Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Kiislam ni rahisi sana.

Baada ya mume kufariki, mgao wa mirathi unafanyika; ambapo mke, mtoto na wazazi wa marehemu (ambao kisheria ndio warithi) kila mmoja anapata fungu lake.

Baada ya hapo kinachoendelea kwa upande wa mjane wa marehemu ikitokea akafariki; warithi wake ni ndugu zake kama hana mtoto wala wazazi!
 
Baada ya kifo cha mume mirathi iligawanywa. Mama napata shamba huko tegeta.mama hakutaka kuolewa lakini sheria ilimruhusu kuolewa.mama kuendeleza urithi wake .sasa yeye kafa mali hiyo wanarithi ndugu zake automatic Maana undugu na Wachagga ulishaisha. Kifo ndiyo kitemnganisho cha ndoa. Hivyo ndoa ilishavunjika na Bi mkubwa alikuwa na vyake hivyo wenye haki ya kurithi ni ndugu zake .
 
Kuna jamii mwanamke akilipiwa mahari anakuwa mali ya ukoo wa mume!

Inasikitisha!
 
Kiwango chako cha elimu tafadhali sana??
Ndoa ya kanisani binti anatoka kwao na kuingia kwenye ukoo wa mume, maadam si ya kiislamu mume akifariki mke anabaki kwenye ukoo wa mume ndiyo sababu ukoo wa mke ulikubali akazikwe Moshi na ukoo wa mume uliridhia kwa sababu ni mke wao, kama wasingeoana kanisani wasingekubali azikwe kwao.
Tatizo hapa kunamitazamo miwili, wakiislamu na wakikristu huku waislamu wanavutia upande wao kwenye ndoa ya wakristu!
 
Eleza ni kigezo kipi kilitumika akazikwe kwa aliyekuwa mume wake huku si kwao!
 
Hili ni swali tu;..
Hivi kama mke wa marehemu angetaka kuolewa tena na mwanaume mwingine ingekuwaje...?

Nani angepokea mahari, wazazi wake au watu wa ukoo wa marehemu mumewe 'alikohamia'..?!
 
Kiislam, nyumba na mali zote ni za huyo mama. Wanaomrithi ni ndugu zake na anapokuwa hana wa kumrithi, yaani hajaacha hata ndugu, zinakuwa mali za wakf ya Waislam kama vile msikiti wa jirani hapo au atavyoamuwa kadhi.
 
Hili ni swali tu;..
Hivi kama mke wa marehemu angetaka kuolewa tena na mwanaume mwingine ingekuwaje...?

Nani angepokea mahari, wazazi wake au watu wa ukoo wa marehemu mumewe 'alikohamia'..?!
Asingeolewa ndani ya kanisa na bado wakwe wanaweza kuweka pingamizi, ndoa ya kanisani ni pingu ya maisha.
 
Wa upande wa mume wapewe pesa nusu ya thamani ya kiwanja tu. Ila nyumba zilizojengwa haziwahusu.
 
Eleza ni kigezo kipi kilitumika akazikwe kwa aliyekuwa mume wake huku si kwao!
Maiti inaweza kuzikwa mahali popote pale na mazishi kufanywa na mtu yoyote yule, na suala hili wala halina uhusiano wowote ule kwa wazikaji kuwa na uhalali wa kurithi mali za marehemu aliyezikwa.
 
Ukoo upande wa mume watafute ndugu wa huyo mume atawale hizo mali. Hakuna majadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…