Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Misa ya Mkapa: Nimeona tofauti kubwa kati ya maaskofu wa Katoliki na wale wa makanisa kama la Gwajima!

Acha kujibaraguza unanifahamu. Rudi shule ulikotoroka ukajifunze Kiswahili badala ya kupoteza muda humu kuandika upuuzi.

Jitizame una kadudu kaina gan mwilin mwako ,hiyo ndio ela
 
Mshana naomba ufafanuzi. Nimetamani kuelewa ila nimeshindwa.

Ile zawadi ya tausi wale, wale, wale! Nje ya maagano ya mbio za mwenge wa uhuru, ni balaa tupu, ni misiba baada ya misiba. Ingawaje ni " consipiracy theory" bali yanayokwenda kutokea ni kifo rasmi ya chama tawala[emoji2958][emoji41][emoji848][emoji851]

Jr[emoji769]
 
Acha kujibaraguza unanifahamu. Rudi shule ulikotoroka ukajifunze Kiswahili badala ya kupoteza muda humu kuandika upuuzi.
Nilipie Ada narudi shule kiroho Safi ,vinginevyo ntaendelea kupoteza mda umu umu ,
 
Acha kujibaraguza unanifahamu. Rudi shule ulikotoroka ukajifunze Kiswahili badala ya kupoteza muda humu kuandika upuuzi.
Na mpak ujuwe sijuw kiswahili Ina maana umenielewa nilicho maanisha ,Wala unisumbui ilo
 
Acha kujibaraguza unanifahamu. Rudi shule ulikotoroka ukajifunze Kiswahili badala ya kupoteza muda humu kuandika upuuzi.
Na kujua kiswahili chako na mm nisie jua ,tunachati ,umeona elimu aina umuhimu Sana ishu ujuwe kusoma na kuandika tu
 
Kwa ufinyu wa akili yako. Kama unadhani kujua kusoma na kuandika ndiyo mwisho wa dunia KALAGA BAHO ungekuwa unajua kusoma na kuandika usingeandika ELA. Rudi shule UKAFUTE UJINGA.

Na kujua kiswahili chako na mm nisie jua ,tunachati ,umeona elimu aina umuhimu Sana ishu ujuwe kusoma na kuandika tu
 
Kwa ufinyu wa akili yako. Kama unadhani kujua kusoma na kuandika ndiyo mwisho wa dunia KALAGA BAHO ungekuwa unajua kusoma na kuandika usingeandika ELA. Rudi shule UKAFUTE UJINGA.
Nimeamin wewe ndo ujuwi kusoma ulitaka niandike nini Sasa? Na mashaka na wewe uwenda ukawa mjumbe umekula jasho la mtu lina kuleta maruwe ruwe
 
Kwa ufinyu wa akili yako. Kama unadhani kujua kusoma na kuandika ndiyo mwisho wa dunia KALAGA BAHO ungekuwa unajua kusoma na kuandika usingeandika ELA. Rudi shule UKAFUTE UJINGA.
Alf vijitu vilivyo soma kayumba na kuenda kwa Ras Simba Wana shida sana
 
