Na bado hatujui mshahara wa rais wetu wa leo.Hivi kinachobishaniwa hapa sasa ni kipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na bado hatujui mshahara wa rais wetu wa leo.Hivi kinachobishaniwa hapa sasa ni kipi?
Nimekuambia hivi, hiyo sheria yako ime-expire, au haipo kabisa, kwa sababu Mkapa anasafiri na kundi la watu 15 wakiwemo maofisa toka Foreign, ambao nusu yao walishatangulia tayari, msimamo wangu ni kuwa hiyo sheria ni either batili, au haitumiki kabisa, au ilishabadilishwa, lakini haitumiki kabisaa na wala sio muongozo wa misafara yake, au ya Mwinyi hiyo sheria yako ilisha-expire!
Ungekuwa na objectivity, then ungeona mwanzoni na mapema nimesema kuwa Dodoma, kuna nyumba za mawaziri viongozi wa Zanzibar, ikiwa ni ile part ya wao kuwa na nyumba Zanzibar na Dodoma, kama vile hawa wengine walivyo na nyumba Dar na Dodoma.
Umetaka sheria. Umewekewa. Sasa unasema ime'expire' maana inapingana na alichokiona the omniscient FMeS. Ndiyo maana bado tunashindaniana kitu ambacho wengi wanashangaa. Sasa unakuwa ubishi wa kitoto.
Sheria hai'expire' maana haina 'sell by' date. Sheria inafutwa, inaongezewa au inarekebishwa lakini hai'expire'. Maneno kama haya ndiyo yanaonyesha kutokufahamu kwako.
Mafao yanayozungumziwa ni yake binafsi na si ya ujumbe anaoweza kujumuika nao. Kama anasafari kwa niaba ya serikali bila shaka kuna watu wengine ambao bado wameajiriwa na serikali watakao ongozana nao. Hawa ni wale ambao wanahusika na jambo ambalo Rais Mstaafu anaenda kutuwakilisha. Kama anaenda kutuwakilisha kwenye mikutano ya Umoja wa Mataifa basi ataongozana na watu wa Foreign. Kama ataenda kutuwakilisha katika kongamano la ugonjwa wa ukimwi basi ataongozana na watu wa wizara ya afya, Tacaids na wengine. Hawa wanaongozana nae kutokana na umuhimu wao na si kwamba ni stahili yake. Vile vile pamoja na hawa ambao analipiwa na serikali hazuiwi kuongozana na watu ziada ambao either anawalipia binafsi au wanalipiwa na taasisi nyingine. KUMUONA Mkapa anaongozana na watu lukuki si ushahidi kuwa wote hao wanaenda kama stahili yake. Ndiyo maana sisi wengine tunaangalia sheria inayoongoza la si maneno ya mtu hata akiwa Rais Mstaafu mwenyewe. Kama maneno hayo yanapingana na sheria ina maana msemaji pengine hajui analolisemaea, ni muongo au anapindisha sheria kwa manufaa yake!
Hakuna mtu aliyekupinga kuhusu kusafiri kwa wastaafu First Class. Tulichopinga ni hao ambao ulidai ni stahili yake kuongozana nao. Watu kama wapishi ambao hawatajwi kwenye sheria. Conveniently, hukuona hilo! Lakini tutegemee nini kwa mtu ambae anaamini kuwa katiba ndiyo inayoelezea mafao ya viongozi, anayeamini binadamu wana specifications, anayeamini sheria ina'expire' n.k. Mwenzetu umekalia ubishi na si kuelimishana.
Stahili za viongozi wa serikali ya mapinduzi zinatawaliwa na sheria ya kwao na kulipiwa na serikali yao na si ya Muungano. Ndiyo maana waliweza kumkatia Maalim mafao yake kumshikisha adabu. Hii mada inazungumzia viongozi wa serikali ya Muungano. Mwenzetu umekalia ubishi na si kuelimishana.
1.
1. Maalim alikataliwa mafao na serikali ya jamhuri baada ya kujiunga na CUF, lakini wakati wa muafaka alirudishiwa mafao hayo na aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Mang'ula kwa niaba ya seriakli ya jamhuri, na anapewa mpaka sasa.
