Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

f5542ceb2c122cb524f4d12a792ad03f.jpg


522f02254bb1029e6cf089bacc8b1921.jpg


a18d370b9af3f60fed0851779d4e3c24.jpg


Kama umeshakipitia kitabu hiki ongezea mistari zaidi

Na Bwana wa Majeshi akijaa kiburi akasema naye atakayenipinga mumuweke mahabusu kwa masaa 48;Kiburi 15:1
 
Kisha wakiwa wale wakamuuliza mfalme, je tutafidiwa uharibifu huu ulioletwa na janga hili?
Mfalme kwa majigambo akawauliza watu wale wenye huzuni kuu, je ni ufalme wangu uliotukuka uliyoyaleta yote haya? Nao wakajibu la hasha mfalme tuhurumie jmn twafaa. Mfalme akawaambia hakika nyinyi mmelaaniwa lile gonjwa kuu limetokea kwenu na bado kutetemeka bado ni nyie.
Baada ya kusema hayo ndipo mfalme akajitwalia na zile shekeli zote kutoka kwa wasamaria na kuondoka zake kimya kimya.
Washomile 1:20 25
Duh! Hii hata Sizonje akiisoma atacheka tu. Umeua kabisa...!!
 
Nae wazir mwenye dhamana akaitwa na kaisari kuulizwa kuhusu vichwa vile akastaajabu na akajibu kwa kusema sivijui vichwa hivi!!!?

Nasi Kando ya bahari ya hindi ndipo tulipo keti tukalia na kushangilia mana ya vichwa vya treni vilivo shushwa kwa upepo wa kisuli suli Tanzania awamu ya 5:17-2020 [emoji23][emoji22]
 
Ndo akafungua kinywa na kunena 'kwa vile umesema wazee tuachwe tupumzike na wala tusihusishwe na mikataba mibovu ya wakati wetu, Bwana wa majeshi, basi ikikupendeza utawale milele' : Kulindana 20:17
 
Mi nadhani ndugu zangu ifikie hatua tukue kifikra. Tunapaswa tuendeshe mijadala yenye tija kuhusu vichwa vya treni itakayomsaidia Rais wetu JPM na sio mizaha na kejeli za kipuuzi.
Nalikuwa katika mji wa Bandari Salama nikiomba,roho yangu ikazimia,nikaona maono;vyombo vinashuka kutoka mbinguni,nikitazama kwa makini,vilikuwa ni vichwa vya treni.[Waraka wa Pili wa Bashite kwa Wanakolomije 11:7-10]
 
Ata maneno yake sizonje yakadirikuwa ni katiba na nchi kuwa mali yake binafsi,waasi na kuangamizwa na kubinya uhuru!akili mzigo 2:7
 
walivyo kuwa katika makutano tazama mfalme aliwatuma majeshi wakamkamate kuhani mkuu anayeusaka ufalme kwa UDI na uvumba hata majeshi yalipomhoji yalishindwa kumtia hatiani mujikiki 20:5-- 9
 
Nae mfalme sizonje akapaza sauti zakee mbele ya wananchi na kuwaambia, aminini nawaambia Kuna wafalme wa mwanzo waliuza kila kitu ila siwataji

Nyamazugo 7:21
 
...Hata ilipotimia miaka miwili ya ufalme wa JeyPiemu walikuwako wote mahali pa moja,kukaja ghafla toka mbinguni uvumi wa upepo wa nguvu ukienda,ukaijaza bandari kwa vichwa vya treni,wote wakashangaa na kustaajabu.[MATENDO YA MAKADA 2:5-8]
 
Sauti ikasisika katika kundi la watu mfalmee! tusaidie ndipo mfalme akajibu niwasaidie nini?
Tuna njaa! Kufeeeni na njaa zenu ama kwa hakika mimi sio mpishi
70:70
Mods mbona mna edit mistari tukufu nani kawapa mamlaka hayo.. Haya mme edit sasa hiyo 70:70 ni nini?
 
Nayo njaa ikaikumba nchi ile, naye mfalme akasema kwenye utawala wangu hakuna njaa na atakayetangaza njaa atatupiliwa mbali, na ufalme wangu hotogawa chakula.
Nayo nchi igajawa na simanzi na asitokee wa kuwatetea.
Lakini tazama mwana mfalme bashite na makada waliomuunga mkono wakila na kusaza.
Nae aliye juu kaona maovu hayo hakika atamtuma musa kuwatoa wanyonge kwenye mateso yao.
Uchaguzi 19:10-2020
 
Ndo akafungua kinywa na kunena 'kwa vile umesema wazee tuachwe tupumzike na wala tusihusishwe na mikataba mibovu ya wakati wetu, mkuu wa majeshi, basi ikikupendeza utawale milele' : Kulindana 20:17
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]atawale milele mfalme belishaza
 
Back
Top Bottom