Hapa upo sahihi, kabisa,kuna kipindi hata Mimi nikiingia kwenye haya makanisa ya wokovu kipindi çha shida,Na nilikikuta moyo unanirudisha katika imani yangu ya kikatoliki,kwani kule kwenye baadhi ya makanisa ya wokovu nilijikuta naanza kujenga chuki Na baadhi ya watu Na kuwa Mtu mwenye wasiwasi zaidi licha ya kunipa uwezo zaid wa kila muda kusali Na kukemea, Tofauti nilizoziona........kikatoliki unakufundisha kumshukuru mungu wakati wote Na kuyapinga maovu baasi. Ila uku kwenye baadhi ya makanisa nadhani haya ya kisasa unawekewa zaidi namna ya kumtafuta adui yako Na kutengeneza hisia za Nani anakuloga au anakuchezea, kubadili akili Na kuwaza namna ya kutajilika kupata Magari Na kujenga nyumba, yaani aitofautiani Na ramli Na waganga,namna ya kucheza Na ndoto,ukiota jirani yako,Mara moja unaanza kumuhisi kitu anakufanyia,yaani taflani Na maisha haikushuki
Tuzidi kumwomba mungu hatuepushe Na baadhi ya balaa za kidunia,
Ni baadhi ya makanisa ya kisasa au ya wokovu
Kama ntakuwa nimemkwaza Mtu labda imemgusa tafadhari anisamehe,sababu uwa sipendi kujadili Imani za watu,ili mradi Amani itawale tujithamini Na kupendana,
Tamati
Utajiri utaupata kwa juhudi zako bila kumdhuru binaadamu mwenzako,huku ukimtanguliza mbele mungu wako,
Wasiwasi wako ndo uoga wako usimsingizie binaadamu mwenzako
Hakikisha Na upate ukweli usitengeneze uoga katika nafsi yako
Tengeneza amani popote pale unapooenda Na ujiamini, kamwe hautopata shida ya kutishwa Na kitu chochote Na unaweza kujikuta umepambana Na kitu usichoamini kama ulikuwa Na uwezo wa kukishinda,
JIamini Na unaweza,kwa kuweka imani yako mbele kwamba unaweza usijivunje moyo,
 
Kanisa katoliki ni kanisa makini katika nyanja zote na kwa umakini wake waumini wake wananufaika sana kwa kupata mafunzo ya kiimani kutoka kwa viongozi makini.Jambo linalosaidia sana kuiimarisha imani za waumini wakatoliki ulimwenguni pote!
Pia NI kanisa ambalo lina bwege 1 anayejiita mwakilishi wa Mungu duniani na maboya humwita baba mtakatifu
 
Pia NI kanisa ambalo lina bwege 1 anayejiita mwakilishi wa Mungu duniani na maboya humwita baba mtakatifu
Hapana.Mafundisho yanafundisha kuwa papa si mwakilishi wa Mungu duniani bali ni Khaifa wa mtume Petro.
Mathayo 8:13
Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.

Petro ndiye aliyekabidhiwa mamlaka hayo kutoka kwa Kristu Yesu mwenyewe ili kuliongoza kanisa lake.Petro amekabidhiwa funguo za mamlaka anaweza kufunga na kufungua jambo duniani na mbinguni ikawa hivyo.Baada ya Petro ambaye ndiye papa wa kwanza kabisa na kiongozi wa kanisa la Yesu kanisa limeendeleza utaratibu wa kiti cha Petro ili kuchunga na kulinda kondoo wa bwana.

Yn 21:15-25

Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

Sote tu mashahidi juu ya kazi kubwa ya kitume inayofanywa na papa dunia nzima katika kumtangaza Kristu na kuhubiri ujumbe wake.Mfano Papa Yohane Paulo II alizunguka nchi nyingi sana duniani na kote alipofika alitangaza na kuhubiri ujumbe wa Yesu kuhusu amani.Papa ni mpatanishi na msuluhishi wa migogoro mingi iliyo na inayotokea duniani.Kazi hizi ni ishara wazi kuwa yeye amekabidhiwa mamlaka na msalaba kama alivyokabidhiwa Petro katika kuendelea kuchunga kondoo wa Bwana.
 
Kuanzia uvaaji, nidhamu ya ibada hadi swala la kuzingatia muda maaskofu wa Katoliki wako vizuri.

Nimesikiliza mahubiri ya mhashamu baba askofu Ngalale Kumtwa hayakuwa na mbwembwe wala malalamishi bali yalijaa busara, hekima na upendo.

Kiukweli ipo tofauti ya kutosha kabisa baina ya maaskofu wa haya makanisa rasmi na wale wa Huduma za kiroho.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Ewe mu roman-katoliki, pole sana kwa kudanganywa na kuwa sehemu ya mafundisho ya uongo ya kanisa lenu la kirumi.

