Mishahara imekatwa: Poleni Watumishi watia nia

Ninachofahamu japo sijasoma sheria yenyewe mtumishi akifanya kazi chini ya siku 15 anatakiwa kulipwa nusu mshahara Happ Sina hakika kwakweli
 
Sifurahii watumishi was umma kukatwa mishahara yao ya mwezi julai ila sheria ni msumeno
 
Mkuu kabla hujalalamika unafahamu taratibu za utumishi wa umma kuhusu mtu ambaye anataka kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa vyama vya siasa ?


Maana tunaweza kuanza kulaumu watu wengine kumbe makosa yapo upande wetu kabisa
Kuchukua fomu na kuchaguliwa kugombea ni vitu viwili tofauti.Hiyo sheria inapingana na katiba.

Ibara ya 21 ya Katiba: 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
 
Eti kisasi!! Huyu mtumishi wa umma wa tz mwente kisasi ni mwalimu au dakrari?? Yani hata wasingepewa mishahara mpaka oct bado watachagua CCM!
 
Ni sheria ipi walivunja mpaka wakasimamishiwa mishahara? kwani hawawezi kushitaki?
Usitugombanoshe na serikali yetu. Ngoka tuvumilie hilo lipite. Tunashukuru kwa kuwa ni mwezi mmoja. Kidumu chama cha Mapinduzi.

Mtia nia.
 
Wambie washukuru pia mwezi ujao watapata mshahala, je wangetimuliwa saivi nadhani wangekuwa ICU.
Kina katika, matambiko, Elia Michael et al nao mwezi ujao watarudishwa kwenye payroll?
 
watumishi wa umma nchi hii hawajielewi wengi wao.
 
Kina katika, matambiko, Elia Michael et al nao mwezi ujao watarudishwa kwenye payroll?

🤣🤣🤣🔨🔨🔨 akina kafulila, makonda hao waendelee kuwa jobless hadi hapo Jiwe akipata nafasi ya kuwapa tena
 
Umetumwa kutusemea?
 
Mistari 3 ya mwisho "kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria."

UTARATIBU uliowekwa kwa watumishi wa umma kuhusu kutaka kugombea nafasi za uongozi wa siasa ndo uko Kama nilivyo eleza katika post ile uliyo i-quote
 
Sheria inasema
Mtia nia yoyote aliyeajiliwa anatakiwa aache kazi ndipo aingie kwenye shuguli za siasa
Washukuru ata wamepunguziwa na sio kuachishwa
Siyo Kweli Mkuu! Anaruhusiwa kuanza michakato ya kuingia kwenye siasa akiwa bado mfanyakazi kwa kuomba ruhusa au likizo isiyokuwa na malipo,akishafanikiwa kuchaguliwa kwenye nafasi ya kisiasa hapo Sasa anatakiwa aache kazi.
 
Sheria inasema
Mtia nia yoyote aliyeajiliwa anatakiwa aache kazi ndipo aingie kwenye shuguli za siasa
Washukuru ata wamepunguziwa na sio kuachishwa
Hakuna sheria inayosema hivyo. Standing orders za civil servants zinasema wakati wa mchakato wa kura za maoni mtumishi anapaswa kuomba likizo ya bila malipo. Hivyo kukatwa mshahara kwa siku ambazo hawakuwapo kazini ni sahihi kabisa, lakini siyo kufutwa utumishi. Mgombea atatakiwa kuacha kazi mara chama chake kikimpitisha kugombea ubunge au udiwani.
 
Sheria mbona iko straight forward, tatizo watu wanataka kumwibia mwajiri. Kuna mambo wanayotakiwa kuyafanya kabla ya kuingia kwenye mchakato wa kura lakini wanataka kujifanya hawajui. Nasema tena sheria haimzuii mtumishi kuingia siasani!
 
Acha waisome namba eeee! Wajinga wale....mbele kwa mbeleeeeee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…