Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Usiemtaka mjini amekuja.(nimeiona kwenye fiat lori latembea pole pole sana)
 
Kumbuka watoto nyumbani

Nafikiri kwangu ndio uliokuwa msemo wenye maana kubwa sana
 
If u dont no, u dont no (no instead of know)
 
amli_jat.jpg

.....
 
1. Kuzaliwa mjini ni sawa na kumaliza form six
2. Hata shetani huitwa Mungu
3. Chezea mshahara usichezee kazi
4. Walidhani halitafika sasa washangaa
5. Ukisikia mlio wa bunduki ujue risasi imekukosa
6. Dogo kwako
 
Hizi nimeziona kwenye daladala Kenya ...kulipa ni lazima,chenji ni ukikumbuka...na hii nyingine,kupanda ni popote kushuka ni stage(kituoni).
 
1. Chezea mshahara usichezee kazi
2. samahani sio sumu
3. huwezi kuwinda usichoweza kukiuwa
4. mrefu anapata sifa kwa sababu mfupi yupo.
 
1. Usione vya elea ujue vimeundwa.!
2. Hasira za mbu hazichani neti
3. Shati bovu si mgongo wazi
4. Gusa unase
 
Back
Top Bottom