1. Kanisa rasmi kwa kutumia maneno yako, haliwezi kuwa kanisa lenu la kirumi, wala la kiingereza~Anglican wala la wajerumani~Lutheran, wala lolote unalolifaham lililoundwa kwa vikao vya wanadam waliokaa na kuamua namna gani wamwabudu Mungu, bali kanisa rasmi ni KANISA LA KRISTO alilolianzisha kwa neno lake mwenyewe. Soma

Math 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

2. Imeandikwa, pia Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Kuheshimu kwa midomo ni ile hali ya kusema hbr za Kristo. Fine. Lkn huamini chochote/ au unaamini kwa sehemu kuhusu habari za Kristo. Mfano, unaamini hbr za ubatizo, lkn ubatizo gani? Hapo kwa sehemu inakutesa.

Kuabudu bure na kufundisha maagizo ya wanadamu, ni pale mnapofanya ambayo hayajaelekezwa kwenye biblia. Mmetunga taratibu zenu wenyewe za ibada na kuagiza watu wazifuate. Mfano, ubatizo wa watoto, ubatizo wa kunyunyiza, sala za maria, matumizi ya rozari, na meeengi mnayofundishana, kwenye biblia hutayaona, mmetunga wenyewe.

3. Mmiliki wa kanisa, ni Kristo mwenyewe. Alisema kanisa langu, ni moja hajawahi kusema makanisa yangu.

Kuwa mrumi, mwa anglican, mruther, mu full gospel, mu ufufuo na uzima, mu tag, fpct, batist n.k, maana yake umekubali kufuata mafundisho ya waanzilishi wa madhehebu hayo. Ndiyo maana pamoja na yote kumtaja Kristo, lkn mafundisho na aina ya ibada zao wanatofautiana. Yote hayo Mungu ameyakataza.

Soma 1kor 1:10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Hayo maswali yanawahusu ninyi na madhebu yenu. Ni sawa na kuuliza, ulibatizwa kwa jina la RC? Au Anglican alikufa kwa ajili yako? Au FPCT alikufa kwa ajili yako? Nk.

Ndugu yangu, neno linasema "...na milango ya kuzimu haitalishinda...". Pamoja na fitina za kila namna zilizofanywa na warumi-RC, kuua, kutesa, kubagua, kutweza WAKRISTO waliopokea injili kwa Kristo na waliokuwa kwenye utume kama walivyoagizwa, "... enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, aaminiye na kubatizwa, ataokoka". Fitina hizo hazikumaliza wakristo, hazikuua kanisa la Kristo, liliendelea, linaendelea na litaendelea. Hakuna milango/madhehebu yatakayo lishinda kanisa la Bwana. Yesu na kanisa lake watabaki hata kama wamezungwa na wapingaji kama nyie.

Nakualika uje ujifunze hbr za Kristo, uanze kuabudu unachokijua tena kilicho sahihi, uachane na hizo misa zilizotungwa na wanadamu. Siyo vitu vya kujivujia.
 
Haya bana sie Waanglicana sijui tunakaa wapi?
Nyote ni kundi moja la mafundisho ya upotofu, yaliyotungwa na wanadamu. Walianza kukosea waroman katoliki, wakafundisha upotofu, baadae King Henry wa viii wa uingereza akakosa mtoto wa kiume, ili kulinda ufalme wake, akaoa mke wa pili, kanisa la roman wakamtenga, hivyo yeye akaanzisha kanisa la waingereza. Ndiyo maana kwa baadhi ya maeneo, hakuna tofauti ya ibada za waroma na waanglican/waingereza, wako sawa. Kwa Tanzania, kuna high church na low church. Waanglican wa kuanzia dodoma, hawawezi kusali misa za anglican ya pwani.

Lkn nyoote mnafundishana mapotofu, yaliyo mmaagizo ya wanadamu
 
Back
Top Bottom