2. Mimi nijuavyo utumishi Dar ndio wanahusika na mafao ya viongozi wote, wa bara na visiwani, wasaidizi wakuu wa wastaafu wote huripoti pale, hayo mengine ni yako mkuu, otherwsie elimu safi sana, tuendelee kukata ishu.
Ahsante Tena.
Hapo ndipo unapoharibu kabisaa, kwa sababu wapishi hawana anything to do na anaenda kuwakilisha what, halafu ni lini basi hao wastaafu walienda bila kuwakilisha serikali? Maana kila wanapokwenda timu huwa ni ile ile, sasa naomba unifahamishe ni lini walienda bila kuwakilisha serikali? Hapo muongo anakuwa yule asiyeelewa anachosema na kulilia sheria ambayo haitumiki au haipo kabisaa, kama haiku-exipire.
Hivi hiki kitu Government Salary Scale ni kitu ambacho kiko public ?
I bet the answer is no.
Kama hiki nacho ni siri ya Serikali, Watanzania tuna panya vichwani. I'm pissed!
Maalim alikataliwa mafao na serikali ya jamhuri baada ya kujiunga na CUF, lakini wakati wa muafaka alirudishiwa mafao hayo na aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Mang'ula kwa niaba ya seriakli ya jamhuri, na anapewa mpaka sasa.
Kuhani,
Goverment salary scale ziko wazi. Mishahara ya watumishi wa serikali (civil servants) iko wazi. Lakina ujue hii mishahara si lazima iendane na wadhfa ambao mtu anaoshika kwa wakati huo. Mishahara inaongozwa na cheo. Mimi kama Fundi Mchundo ninaweza kuwa na cheo cha Fundi Mchundo daraja la 3 lakini wakati huo nikawa na wadhfa wa Mhandisi wa Mkoa! Cheo changu cha FM daraja la 3 ndicho kitaainisha mishahara na vitu kama allowance kama nikisafiri na si wadhfa wangu kama Mhandisi wa Mkoa. Hivi ndivyo ilivyokuwa enzi zile. Sijui hali ya sasa hivi ikoje.
Mishahara na stahili ya viongozi wa kisiasa, mawaziri, wakuu wa mikoa, mpaka mheshimiwa Rais ndiyo haiko wazi.
Ahsante, Mkuu.
Kama naweza kuuliza lingine:
Tanzania, katika ajira za Serikali, kuna kitu kinaitwa "Performance Review" ?
Ahsante.
Tanzania, katika ajira za Serikali, kuna kitu kinaitwa "Performance Review" ?
Maalim alikataliwa na serikali ya mapinduzi na si ya Muungano. Kwa mtazamo wako basi hata mishahara ya viongozi wa serikali ya mapinduzi inalipwa na JMT? Utumishi has nothing to do with mafao na mishahara ya viongozi wa Zanzibar.
Si safari zote wanazosafiri kuwakilisha serikali. Wao kama wastaafu ni raia huru kama wengine. Mkapa anaenda Geneva mara nyingi kwenye masuala ya South South Commission. Anaenda kama raia na si kama mwakilishi wa serikali. Kwa maneno mengine nafasi yake huko ameipata kama Mkapa na si kama mtumishi wa serikali. Anawakilisha serikali anapoombwa kusuluhisha migogoro kama ile iliyotokea jirani kwetu, Kenya. Rais anaweza kumuomba amuwakilisha katika kongamano, mikutano kwa jinsi anavyoona inafaa. Yeye kama raia mwingine anaweza kusafiri kokote anakotaka bila kuwakilisha serikali. Anaweza kwenda Jordan kumwangalia rafiki yake, anaweza kwenda Marekani kutembelea rafiki zake na kwingineko. Yeye ni raia na hafungwi na chochote. Kwa kifupi, si kila ukimwona Mkapa yuko kwenye safari za serikali. Vile vile kwa wastaafu wengine.
