Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Banki moon

Mkuu, hicho ulichoweka si msemo ni jina la mtu (nomino). Wako wengi wanaoweka/kuandika majina ya watu mfano Furgason. Aresene wenger, Morinho, Osama, G. Bush, Obama nk.
Katika thread hii weka semi zile wanazoziandika kwenye magari na wala si aina ya gari au watengeneza body kama vile Scania, Leyland au Marcopolo,Binbross.

Nafikiri hapo nitakuwa nimeeleweka. Tuendeleee!
 
Si uliingia mwenyewe, uwii ya nini?

Tatizo pesa.

Una beep....Ntakupigia!!

Salio dogo.

Panda juu kazibe.

Usizame chubwiii

Kamba fupi

Yeboyebo haimalizi mwaka

Mmmh! nani kasema sitaki?

Hata paka mzee hutamani maziwa.

Shemeji ananitega

Usinichumm...wanaona.

Wapambe nuksi.
 
Usijifunge kibwebwe na ngomasiyako

paka ni paka tu

komba kasoma

sanga mwanitu

7 + 7= 21 vemasana
 
1. 6 ilikuwa 9, kiburi tuu.
2. kusoma hujui hata picha huoni.
3. eti shikamoo, unataka kuninyima nini.
 
1.Kaza buti safari ndefu
2.no gain no pain
3.no easy task
4.no longer at easy
5.kesheni mkiomba
6.kufunga si kazi, kazi kuchunga swaum
7.kunyamaza sio kushindwa
8.umekula perege unasema umekula samaki ukila pweza utasema umekula nini?
9.ving'aavyo si dhabu
10.bure ghali
11.kizuri chajiuza kibaya chajitembeza
12.baniani mbaya kiatu chake dawa
13.mkulima kala mbegu
14.utakula jeuri yako
15.hata ukinawa huli
16.utakula kwa macho!
17.ikisimama chapa ilale
18.man on work/wanaume kazini
19.mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba
20.kichwa cha mwendawazimu
21.ukitia mguu pesa

Duh zipo nyingi sana kwa leo zinatosha
 
1. Ndoto si pato
2. Masikini haishiwi ndoto
3. Safari za masikini ni za bure
4. Haidakishi
5. Haina kwere
6. Bila ubishi huli
7. Kazi na swala
8. Swala na kazi
 
Back
Top Bottom