Mitaani Hakukaliki . Wananchi walipuka kwa shangwe na Nderemo baada ya Kupitishwa kwa Rais Samia Kugombea Urais

bwana luka unafaa sana kuwa mshereheshaji katika matamasha,warsha,mikutano na ziara za ndani ya nchi za rais hongera kwa kuwa na talanta hiyo ila teuzi hupati.
 
Was this suppose to be a surprise, mbona tulishaiona hii movie tayari?
 
Hii CCM ya sasa hivi inarudisha nchi kwenye ujinga tena tena.
 
Nadhani ulikuwa hujaanza kufuatilia siasa siku Nchimbi na Sophia Simba walipoitisha press nje ya ukumbi baada ya jina la Lowassa kukatwa, na ndani ya ukumbi wimbo wa tuna Imani na Lowassa ukiimbwa hadi na waziri mkuu wa sasa
Ushasema nje ya ukumbi lkn haikuwa public.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni shangwe , Nderemo,vifijo na vigelegele huku mitaaani baada ya kupitishwa kwa jina la Rais Samia kugombea Urais kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika hapo baadaye mwishoni mwa mwaka huu.

Wananchi wamejaa raha ,furaha,tabasamu na matumaini makubwa sana mioyoni mwao.Ni chereko chereko tu .ni nyuso za furaha na tabasamu ndizo zimetawaliwa kwa wananchi wengi mitaani. Ni makelele na mirunzi ya furaha ndiyo inayosikika huku mitaaani kushangilia uteuzi wa Rais Samia kugombea Urais.

Mkutano mkuu maalumu wa CCM umekata kiu ya mamilioni kwa mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo vifuani pao ya kutaka kuona Rais Samia akirejea Ikulu kwa awamu ya pili.

Hii ni kwa kuwa Mama amegusa Maisha ya mamilioni ya watanzania,ameleta furaha na tabasamu katika maisha ya watanzania,amebadilisha maisha ya watanzania na kuleta matokeo Chanya kwa watu.

Mama amewaleta pamoja watanzania na kuwafanya wajivunie utanzania wao.kila mtanzania ana amani na matumaini ya kutimiza ndoto zake na kila mmoja analiona Tumaini machoni pake.ndio sababu watu wanashangilia kwa nguvu huku wakiwa vifua wazi bila kujali baridi wala upepo. Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe.View attachment 3206839

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Upuuzi mtupu
 
CCM itapata pigo kubwa sana mwaka huu, pigo moja tu, pigo lililonyooka, pigo takatifu.
 
Hivi huoni utaratibu umekiukwa aisee janauari kutangazwa mgombea. Haya machozi yanakububujika mwenyewe.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni shangwe , Nderemo,vifijo na vigelegele huku mitaaani baada ya kupitishwa kwa jina la Rais Samia kugombea Urais kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika hapo baadaye mwishoni mwa mwaka huu.

Wananchi wamejaa raha ,furaha,tabasamu na matumaini makubwa sana mioyoni mwao.Ni chereko chereko tu .ni nyuso za furaha na tabasamu ndizo zimetawaliwa kwa wananchi wengi mitaani. Ni makelele na mirunzi ya furaha ndiyo inayosikika huku mitaaani kushangilia uteuzi wa Rais Samia kugombea Urais.

Mkutano mkuu maalumu wa CCM umekata kiu ya mamilioni kwa mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo vifuani pao ya kutaka kuona Rais Samia akirejea Ikulu kwa awamu ya pili.

Hii ni kwa kuwa Mama amegusa Maisha ya mamilioni ya watanzania,ameleta furaha na tabasamu katika maisha ya watanzania,amebadilisha maisha ya watanzania na kuleta matokeo Chanya kwa watu.

Mama amewaleta pamoja watanzania na kuwafanya wajivunie utanzania wao.kila mtanzania ana amani na matumaini ya kutimiza ndoto zake na kila mmoja analiona Tumaini machoni pake.ndio sababu watu wanashangilia kwa nguvu huku wakiwa vifua wazi bila kujali baridi wala upepo. Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe.View attachment 3206839
ta
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe jamaa ni mtu hatari sana kwa usalama wa taifa hili, hufai hata kidogo! Ajabu iliyoje ni kwamba viongozi wengi wa kiafrika wamezungukwa na watu wa namna Yako wakiwaita eti washauri wao. Viongozi wengi wanaingia madarakani wakiwa wazuri sana lkn nilichogundua wanakuja kuharibiwa na hawa machawa" wenye kivuri Cha washauri wa Rais"
Ingekuwa uwezo wangu wewe hupaswi kumsogelea Rais hata kilometer 1
 
Mimi ni mzalendo wa kweli wa Taifa na mwenye uchungu mkubwa sana.
 
😩😩
 
Attachments

  • IMG_4986.jpeg
    IMG_4986.jpeg
    124.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom