Nachoshindwa kuelewa mimi....hivi kwani Ms. Tanzania ni big deal kiasi hicho mpaka uongope kama inavyodaiwa huyo binti alivyofanya?
Halafu, kama kweli kadanganya umri wake pamoja na hayo mambo mengine basi atakuwa ni bonge moja la mjinga.
Bonge moja la mjinga kwa sababu, katika dunia ya leo ya utandawazi huu, kuna mambo na mambo ambayo huwezi ukadanganya hususan mbele ya umma.
Sasa wewe mtu uko kwenye social media huko, halafu unaenda kwenye national stage na kuongopa taarifa zako mwenyewe, unategemea kweli watu hawatajua kuwa unaongopa?
Binafsi sifuatilii kabisa haya mambo ya mamiss lakini kama hizi habari kumhusu huyu binti ni za kweli basi akili yake itakuwa na hitilafu sehemu fulani.
Na nani anataka kuwakilishwa na mtu zuzu kama huyu?
Hili saga lina kila dalili ya kuja kuwa bonge la kashfa.