Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Hii thread naona waliyoielewa ni wachache sana wenye exposure ya kutembea au kuishi ughaibuni.

Na wachache sana ambao wameona kwenye filamu jinsi umuhimu wa public parks ulivyo muhimu

Nimekumbuka mwalimu wangu wa falsafa mjapani mmoja alikuwa anapenda kusema akili yenye utulivu inaweza kufanya mambo mengi makubwa na katika utulivu ndio vitu vingi hutengenezwa.

Ajabu serikali ya CCM imeruhusu hapo kelele za bar, pembeni hapo huyo anacheza singeli, kulia mtu anahubiri, kushoto kuna watu wa biashara zao yaani hakuna mpangilio wapi ujue ni eneo fulani la kibiashara na wapi ni maeneo ya utulivu.
 
Mkuu! Umeongea vizuri sana! Tunashida na open space za mitaa ya kati posta! Kuna hawa kunguru wanazingua! Ukizubaa wanakuchafulia nguo na kinywaji chako. Alafu na uchafu garden hazisafishwi! Ukitembeza macho unaweza ukakutana na nnnya! Nilisomaga IFM kipindi fulani kuna garden mitaa hiyo kuelekea ukuta wa Hospitali ya Cancer patient! Hiyo sehemu ni nzuri kwa kivuli hila ni chafu!
 
Umeongea point mkuu!
 
Kama una familia na unapata stress kiasi cha kutaka kuwa mwenyewe basi ujue umeingia choo cha kike.

Hayo mambo waachie mabachela wanaosaka warembo wakuchakata ila kama una familia kaa na watoto wako na mkeo. Wanahitaji uwepo wako zaidi.
We mwenzetu unaishi kama roboti nini?
Hivi umeowa? Unakaaga nyumbani muda wote wa free time?
Ameshatoa condition kwamba kuna times unahitaji uwe peke yako.....sjui kama unamuelewa?
Utadhani kama vile ukiowa ndio sababu ukae tu nyumbani na watoto. Hao watoto wenyewe kuna times hawataki uwepo nyumbani au hujui?
 
Asante sana mkuu naona umempa za uso! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wewe utakuwa mfupi na una kitambi kikubwa maana ndiyo wenye tabia hizi unazotaka kufanya ukioa (jokes bro)πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Mimi nmekulia kinondoni kukikuwa na maeneo mengi ya wazi na garden
Na maeneo mengi huko tuliyapigania na kuyalinda na uvamizi wa kpmbvpmbv
Ila uvamizi na kuchukuliwa maeneo inategemea na wakazi majirani wa maeneo hayo watu mkilegea eneo linaondoka
Mfano jirani na makazi yangu nyuma ya mango garden kuna eneo linaitwa garden mpaka leo hii watu wanacheza michezo nk
Ukija kinondoni buibui kuna uwanja pale,kuna wakat kidogo uondoke sema wakina songoro mnyonge walikutana na mziki
Ona uwanja wa biafra ccm wamejipa wao tu wote
Wamejaza wafanyabiashara,wakati ule uwanja huo ulikuwa unatumika na watu wa care,na Black wizard
Kwanza kuanzia pale shule ya biafra sahv chuo kikuu huria kushuka chini kdg kote ni eneo la wazi watu walivamia tu

Ova
 
Zamani maeneo yalikuwa safi
Bryson alipanga vzr sana kunondoni,lami,taa ziko mtaani

Ova
 
Mimi huku Mbeya nikikosaga hela ya pombe na nikawa nimefokewa kidogo na boss ,basi naendaga milimani nakaa pekee yangu nakuwa naona mji wote naanza kuplan siku nikiwa na hela niinununue Mbeya yote alafu niwafukuze akina Mwaisa .

Haya mawazo uwa yanahitimishwa na mijusi ikija upande wangu maana ndiyo wadudu ninaowaogopa basi nitakimbia zangu kurudi kwangu,Ila hapo nakuwa niko fresh kabisa inakuwa imebaki shift ya kucheza na paka na mbwa jioni inakuwa imeingia nalala kesho niamke niendelee kulijenga taifa
 
Zamani maeneo yalikuwa safi
Bryson alipanga vzr sana kunondoni,lami,taa ziko mtaani

Ova
Yaani kulikuwa na nidham ya hali ya juu ila leo hata ndege wote wamepotea
Naona watu sasa hawana utu kabisa wala hawajali na ubadhirifu umekithiri kila mahali
Utafikiri umeme tumeuona leo kumbe maisha ya zamani yalikuwa mazuri zaidi hata currency yetu ilikuwa na nguvu sana
 
Inauma sana mkuu jinsi walivyojigawia maeneo, imagine watu wameuza mpaka maeneo ya misikiti na wamejenga daa
Nakumbuka shule ya msingi niliyosoma miaka ya zamani leo imebaki shule tu viwanja vimevamiwa vyote
Sijui kama tutavirudisha tena
Mkuu kama mlivipigania mna umoja sana kuliko hao majizi
 
Kinachofanya mkutane bar ni ufinyu wa backyard. Ukiwa na eneo kubwa kama mna ishu ya kuongea ya maana hamhitaji kukutana bar. Unafikiri madon huwa wanakutana bar kupanga mbanga zao?
Sio kila mtu utampeleka home, yaani eneo neutral kwa kila mtu, mkae muongee mambo yenu kila mtu aende mingo zake. Mbona Zanzibar tu hapo zipo recreation parks nzuri tu na ili ujue tu watu wanazipenda sana. Nilikuwa naona jinsi mida ya mchana na jioni, weekends watu wanavyoenda kupumzisha akili zao huko.

Maeneo ya wazi kwa Dar yapo mengi tu, yangefaa kutengeneza Parks ila ustaarabu wa watu wa Dar ni almost zero, serikali ya mkoa nayo imejilalia usingizi wa pono.
 
Dah ww acha tuu ndugu yangu, na Siwez kwenda pale darajani mana kuna kelele za watu na magari hvy huwezi kuwaza mambo yako atleast coco beach utanunua soda au maji unaenda kukaa kwenye mchanga unaangalia bahari siku imeisha
Na mfuko uwe safi maana nauli na muda wa usafiri kama sio garama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…