MImi shabiki wa yanga lakini nakuliana na mtoa mada, Abuya bado hajaingia kwenye mfumo.
Game ya jana Gamondi akucheza ule mpira wake wa msako wa nyani ni kwa sababu alikua hajui anaenda kucheza na mpinzani wa aina gani.
Simba hii ni timu tofauti na mwaka jana, imebadilisha wachezaji wengi pamoja na kocha vile vile mechi zake zote amecheza indoor kasoro ile ya simba day tu kwaiyo Gamondi aliingia uwanjani akiwa hamjui mpinzani wake ikamlazimu awaambie wachezaji wake wacheze kwa tahadhari kwanza ili apate muda wa kumsoma mpinzani.
Benchi la ufundi simba walifanya homework yao vizuri, waliona kwenye mechi na red arrows combination ya aucho na abuya haijkaa sawa wanasimama mbalimbali sana na hawachezi katika horizontal line, kwaiyo mpango wao ulikua kufanya pressing ya haraka sana mara tu wanapopata mpira, mpango wao ulifanya kazi, simba walionekana na hatari dakika 30 za mwanzo kikwazo kilikua maamuzi yao ya mwisho pamoja na umaili wa job na baka pale nyuma.
Second half baada ya kuingia mudathir ikarudi yanga ile tunayoijua. Mudathir anatakiwa kuanza na aucho pale kati. Abuya bado hajajipata na anaingilia sana nafasi ya aziz ki pale kwenye shimo.