeni za kupangisha. Maana kiwanja kilikuwa kikubwa sana ( maana enzi wananunua tegeta ilikuwa pori ardhi haina thamani miaka ya 90 muuzaji anakuuzia bonge la kiwanja kwa bei ndogoo..)
Baada ya kumaliza ujenzi yeye na mwanae waliendelea kuishi nyumba ya NHC na kule tegeta walipojenga wakapangisha wapangaji kadhaa.
Mwaka 2015 mama alipata msiba mwingine wa kufiwa na mtoto wake huyo mmoja kwa ajali ya gari na hii ikamfanya mama kubaki peke yake bila mtoto wala mume.
Mama akaendelea kuishi mwenyewe mpaka na yeye mama alipofariki mwaka huu mwanzoni.
Mwili wa mama ulisafirishwa kwenda moshi kuzikwa walipozikwa mume wake na mwanae.
Shida imekuja kwenye nyumba zilizojengwa na huyo mama. Ukoo wa mume unasema ni mali zao. Na ukoo wa mke nao unasema ni mali zao maana zimejengwa kipindi mume wa huyo mama ameshafariki.
Wataalamu wa mirathi Kesi kama hii upande upi kati ya ukoo wa mume na ukoo wa mume una haki ya kurithi hizo mali za huyu mama
Ndugu wa mume Wanatumia mantiki gani kudai Mali ni zao?
Mjane ni mwanamke single. Kuzikwa Moshi au Dar hakumfanyi kuwa mke wenu.
Hawa kwanini walikubali azikwe moshi wakati wanasema ni wakwaoWanadai Mtu kuolewa maana yake ni kuhamishwa ukoo.
Ile mahari waliyopokea maana yake ni mwanamke anahama ukoo wake na kuhamia ukoo wa mume.
Ndio maana hata mwili wake wameenda kuuzika moshi alipozikwa mume wake na mwanae.
Sasa kama mwili wake umzikwa kwenye makaburi ya ukoo wao. Na hata mali zake zisimamiwe na ukoo huo huo uliomzika
Hapa bado hujatoa suluhu maana kama Mume alishafariki, nyumba imejengwa na sasa Mume, Mama na Mtoto wote hawapo..ni nani huwa ndio '"next of kin?"mwanamke kama alilipiwa mahari hao ndugu wa mwanamke hawana wanachodai kwa upande huo alioolewa huyo mwanamke. wanachotaka kufanya hakina tofauti na wizi
Uhalali upo sababu mume alitoa mahari na pia mwanae kazikwa hapo. Mfumo mnaoutetea ulishapitwa na wakati.
Hapa bado hujatoa suluhu maana kama Mume alishafariki, nyumba imejengwa na sasa Mume, Mama na Mtoto wote hawapo..ni nani huwa ndio '"next of kin?"
Hapa kama Mama hajaacha maandishi hakika ni mtihani.
Hapana mkuu wagawane kwa misingi ipi wakati unaambiwa nyumba alijenga huyo mwanamke na wakati anajenga mme wake alikuwa ameshafariki.Wote hawana haki mkuu, win win situation apo ni mjengo tu uuzwe wagawane fungu ila umasikini ni mbaya sana aloo
Hapo hakuna cha malezi wala mchango,nyumba ni ya mwanamke aliyefariki hao ndugu wa mme wanahusika vipi hapo?ndugu wa huyo mke aliyekufa ndio wenye mamlaka na hiyo nyumba very simplemimi sijui kabisa sheria lakini kuna maswali ya machache ya kujiuliza?
na mengine mengi mwisho wa siku busara inaweza kutumika kwa familia zote mbili kugawana wakipata ratio ya 2:3
- je baada ya mume wa marehemu kufariki nini kiliamliwa kwenye miradhi
- kama mke alikubali kuwa mjane na atabaki kama mwanafamilia je wanafamilia walihusika vipi na malezi ya mtoto wa ndugu yao?
- mawasiliano yalikuwaje kati ya familia iliyooa na mjane wakati wa uhai wake?
- Je walikuwa na mchango wowote
Kwa hiyo zitakuwa chini ya nani haswa au ni ukoo mzima?.Huyo mjane kazikwa wapi?
Alipozikwa mjane ndipo wenye mamlaka na Mali za marehemu
Kiwanja kilikua cha mume lakin kwa msingi huo wana haki na jasho la ndugu yaoHapana mkuu wagawane kwa misingi ipi wakati unaambiwa nyumba alijenga huyo mwanamke na wakati anajenga mme wake alikuwa ameshafariki.
Hao ndugu wa mme ni njaa tu zinawasumbua mbona jambo liko wazi kabisa hata mtoto wa chekechea anaweza kusuluhisha hiyo kesi.
Hapana mkuu wagawane kwa misingi ipi wakati unaambiwa nyumba alijenga huyo mwanamke na wakati anajenga mme wake alikuwa ameshafariki.
Hao ndugu wa mme ni njaa tu zinawasumbua mbona jambo liko wazi kabisa hata mtoto wa chekechea anaweza kusuluhisha hiyo kesi.
Wazazi wa huyo mama Marehemu bado wapo? Kama wapo hao ndiyo warithi halali wa mali hizo!
Kama ishu ni mahari wadai hiyo mahari walipwe lakini si nyumba.Uhalali upo sababu mume alitoa mahari na pia mwanae kazikwa hapo. Mfumo mnaoutetea ulishapitwa na wakati.
Hili ndio jibu sahihi,hakuna mambo mengi hapohapo mirathi itakwenda kwa NDUGU WA MAREHEMU