Mitambo ya kuzuia vurugu za uchaguzi wa Rais mwaka 2025 iliyonunuliwa na Serikali inatisha sana, vyama pinzani vitakapoleta vurugu vitaishia pabaya

Wapinzani hawaleti vurugu acheni uongo.

Halafu si muongeze hata ambulance au magari ya zimamoto maana ndio yenye uhitaji mkubwa.
 
Mwafrica ananunua vifaa vya kuumiza ndugu zake, huku anawabeba wageni. Hana vifaa tiba, hana miundombinu, vijana hawana ajira, shida kila kona. Hakika ngozi nyeusi kuna mahala haiko sawa.
 
Mimi ndiyo maana sioni mantiki ya kushiriki hilo zoezi la kupiga kura. Yaani uniibie kura yangu, na bado unaenda kununua gari la kunitishia!!
 
Hizo ni pesa zinazotokana na mfumo wa MUSE,hebu jiulize kwanini bajeti haikai sawasawa
 
Swa na kujenga madarasa mangapi?
 
Mwafrica ananunua vifaa vya kuumiza ndugu zake, huku anawabeba wageni. Hana vifaa tiba, hana miundombinu, vijana hawana ajira, shida kila kona. Hakika ngozi nyeusi kuna mahala haiko sawa.
Hii ni hatari
 
“Apiganiae haki atakuwa na mafanikio tele;

Bali afuataye mambo ya upuuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Mithali 28:19.

Nakumbusha tu madhara ya udhalimu, rushwa, ubadhirifu, na matumizi mabaya ya fedha za umma na madaraka
Yana athiri wote walio wa chama na wasio wa chama.
Acha ccm itawale milele
 
Huu ni mtambo?...hahaha...
 
Hakuna dolla iliyowahi ishinda nguvu ya umma pia hakuna mtanbo wa maana hapo raia wakiamua kuliamsha dude.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…