Kuanzia uvaaji, nidhamu ya ibada hadi swala la kuzingatia muda maaskofu wa Katoliki wako vizuri.
Nimesikiliza mahubiri ya mhashamu baba askofu Ngalale Kumtwa hayakuwa na mbwembwe wala malalamishi bali yalijaa busara, hekima na upendo.
Kiukweli ipo tofauti ya kutosha kabisa baina ya maaskofu wa haya makanisa rasmi na wale wa Huduma za kiroho.
Nawatakia Dominica yenye baraka!
Ewe mu roman-katoliki, pole sana kwa kudanganywa na kuwa sehemu ya mafundisho ya uongo ya kanisa lenu la kirumi.
1. Kanisa rasmi kwa kutumia maneno yako, haliwezi kuwa kanisa lenu la kirumi, wala la kiingereza~Anglican wala la wajerumani~Lutheran, wala lolote unalolifaham lililoundwa kwa vikao vya wanadam waliokaa na kuamua namna gani wamwabudu Mungu, bali kanisa rasmi ni KANISA LA KRISTO alilolianzisha kwa neno lake mwenyewe. Soma
Math 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
2. Imeandikwa, pia Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Kuheshimu kwa midomo ni ile hali ya kusema hbr za Kristo. Fine. Lkn huamini chochote/ au unaamini kwa sehemu kuhusu habari za Kristo. Mfano, unaamini hbr za ubatizo, lkn ubatizo gani? Hapo kwa sehemu inakutesa.
Kuabudu bure na kufundisha maagizo ya wanadamu, ni pale mnapofanya ambayo hayajaelekezwa kwenye biblia. Mmetunga taratibu zenu wenyewe za ibada na kuagiza watu wazifuate. Mfano, ubatizo wa watoto, ubatizo wa kunyunyiza, sala za maria, matumizi ya rozari, na meeengi mnayofundishana, kwenye biblia hutayaona, mmetunga wenyewe.
3. Mmiliki wa kanisa, ni Kristo mwenyewe. Alisema kanisa langu, ni moja hajawahi kusema makanisa yangu.
Kuwa mrumi, mwa anglican, mruther, mu full gospel, mu ufufuo na uzima, mu tag, fpct, batist n.k, maana yake umekubali kufuata mafundisho ya waanzilishi wa madhehebu hayo. Ndiyo maana pamoja na yote kumtaja Kristo, lkn mafundisho na aina ya ibada zao wanatofautiana. Yote hayo Mungu ameyakataza.
Soma 1kor 1:10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Hayo maswali yanawahusu ninyi na madhebu yenu. Ni sawa na kuuliza, ulibatizwa kwa jina la RC? Au Anglican alikufa kwa ajili yako? Au FPCT alikufa kwa ajili yako? Nk.
Ndugu yangu, neno linasema "...na milango ya kuzimu haitalishinda...". Pamoja na fitina za kila namna zilizofanywa na warumi-RC, kuua, kutesa, kubagua, kutweza WAKRISTO waliopokea injili kwa Kristo na waliokuwa kwenye utume kama walivyoagizwa, "... enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa, ataokoka". Fitina hizo hazikumaliza wakristo, hazikuua kanisa la Kristo, liliendelea, linaendelea na litaendelea. Hakuna milango/madhehebu yatakayo lishinda kanisa la Bwana. Yesu na kanisa lake watabaki hata kama wamezungwa na wapingaji kama nyie.
Nakualika uje ujifunze hbr za Kristo, uanze kuabudu unachokijua tena kilicho sahihi, uachane na hizo misa zilizotungwa na wanadamu. Siyo vitu vya kujivujia.