Wanabodi,
Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.
Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.
Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.
Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.
Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda.
P