Mishkaki ya Tsh.100 Dar

Mishkaki ya Tsh.100 Dar

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,903
Reaction score
1,979
Wakuu,huwa najiuliza kila siku, hii mishkaki [ya ng'ombe] inayouzwa sh.100 maeneo mbalimbali ya dsm, wauzaji wanapata faida gani?

Maana ni vipande 5 vya nyama, tena vitam tu, sasa kama kilo ya nyama ni Tsh. 5000 hadi 6000, hawa wandugu wanafanya biashara ya aina gani?
 
Ukishindwa kusthimili na kupenda kula tu huenda ukala hata visivyofaa maana mji huo una mambo sana hasa nyama zakukuta barabarani ni hatari sana.
 
Chunga sana ndugu ulaji wa mishikaji,huku kwetu kuna mzee alikuwa anauza mishikaji kwa 50/= amefungwa,kumbe alikuwa anachinja mmbwwaa!!

Duh!
Kama ni mbwa kwelh,bs watakuwa watam balaa.
Ila...
 
Chunga sana ndugu ulaji wa mishikaji,huku kwetu kuna mzee alikuwa anauza mishikaji kwa 50/= amefungwa,kumbe alikuwa anachinja mmbwwaa!!

Hiyo kitu chungana nayo sana hata huku mitaa ya kwetu kuna jamaa alikuwa na wateja kibaoo wa hiyo kitu, siku ya siku jamaa si ikaja gudulika alikuwa analisha watu nyama ya mbwa, na alipobanwa sana kwa nini anafanya kitendo hicho cha kulisha watu nyama isiyo faa, jamaa si akawageuzia kibao akawauliza ebu nambieni nani kati yenu hajawahi kula nyama hapa?,au nani kati yenu alishapata madhara kwa kula mishikaki hapa?

Nyie nyote kila siku mlikuwa mkinisifia kwa kuwauzia mishikaki yenye radha leo hii mmenigeuka kwa kuwa tu mmekuta ni ya mbwa! Mbwa ni jina tu, nyama ni ile ile sawa na ya swala, mbuzi nk. hata bata ukimchunguza sana huwezi mla.Mwisho wa siku jamaa alishauriwa aombe kibali aendelee na kazi.
 
Hiyo huwa ni ya ng'ombe, mbuzi waliokufa+dog wanaozurura ovyo mitaani especially usiku.
 
Mwingine aliwahi kukiri kuwa ni nyama ya paka.
 
nyau wale mkuu, hasa wanaoshinda masokoni!
 
Wakuu,huwa najiuliza kila siku,hii mishkaki [ya ng'ombe] inayo uzwa sh.100 maeneo mbalimbali ya dsm,wauzaji wanapata faida gani?
Maana ni vipande 5 vya nyama,tena vitam tu,
sasa kama kilo ya nyama ni sh.5000 hadi 6000,hawa wandugu wanafanya biashara ya aina gani?

mkuu kiukweli ile huwa tunatengeneza kwa ajili ya Wahehe tu, sasa siku hizi kila mtu anaipenda. ila saiv itakuwa Tsh 150 kwa sababu mbwa wanaadimika.
 
mkuu kiukweli ile huwa
tunatengeneza kwa ajili ya Wahehe tu, sasa siku hizi kila mtu anaipenda.
ila saiv itakuwa Tsh 150 kwa sababu mbwa wanaadimika.

Unamaanisha kuwa wateja wakubwa wa mishikaki n wahehe!
 
Kuna miguu na vichwa vya kuku hapo ubungo,ni vitamu balaa!vimenisukuma sana hapo pamoja na mihogo ya kukaanga
 
nasikia huwa ni vitamu hasa.......

ila hiyo bei mi ndo ilinidiscourge kuna mahala nilipita watoto wa shule wamejazana wanasubiria mishkaki yao
 
Back
Top Bottom