kwahiyo hakuna mwenye data kamili za mshahara wa mkulu wetu waungwana? kwanini iwe siri kwa tanzania tu?
Bado sielewi kwa nini mishahara ya watumishi wa umma iwe siri hususan ule wa raisi.
there you are, mkuu!Nadhan amount ni kubwa mpaka kutangaza wanaona soo angekuwa analipwa laki 5 au mill2 angesema ila ni nying ukisikia utalia.
..........Ajabu kubwa muajiri muajiri asipojua mzhahara wa mtumishi wake............Ni 2011 na bado hakuna anayejua kwa uhakika mkuu wetu wa nchi analipwa mshahara kiasi gani! Hii ni aibu kubwa sana hususan ukizingatia kuwa walipa kodi hela zao ndiyo zinatumika.
Shameful!
Jamani kuna mtu anayejua mshahara wa raisi wa Tanzania ni kiasi gani? Kuna mtu kaniambia ni $200,000 na kitu kwa mwaka...sikuamini lakini akanihakikishia kuwa taarifa zake ni za uhakika. Bado ninasita kuamini ingawaje sina taarifa zozote na sijawahi kuona mahala popote pale kuhusu mshahara wa raisi.
Na mshahara wa makamu wa raisi..?
Waziri mkuu..?
Spika wa bunge..?
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, polisi,magereza..?
Jaji mkuu..?
Kama kuna mtu anayejua...ni wapi tunaweza kupata taarifa hizi?
Mazee Nyani Ngabu kapatwa na maswahibu gani tena.....
Hilo nalo neno!Kwa nini rais wa Tanzania, mawaziri na gavana wa BOT walipwe mishahara yao katik US$ wakati currency yetu ni TSh?