Misururu ya magari kwenye misafara ya ziara za viongozi wetu ni ushamba wa kizamani sana!

Kiongozi wa chama anafanya shughuli za serikali, watumishi wa serikali wanakula posho na mishahara, kiongozi wa chama anao uwezo wa kumkemea na kumuagiza kiongozi wa serikali atakavyo
Ahyan chama ndicho kinachoomba ridhaa ya wenye nchi ili kiwaongoze na kikishinda kinaunda serikali na hao watumishi wa serikali wako chini ya chama ndiyo maana ulimwoma kanali kasimamishwa ajibu mbele ya katibu.
 
Kila kitu kama USA....hivi hao ni wenzetu kujilinganisha nao ? ...ulinzi wa nchi yao na level uchumi wao ni sawa sawa....maadui wao sio sawa na sisi huku...plus uchumi hoi kbs nchi pili toka mwisho umasikini
Umeomba mfano duniani umetolewa halafu unapiga kelele tena- sijui tukusaidie nini
 
Ahyan chama ndicho kinachoomba ridhaa ya wenye nchi ili kiwaongoze na kikishinda kinaunda serikali na hao watumishi wa serikali wako chini ya chama ndiyo maana ulimwoma kanali kasimamishwa ajibu mbele ya katibu.
Sawa kaka yaza, nakuelewa sana, na probably ni katika harakati za chama kuangalia kama ilani yao inatekelezwa vyema

Lakini, ninachoona mimi binafsi ni "uitikadi na uenezi wa siasa za chama" kuliko uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya chama

At least angekuwa makamu mwenyekiti wa chama.... Ingemake sense
 
Wala nchi hao...

Hao wanaokuwa kwenye hiyo misafara wana posho zao na per diem nzuri.
 
Hio misafara ndio inayofanya malaya waendelee kulipiwa apartment maeneo mbali mbali ya jiji huku wake wakiwekewa mafuta na kununuliwa magari na watoto kusomeshwa shule za mabasi ya njano.
 
Siasa ni moja ya biashara nzuri sana, mtaji ni Watu.
 
Nini msururu wa magari, wabunge wamesema waongezewe na msafara wa ndege, zilizopo haziwatoshi
 
Kuna katajiri fulani nako kakienda kijijini kanatamba na msafara wa magari na bodaboda.
 
Hata mbowe huwa na msururu
 
 
Kwangu mimi naona viongozi bado wanaogopa kushambuliwa. Wanawaza kwamba, endapo watatumia magari mengi, labda wanadhani kuwa ndilo suluhisho la kutoshambuliwa kirahisi. Unajua kwanini? Wanawaza kwamba, kutumia magari mengi kwenye msafala, ni kumchanganya mshambuliaji asijue ni lipi gari la kiongozi husika. Ndiyo mawazo yao.
 
Mkuu acha ubishi wa kijinga
Huu ni msafara wa POTUS- Washington DC
View attachment 2901442
Ko hap maan Yako n ipi
Kwamba waongeze idadi ya magara Kwa kuchukua had wafanyakaz wa kuwafuria nguo zao Ili twende sawa n marekan
Au tujitahid kukemea wapunguze idadi ya hayo magar Kwa kujiangalia na kupunguza cost tunzozipat πŸ€”
 
Kiongozi upo sahihi sana! Kikubwa ambacho hatujajua au tunakipuuza ni kwamba waafrika wengi na hasa mashariki na kusini tuna chronic malnutrition yes tuna utapiamlo wa vizazi na vizazi so development yetu mentally inamiss sana nutrition tangu tukiwa mimba, makuzi, then social development inakuja pia kuharibiwa na wazazi wetu ambao pia wameathirika sana na utapiamlo. Tunasoma elimu zetu hazibadilishi tabia, mitazamo wana haziongezi maarifa yetu. Tz kwa mfano huwezi kutofautisha tabia na vitendo vya msomi na asiyesoma kbs, unakuta profesa kbs wa science lkn haamini kwnye science bali uchawi na matunguli. Bungeni mchango wa msomi wa juu kbs hauna tofauti na anayejua kusoma na kuandika tu! Wasomi wanaona ufahari kuitwa madokta lkn wamechangia nini kwenye taaluma zao zaidi ya kukariri kwa ajili ya mitihani wanavyopanda juu?

Tumekuwa na blabla katika kila fani iwe michezo, angalia wachezaji wetu waliokulia chips dume wanapocheza na team za wajuzi, aibu, wanasiasa wetu ndo hawa wamekulia kula mlenda na kuchunga mbuzi wakipata madaraka tu wanataka gari ya milioni 600 (kwa pesa zake hawezi kununua hata kama anazo) za serikali anasign tu na misafara yao ya kulinda ego zao. Tazama madaktari, waalimu, maengineer, wataalam wetu wengine wote maamuzi yao ya kila siku. Unasikitika na kushangaa kama wamesoma hata kidogo. Wanashauri ndege ziongezwe kwa ajili ya viongozi wakati basics kama umeme na maji hamna, chakula tu tunaagiza nje tumeshindwa kujitosheleza ngano na mafuta ya kula tu, matrilioni yanaenda nje kila mwaka! Maajabu

My 50 cents
 
Wakienda ulaya wanaona aibu maana misafara hata gari 5 haifiki
 
Ko hap maan Yako n ipi
Kwamba waongeze idadi ya magara Kwa kuchukua had wafanyakaz wa kuwafuria nguo zao Ili twende sawa n marekan
Au tujitahid kukemea wapunguze idadi ya hayo magar Kwa kujiangalia na kupunguza cost tunzozipat πŸ€”
Acheni roho mbaya- sidhani kama watu walioko kwenye magari hayo hawana maana, sababu ya kuwepo hapo wala kazi ya kufanya. Ona mambo anayofanya Makonda- suala la ardhi wanaitwa maafisa ardhi, ndoa wanaitwa watu wa ustawi wa jamii, kodi wanaitwa TRA, polisi wanaitwa polisi; ushuru anaitwa mkurugenzi na wakuu wake wa idara, utawala kwa ujumla anaitwa , RAS, RC, DC au DAS wake. Hayo tayari na magari 10
 
Hujui unachoongelea! Usalama wa kiongozi gani uko mashakani?

Baba wa Taifa alikuwa ame-limit msafara wake kwa magari matano, na hakuna kilichomtokea, pamoja na kwamba miaka ile, wazungu walikuwa wanamtafuta kwa udi na uvumba kumshughulikia. Ni ushamba, ujinga, ubinafsi wa viongozi kuwa na magari lundo, tena magari ya bei kubwa sana, na matumizi makubwa sana, huku wananchi wakilia njaa, na vitu vya msingi kama bima ya afya kwa watoto, umeme, maisha magumu na matatizo kibao! Afu eti unatetea???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…