Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Hii misafara iwe inatolewa taarifa kama zile za utabiri wa hali ya hewa, walau ukisikia kuna Mh atakuwa mahali fulani Mtu utafute option nyingine, kama kuna barabara mbadala basi upitie huko.

Kuna siku tumesimamiswa tukiwa kwenye basi kwenda Dar, maeneo ya Tanga, kuuliza uliza kumbe kulikuwa na Mh ametembelea Tanga wakati huo....inakera maana hata utaratibu wa kuchimba dawa kwenye maeneo maalum unavurugika na Abiria wanalazimika "kurutubisha" mapori yaliyo jirani nao kwa wakati huo.

Ona Vladmir Putin anavyojichanganya asipotezee Watu muda, labda yeye ni muumini wa "muda ni pesa".
 
Inakera sana,kuna siku niliganda pale Tazara Massa 2 bila sababu ya msingi,anayetusubilisha ndiyo kwanza alikuwa anahutubia Mwanza.

Sikulaumu ila nikaconclude kuwa kweli sisi ni dunia ya tatu
Mkuu ngoja nitafute mtu anishikilie nicheke 🀣
Stop wa Tazara anaetaka kupita anahutubia Mwz πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ‘πŸ‘ pole sana mkuu!
Ukiongeza na sifa wazipendazo maaskari full hasira pa kusemea napo hamna labda humu!

Last week naenda Biharamulo ikapigwa stop pale Bwanga kuuliza naambiwa mukubwa yupo Kahama anahutubia kisha anakuja atapita hapo baadae kwenda Chattle. Nikashuka kwenda kuwaeleza traffick niendako waniruhusu hawakutaka na kulikuwa hakuna magari ni kama vile kwangu ndo walianzia stop!
Aiseeh toka saa 9jioni kaja kupita saa 1jioni. Sio siri hili jambo lifikiriwe na lijadiliwe upya, muda ni jambo la KUHESHIMU kama kweli tunahitaji kusonga mbele. Thanx PASCAL.
 
Pamoja na hayo huoni hicho kipato cha $2000 kitazidi kushuka kwa kusuburi mukubwa apite? Lakini kama jeshi linathibitisha usalama kwa sasa ni mkubwa hofu ya nini?
Kwanza kimya kimya ni nzuri kuliko taharuki!
 
Pole sana,ndiyo hali halisi yenyewe hiyo inakera sana
 
Hatuwezi kuiga ya Sweden kwa sababu kadhaa.
Hatuna miundombinu ya kuwezesha watekeleze hayo mafunzo. Hilo ndiyo kubwa.
Mfumo wetu wa kulinda viongozi ni tofauti mno. Upo based kwenye yoga - real or assumed. Magari ni mengi mno. Tuna exaggerate mno precautions.
 
Weupe Weupe tu...Hao wenye Rollers waliovuka ingekuwa huku.Wangetaga mayai
 
Pamoja na hayo huoni hicho kipato cha $2000 kitazidi kushuka kwa kusuburi mukubwa apite? Lakini kama jeshi linathibitisha usalama kwa sasa ni mkubwa hofu ya nini?
Kwanza kimya kimya ni nzuri kuliko taharuki!


Kila nchi inalinda Viongozi wake asikudanganye mtu hata huko Sweden sema hauoni kwa sababu wana options nyingi, wana pesa ya kuweza kufanya mengi.
Wana public transportation imara unaweza kupanda treni, subways, tramway system, n.k.

Bajeti ya Jeshi la Polisi peke yake huenda ikawa sawa na Bajeti ya JMTZ ya kuhudumua > milioni 45, isitoshe ni jukumu lao kuhakikisha Viongozi wa nchi wako salama sasa huo Usalama unafanikishwa vipi inategemeana na rasilimali zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…