Mimibaba
JF-Expert Member
- Jul 1, 2009
- 4,557
- 1,294
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.
Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?
Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?
Kwa kweli kulingana na ikama itolewayo na serikali mara kwa mara hii mishahara ni midogo kukidhi mahitaji ya kila siku kwa watumishi wote wa seikali. Inaanzia $1200 kwa KM hadi kama $5000 kwa Rais kwa mwezi.
Ila mshahara si issue kwa vile ana "entinlements" (stahili) nyingi. Zinajumuisha matumizi ya kawaida kama usafiri ulinzi, mawasiliano, kiwango cha posho ya kusafiri hata posho ya vikao. Mfano mimi kidampa mshahara wangu $100 kwa mwezi nikisafiri nje say Nairobi au Kampala nastahili kulipwa $ 230 kwa siku sawa na mishahara ya miezi miwili na zaidi. Hapo ndipo kwenye utata. Iweje posho ya kusafiri nje kwa siku izidi mshahara wa mwezi? Jibu ni kuwa watumishi wengi hawana fursa hiyo ila baadhi tu ya wanamtandao. Lakini uchambuzi wa ndani unadhihirisha kuwa viwango vya mishahara vinalingana na tija. Maana yake udogo wa mishahara unalingana na udogo wa Tija, ujuzi, uweledi fikira fupi, hata uaminifu na utiifu kwa serikali.
Nakushauri usiangalie sana viwango vya mishahara kwa sababu siyo realistic na mfumo fare na productive wa serikali makini