Mishahara imekatwa: Poleni Watumishi watia nia

Wamevunja sheria ipi?
 
Afadhali hao.. akina daudi bashite walotumbuliwa kabisa wasemeje?
 
Waraka wa Watumishi wa UMMA wa mwaka 2015 umeelezea vizuri kabisa, labda kama walienda kutia nia bila kuusoma na kuuelewa
 
Yasome vizuri maandishi haya uliyoandika "kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria"
 
Hapo mwisho umepasoma inapoeema kwa kuzingatia sheria na utaratibu???
 
Anaetaka kugombea kwamujibu Wa taratibu Za utumishi, waraka wa mwaka 20015 uko wazi mtumishi wa umma anaetaka kugombea nafasi ya kisiasa atapaswa kuomba likizo ya bila malipo na atajibiwa nakuruhusiwa.
Kwa mgombea ubunge likizo itaanza siku litakapovunjwa bunge mpaka siku tume ya uchaguzi itakapotangaza rasmi majina ya wagombea.
Ambae hatatangazwa kuwa mgombea ataomba kwa barua kurudi Kazini na kama nafasi ipo atarudishwa Kazini.
Ninachoona nikwamba taratibu Za utumishi zimetumika Barabara Kama ambavyo wengi mngependa utawala wa Shera ila ikikukata sheria unaanza kulia.
Mimi nakumbuka kabla yakuanza michakato utamishi walituma huu waraka kukumbushia ili tusijisahaulishe lakini bado tunahaha.
Nikionacho watia nia wamerudi Kazini huku muda wao walikizo ya bila malipo haujaisha kwasababu tume bado haijatoa majina ya wagombea. View attachment Waraka_wa_Mkuu_wa_Utumishi_wa_Umma_Na_sw.pdf
 
Kwenye maswala ya fedha jiwe anajifanya anafuata sheria ila kwenye maswala ya haki hafuati sheria.(watumishi kuongezewa fedha kila mwaka).
 
Siyo kukatiwa mshahara ila sheria ya Utumishi inasema lazima ujiuzulu ndiyo ukagombee,washukuru hata hilo mshahara wa mwezi mmoja,mtumishi wa umma hatakiwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa
 
Hongera serikali kwa kusimamia sheria na kwa matumizi bora, tena mngewafurusha kabisa. Mtu unaacha ofisi unaenda kuchukua form unaijaza unapitisha kwa wadhamini unairudisha unaitwa kujinadi kwa wajumbe unapoteza muda wote huo nje ya ofisi halafu unategemea nini
 
Afuate na sheria ya kuwaongezea nyongeza ya mwaka. Sheria msumeno
 
'Kwa mgombea ubunge likizo itaanza siku litakapovunjwa bunge mpaka siku tume ya uchaguzi itakapotangaza rasmi majina ya wagombea'.

Aisee hapo ndipo pagumu,wasishangae na August hawatalambishwa mashahara.
 
Huyu atakuwa ni mmojawapo
 
Kama uliweza kuweka nia ya kugombea ubunge, mshahara sio kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…