Miss Reds Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kazi anayo, Umri wake utata mtupu

Kwani wapi sisi ni wa kweli?
Kuanzia Siasa mpaka kwenye Madhehebu ni uongo tu. Sembuse sanaa!
 
Mods please. We have had enough of this.
 
Hahahahaa daah!

Huyu binti ana wakati mgumu sana.

Baba zao tumeshachelewa kuwadhibiti sasa hivi vitoto vyao ni sawa na nyoka wadogo ni kukata vichwa mapema sana, matapeli kama hawa baadaye unasikia ni Waziri sasa tutakuwa na Taifa la namna gani?

Tena nimejitolea hizi evidence kuzituma Miss World, Lundenga achaguwe kusuka au kunyoa.
 
Natamani kamati ya Redd's Miss Tanzania ialikwe kwenye vipindi vya mahojiano kwenye TV ili wananchi wapate kuwatandika maswali.
 
Hivi age limit ya Miss Tanzania ikoje? Je Miss World?
Nimesoma sehemu Miss Amerika ni miaka 17 hadi 24.
Kwa umri wake unaoonyesha kwenye hiyo pasipoti asingetoboa mdada.
Miss world mwisho wa age limit ni miaka 24. Lundenga atalinywa hili.
Mods please. We have had enough of this.

Not yet, mpaka mkome nchi imeoza kabisa hii.
 
Haya ndio matokeo ya taifa kujengwa kwenye msingi gushi- muungano feki. Mambo yote yatakwenda kigushi gushi.
 
 
Last edited by a moderator:

Wewe mchovu Kabisa, hamna cha Dallas Wala nini! Sasa na mi document yote umeshindwa kuandika kitu cha maana ueleweke; "ana elimu zaidi ya...." What the hell does that mean, anayo ama hana? Kithibitisho chochote cha kuwa ama kutokuwa na hiyo elimu? Ama ndiyo passport? Duh! Kazi ipo?
 
Kungekuwa na utawala wa sheria nchi hii, kwanza muandaaji wa mashindano angewajibika na pia kashfa za babake ambaye ni mbunge polisi wangeshashughulika nae
 
Hii ni aibu kubwa kwa familia yake pamoja kamati nzima inayohusika na uandaaji wa mashindano ya umiss.

Inakuwaje hadi wakati huu wa karne ya 21 wapo watu wanaofanya mambo kijima?

Hivi walishindwa nini kuthibitisha taarifa za wasichana hao kipindi wanaomba kuwania umiss! Tena njia zipo kemkem?

Huu upuuzi wa kuwa na watu vilaza ambao wamekabidhiwa mamlaka nyeti tutauendekeza mpaka lini!

Kwanza huyo msichana sura yake tu nilipoiyona niliitilia shaka. Sura inaonyesha kabisa ana zaidi ya miaka 25 ila bila aibu yeye anajitangaza kuwa ni teenage! Mpuuzi kweli huyo binti.
 
Kwani wapi sisi ni wa kweli?
Kuanzia Siasa mpaka kwenye Madhehebu ni uongo tu. Sembuse sanaa!

Huo ndio ukweli. Wapi tumesema ukweli sisi? Maneno mengi, uongo mwingi..!
 
Hivi 2014 -1989 mbona ni 25 mmefanya hesabu gani? Miaka hiyo 25 kuwa na master ni sawa. Acheni kumshambulia binti mtieni moyo.

Hujaelewa labda, kwenye mashindano hayo aliyoshindishwa mwaka huu inasemekana ana miaka 18. Umri wake wa ukweli ni 25, ambapo asingeweza kushiriki kwa sababu limit ni 24yrs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…