Kutotumika au kukiukwa kwa sheria hakuifanyi kuwa ni batili. Uwezekano unabakia pale pale kuwa akija mwenye nia anaweza kutumia sheria hiyo kuwafanya wanaoitumia vibaya au kuikiuka accountable. Pasingekuwa na sheria ya procurement hamna ambalo lingeweza kufanyika juu ya Richmond. Kukiukwa kwake hakukuifanya iwe batili. Vile vile kwa sheria nyingine za nchi zikijumuisha na hii ya mafao na maslahi ya viongozi.
Mang'ula kama makatibu wakuu wa vyama vingine vya siasa, hatambuliki kama mlolongo wa viongozi wa serikali. haiwezekani yeye akamrudishia aliyekuwa mtendaji wa serikali mafao. Hana uwezo wa kuandika barua kutumia nembo ya serikali. Sasa aliwezaje kutoa taarifa ya uamuzi wake? Huu ni uongo mwengine.
1.
Haya yote uliyoyasema hapo juu hayana uhusiano wowote na the ishu, ya kwamba kwa nini kila anaposaifiri anakuwa na kundi la watu zaidi ya 10? wakati wewe umesema kwua anakuwa na hilo kundi wakati tu anaenda kuwakilisha serikali? Mimi ninakwamba toka nimeanza kuwaona Mkapa na Miwnyi wakisafiri, siku zote wanakuwa na kundi la watu zaidi ya 10,
Wewe unasema sheria inasema anatakiwa kusaifir na watu wawili tu, sasa naomba jibu kwa nini huwa anakwenda na watu zaidi ya 10?
2.
Finally, sasa unakubali point yangu lakini bila kukubali wazi, kwamba sheria yako kama ipo haitumiki, ambayo ni moja ya argument yangu au? ungekubali hili mapema tusingefika kote huku, nimekuambia na ninarudia tena kuwa kwenye sheria zote mlizozileta kuhusiana na mafao ya viongozi wakuu, binafsi nimeiona sheria ikiwa na kipengele kimoja tu cha tiketi First Class, basi mengine yote sikuyaona, na imenifanya kuamini kuwa either hakuna sheria, kama ipo haitumiki, au ilisha- expire, au ilifanyiwa marekebisho.
Hauna point sasa nitakubali nini. Toka mwanzo uliambiwa kunasheria inayoongoza stahili za wastaafu. Wewe ndiye ulikuwa unapinga kuwepo kwa sheria kwa sababu unaona mengine. Hauwezi kusema kuwa hakuna amri kumi katika biblia zinazoongoza miendendo ya wakristu kwa vile wakristu wengi hawazifuati. vile vile kwa sheria. Ndiyo maana sisi tunakupinga wewe kutuletea unayoyaona kama facts mbadala wa sheria.vile vile kwa Mkapa kuongozana na watu hata hamsini hakumaanishi kuwa hiyo ndiyo stahili yake. Kigezo ni sheria inasema nini. Zaidi ya hapo ni kuwa anakiuka sheria.
Haujui taratibu za serikali. Kiongozi wa chama chochote cha siasa asiye katika utawala wa serikali hawezi kufanya lolote. Anaweza kuamrisha lakini hawezi hata kuandika. Kwa taratibu za serikali yule aliyeandika barua ya kutoa agizo ndiye anayewajibika na si yule aliyetoa maagizo kwa mdomo tu! Of course, idara ya utumishi inaongozwa na katibu mkuu. Sasa unataka kudai kuwa na hiyo ni dataz!
Unanipotezea muda. Hautakuja kuelewa.
Niliposema kuhusu ninayoyafamu na wastaafu, wewe uliesema ni uongo kwa sababu sheria haisemi hivyo, ukaileta sheria ambayo ni clear kuwa wastaafu hawaitumii kulingana na ninayoyaona in wastaafu, sasa nikasema kuwa either hiyo sheria haipo, haifanyi kazi, ime-expire, au haitumiki kabisa,
Badala ya kukubali point yangu, ukaamua kubisha kuwa ninayosema kuhusu wastaafu sio kweli ni uongo, nikasimama kidete na ksuema wazi ninayoyaona, then sasa unasema kuwa sheria ipo lakini haitumiki, sasa ndipo ninapokuuliza kosa langu lipo wapi? Mimi nimesema kuwa nijuavyo wastaafu wana mafao makubwa sana tena kuliko hata hii sheria mliyoileta,