Mkuu R.B, hili haliwezi kuwepo, Generali Pascal Kamazima, ametumia jeshi letu maisha yake yote!, kama issue ni uasili, hiyo sio issue kabisa kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya uraia, watu wote walikuwa ndani ya ardhi ya Tanganyika kuanzia saa 6:00 usiku wa Dec, 1961, watahesabika ni raia halali wa Tanganyika huru, regarless asili zao!.
Tukianza na chimba chimba za nani alitoka wapi na asili yake ni wapi, mtakuja kukuta Watanzania Halisi ni Wasukuma na Wagogo na makabila mengine machache!.
Tkianzia na Mkombozi wetu, inasemekani huyu baba yake ambaye ni Chifu, alitoka Rwanda, uchifu wakati ule ukitolewa kwa mwenye ng'ombe wengi!, bila kuuliza alikotoka!.
Tukija kwa yule wa Zanzibar, alitokea Malawi, na wanae wote wamesomea kwa babu yao tangu shele ya msingi!.
Hata "Che Nka!", kwanza hilo jina ni la kikeni!, na alikuja nchini akiwa na miaka 6 huku akitembea mwenyewe kwa miguu yake miwili!.
Wangoni wanajulikana walikotoka, wakiongozwa na Zongendamba!. Wamasai na Wachaga wanajulikana walikotoka!. Wahaya na Wahangaza wanajulikana fika ni sehemu ya dola ya Bunyoro!. Musoma karibu wote wametokea kule!. Kigoma karibu wote wametokea kule!.
Wanyasa ni jina tuu, kiukweli ni Wamalawi!. Wamakonde hakuna siri wote wanatoka "nchumbiji!.
Tusifikishane huko tukaanza kunyoosheane vidole kila mmoja arudi kwenye asili yake!.
Pasco