Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Apite kushoto mi niendelee kumwaga moto upande wa kulia. Nchi ina amani sana hii.
 
Kuna siku nikuwa natoka Buza asubuhi naelekea Posta aiseee.Kufika mataa ya Keko aiseee tulisimamishwa ili msafara wa kiongozi upite yaani magari yamekuja kuruhusiwa saa 2:45 yaani tangu saa 1 tupo pale.
 
Alichoelezea Pascal Mayalla hakina uhusiano na utajiri wa nchi. Hizo hizo pikipiki tulizonazo zikitumiwa vizuri zinatosha, tena na kubaki.
 
Ungesema je kwa Mabeberu kiongozi wa nchi anapopita huwa anaunga foleni na yeye ili na sisi tujifunze

Ila Kumbuka jamii yetu bado tupo nyuma kwa kifupi hatujastaarabika.
Kwa hiyo mnatuchukulia kuwa hatujastaarabika ndiyo maana mnatufanyia mambo ya kishenzi? Usituingize huko mkuu, wengine tumestaarabika.
 
Alichoelezea Pascal Mayalla hakina uhusiano na utajiri wa nchi. Hizo hizo pikipiki tulizonazo zikitumiwa vizuri zinatosha, tena na kubaki.
Mkuu kuna watu watatetea kila ushenzi tunao fanyiwa ikiwa ni pamoja na hili. Tecnology zipo za kuweza kupunguza muda wa kufunga barabara lakini jitu linatetea ujinga. Mwingine anaona hii sawa hati hatujastaarabika-my foot.
 
Kuna siku tulisimamisha Namtumbo karibu masaa 2 na 30 kusubiri msafara wa PM aliyeko Tunduru
 
Wenzetu per capita ni >$ 50,000 sisi <$ 2,000. Kwa hali hii basi tutumie muda wetu vizuri ili kujenga uchumi badala ya kupoteza muda mrefu tukisubiri misafara ya viongozi ambao hupita baada ya saa nyingi.
 


Hamna haja kumpeleka askari kwenda kujifunza, wanaweza kuwakusanya watu wenye wepesi wa kuona na kuelewa jambo kama wewe najua mpo wengi mliojifunza mengi huko ughaibuni mkawafanyia exposure au workshop hao askari hapahapa nchini kama huyo IGP anathamini michango ya watanzania
 
Tuliwahi kusimamishwa pale Veta Zaid ya Saa 1 Kusubiri msafara Sijui wa kiongozi Gani,,Nashindwaga kuelewa hawa wahusika Inakuaje hawajali muda wa wanachi
 
Sanasana mtu fulani kama anatoka Dsm anaenda dodma watu tunakaa kwenye mabasi masaa hata mawili na wakiachia barabara mkanyagano huo ajari ndogongogo zinatokea sana
 
Sweden mbali sna waje hapa kwa Madiba tu kupata Elimu hiyo kingine sio kila kiongozi Msafara hapa kwetu hatari sna...
 
Kuna siku niliona documentary moja jamaa walisema kwa jinsi viongozi wetu wa Afrika wanavyokuwa spiidi kwenye misafara yao basi ile spiidi wangeihamishia kwenye maendeleo tungekuwa mbali sana.
 
Wewe umetumwa na mabeberu sio bure. Hii nchi ni tajiri sana,hatuwezi kushindwa jambo dogo kama hilo. Kama vyama vya upinzani vimedhibitiwa,mafisadi wote wameisha hili ni jambo dogo. Ngoja mr Prezidaa ausome huu uzi ndio utaamini hatishindwi kitu.
 
Kwa msafara unaotumika unahitaji kama dk 5 tu kusafisha njia. Gari ya polisi ikimove 1km away na anapoanzia kiongozi msafara inatosha kupisha. Bado tupo kwenye mazoea sana .. jamaa yupo dar,mikoani anapokuja mshapigwa pini.

Unaambiwa polisi ndiyo waoga zaidi,watu wa usalama huwa hakuna shida kbs. Inabakia kushangaza tu.
 
Unahisi kuna wese la mawazo hapa mkuu?

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…