Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Hii siku ilitesa watu sana. Msamvu ilisimama tangu saa 12 asbh mabasi yaliondoka saa tano.. Kuna umuhimu wa kufanya hii misafara isitese watu.
Uko sawa kabisa. Juzi juzi wakati Mhe. Rais anaenda Dodoma kwa njia ya barabara magari yaliyokuwa yanatokea Dar kwenda Mikoani kwa njia ya barabara ya Morogoro yalimamishwa tangu saa kumi na mbili asubuhi lakini Mhe. Rais alipita njia hiyo mnamo saa tano asubuhi. Hii ni kuwatesa wananchi. Kweli time is money.
 
Mkuu Pascal kulaumu traffic wetu na Sirro ni kazi bule ,utawala wa awamu hii unapenda misafala ya ndani zaidi wakati awamu iliyopita ilipenda misafala ya nje. Sirro na traffic wake wanapewa amri tu ya kusafisha njia na kama unavyo jua amri toka juu za awamu zinavyotisha...😀😀😀
 
Hii siku ilitesa watu sana. Msamvu ilisimama tangu saa 12 asbh mabasi yaliondoka saa tano.. Kuna umuhimu wa kufanya hii misafara isitese watu.
Chakushangaza msafara unagar zaid ya 10na pikipiki lkn bado watu wanawacwac
 
Wanabodi,

Ukiondoa thamani ya uhai, hakuna kitu kingine duniani chenye thamani kama muda, time is money, kupotezeana muda ni kuzorotesha maendeleo.

Niko njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, tumesimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani anatokea njia ya Bagamoyo.

Huku kusimamishana babarani nusu saa nzima, kisa anapita kiongozi, ilikuwa ni zile enzi za ujima, kwenye dunia ya sasa ya the age of information science, unamsimamisha mtu dakika 30 kupisha msafara wa kiongozi ni kupotezaana muda. Wengine kazi zetu zina very tight deadlines, kama zilivyo tender deadlines, umechelewa hata dakika moja, imekula kwako.

Ndio maana sisi tunawasisitiza viongozi wetu, wasiopenda kusafiri nchi za watu kwa lengo la kubana matumizi, mara moja moja wasafiri tuu kwenda nchi za Ulaya na Amerika, sio kwa ajili ya kwenda kuponda raha, au kubembea hewani kwa kukwea pipa bali kusafiri ili kwenda kupata tuu exposure, wenzetu wakoje na wanafanyaje mambo yao.

Kwa hili la misafara ya viongozi ya kupotezeana muda, namshauri Afande IGP, Kamanda Sirro, amchukue Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akafanye ziara ya kimafunzo nchini Sweden aone misafara ya viongozi wa wenzetu wanaojali muda.

P
Point, na tupate definition ya kiongozi ni nani. Kuwe na viongozi wawili tu kitaifa wenye motorcade na outriders
 
Usalama wa viongozi hususani no.1 ni wa lazima. Nashauri polisi na vyombo usalama watumie tekinolojia zaidi.Wanavyotoa muda mwingi alert ni hatari zaidi. dakika 10 zinatosha safisha njia.
 
Hakika inachosha tena haswa hii njia ya posta-airport (gongo la mboto) aisee inawaumiza sana watu wanaotoka njia ya ilala kwenda veta.
Unakuta mtu umetoka mikochen labda unaenda mbagala, ukifika pale mataa ya veta unaweza ganda pale hata kwa 2 hours kupisha hawa wanatoka na kwenda njia ya airport.
So disguisting kwakwel
 
Back
Top Bottom