Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,041
- 13,907
Muwe mnapita na kwenye flyovers...msipende kulalamika saaana..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu ngoja nitafute mtu anishikilie nicheke 🤣Inakera sana,kuna siku niliganda pale Tazara Massa 2 bila sababu ya msingi,anayetusubilisha ndiyo kwanza alikuwa anahutubia Mwanza.
Sikulaumu ila nikaconclude kuwa kweli sisi ni dunia ya tatu
Wewe hata ukichelewa una faida gani??Kawaambie wenzako mzee baba "time is moniii"
Jifunze kuheshimu mamlaka
Pamoja na hayo huoni hicho kipato cha $2000 kitazidi kushuka kwa kusuburi mukubwa apite? Lakini kama jeshi linathibitisha usalama kwa sasa ni mkubwa hofu ya nini?Sidhani kama in sawa kumlaumu Mkuu wa Polisi na kumtaka kupeleka Polisi Sweden kujifunza zingatia hili labda unapotaka kulinganisha;
Sweden per capital income > 50 000 USD.
TZ yetu per capital < 2 000 USD
Sasa unawezaje kulinganisha hizo nchi mbili, Uchumi wa Sweden > 500 Billion USD idadi ya watu 10 million vs TZ yetu ukubwa wa uchumi < 80 Billion Idadi ya watu > 45 million.
Hivyo majibu yote yako hapo na hakuna kitu IGP atafanya usifikiri hawajui cha kufanya, wanajua ila wana limitations wakati huo huo ni jukumu lao kuhakikisha Usalama wa Viongozi, wanaweza hata wakawasafirisha kwa helikopta lkn who pays? Unaongelea nchi ambayo hata magari ya Polisi tunapewa msaada na hata kuweka mafuta tu wakati mwingine ni ishu, ...
Wewe ukiwahi una faida gani kwa mfano??Wewe hata ukichelewa una faida gani??
Pole dada..Wanaoniumizaga zaidi katika maisha haya ni wajinga wachache kama wewe tunaoishi pamoja. Ninyi mnaumiza kuliko viongozi wenyewe
Pole sana,ndiyo hali halisi yenyewe hiyo inakera sanaMkuu ngoja nitafute mtu anishikilie nicheke 🤣
Stop wa Tazara anaetaka kupita anahutubia Mwz 🤣🤣🤣🤣👏👏 pole sana mkuu!
Ukiongeza na sifa wazipendazo maaskari full hasira pa kusemea napo hamna labda humu!
Last week naenda Biharamulo ikapigwa stop pale Bwanga kuuliza naambiwa mukubwa yupo Kahama anahutubia kisha anakuja atapita hapo baadae kwenda Chattle. Nikashuka kwenda kuwaeleza traffick niendako waniruhusu hawakutaka na kulikuwa hakuna magari ni kama vile kwangu ndo walianzia stop!
Aiseeh toka saa 9jioni kaja kupita saa 1jioni. Sio siri hili jambo lifikiriwe na lijadiliwe upya, muda ni jambo la KUHESHIMU kama kweli tunahitaji kusonga mbele. Thanx PASCAL.
Hatuwezi kuiga ya Sweden kwa sababu kadhaa.Wanabodi,
Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.
Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.
Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.
Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.
Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda.
P
Kila mtu akijua ile gari ndani kuna mtu mzito (yupo foleni) wanaweza isogelea waizonge hadi wamuone.Ungesema je kwa Mabeberu kiongozi wa nchi anapopita huwa anaunga foleni na yeye ili na sisi tujifunze
Ila Kumbuka jamii yetu bado tupo nyuma kwa kifupi hatujastaarabika.
Beberu mweusi [emoji23][emoji23][emoji23]Huo muda mchache sana njia ya kwenda mikoani huwa inafungwa hadi masaa ma 5 mnamsubiria beberu wa kiafrika apite.
Hii misafara iwe inatolewa taarifa kama zile za utabiri wa hali ya hewa, walau ukisikia kuna Mh atakuwa mahali fulani Mtu utafute option nyingine, kama kuna barabara mbadala basi upitie huko.
Kuna siku tumesimamiswa tukiwa kwenye basi kwenda Dar, maeneo ya Tanga, kuuliza uliza kumbe kulikuwa na Mh ametembelea Tanga wakati huo....inakera maana hata utaratibu wa kuchimba dawa kwenye maeneo maalum unavurugika na Abiria wanalazimika "kurutubisha" mapori yaliyo jirani nao kwa wakati huo.
Ona Vladmir Putin anavyojichanganya asipotezee Watu muda, labda yeye ni muumini wa "muda ni pesa".
Pamoja na hayo huoni hicho kipato cha $2000 kitazidi kushuka kwa kusuburi mukubwa apite? Lakini kama jeshi linathibitisha usalama kwa sasa ni mkubwa hofu ya nini?
Kwanza kimya kimya ni nzuri kuliko taharuki!
Jifunze kuheshimu mamlaka
Au ajifunze kuto-reason mambo, yaani ubongo wake aufungie kabatini kama wewe.