Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Wakasemezana....Je sisi ni kina nani mpaka BWANA atufanyia haya yaliyo makuu kwa kutu nyunyizia mvua ya vichwa vya Treni?.....Acacia:3:2-4
Ndipo Barick mkuu akasema,mkiyashika mausia yangu mtakula mema ya nchi.Kuchenjua 4:5.
 
[emoji13] [emoji13]
 
Enyi watu wa nchi,msifadhaike kwa vile afanyavyo sherehe kila wiki,maana segerea inamtamani. Iptl 20:7
 
Tena amini nawaambieni yeye aliyepokea kwa mkono wa kulia atatoa kupitia tundu lolote.Na haya nimewaambieni mbele ili wakati atoapo muwe tayari kushuhudia.Naye aliyeko wodini asitoke hapo mpaka kesi yake iishe kusomwa. Mbagala 6:5.
 
Ndipo mfalme akasema nchi hii imebarikiwa kuliko dunia nzima, maana asema bwana wa majeshi kuwa atatelemsha vichwa vya treni visivyokuwa na mwenyew.. Koromije 2:3
 
Ndipo makada wakajipiga vifua na kugalagala kwenye mavumbi kama chatu huku wakisema, "ewe Sizonje tuchukue utumwani milele"
Lumumba 4 : 5-13
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nami nilipochangia nikatoka na kwenda zangu na niliporudi jioni nikakuta jamii forum imechafuka na makada wa Lumumba wameenda kuishitaki kwa kuhani ili malaika alieshusha vichwa vya treni ashuke kuizima mitandao
Koromije 8:15
 
Wakasemezana....Je sisi ni kina nani mpaka BWANA atufanyia haya yaliyo makuu kwa kutu nyunyizia mvua ya vichwa vya Treni?.....Acacia:3:2-4
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hahahaha hatari[emoji581] [emoji581] [emoji582] [emoji582] [emoji586] [emoji586] [emoji586]
 
Nchi ya Giningi, Watu wake wamekunywa uji Wa ndele amabo unawafanya Mzugo wao kuona nyeupe kuwa nyeusi na kinyume chake. .

Bi Kilembwe 2:6:9
 
Ndipo Farao akastaajabu kuona hakuna aliyejitokeza na kukiri vichwa vile ni mali yake,wafuasi wake wakaangaliana na kusema,"hakika Mungu yu upande wetu,ametushushia vichwa kutoka mbinguni".Nao Wadanganyika wakaangaliana kwa mshangao kwa maana waliijua kweli.Nae Erode ambaye ambaye alikuwa kipindi cha utawala wa Mroma(JK),akakaa kimya hasiseme neno maana akikumbuka kupukutika kwa nywele kichwani hana hamu....Watch Out 22:12-20
 
Wadanganyika wakasikika wakiitikia Amina Amina SIZONJE Wewe ndiye Rais wa milele wa nchi yetu utukuzwe milele na Wadanganyika wote. ZERO BRAINS 10:25-30


Na kwa jinsi gadhabu ya Bwana,SIZONJE ilivyo waangukia wana wa DANGANYIKA......wakaambizana ole wake atakaye vikubali na kuvitwaa VICHWA HIVYO.....Hatusomeshi Wazazi-7:28-31
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…