Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

e1a815a8d11e880c58880803bd5c6917.jpg
408782e0dfc1b8dfba74247b2cab4012.jpg
 
jr.jpg


Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

- Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
- Ukicheka na nyani utakula mabua.
- Hata ukioga, mjini huendi.
- Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
- Akikua ataacha!
- Hata kwetu wapo.
- Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
- Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
- Jino moja mswaki wa nini?
- Swali kabla hujaswaliwa.
- Dume kwenye mfuko wa nyuma?
- Usivue viatu kuna mbigiri.
- Changanya na zako!!!
- Unga robo, usicheze mbali.
- Butua uwakomboe wenzako.
- Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.

Ngariba haogopi mkojo..
 
Back
Top Bottom