Mitambo yashindwa kuondoa mti wa asili Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Mitambo yashindwa kuondoa mti wa asili Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika mikoa ya Morogoro na Pwani imelazimika kuuhifadhi mti wa asili jamii ya Marula uliokuwa ukitumiwa na watu mbalimbali wa zamani kufanya matambiko ya asili kuwa kama sehemu ya kivutio ndani ya hifadhi hiyo baada ya kushindwa kukatika kwa zana na mitambo mbalimbali ya kisasa ili upishe upanuzi na matengenezo ya barabara kuu inayokatiza hifadhini hapo.

Huo mimi naupiga mtama mmoja tu.
 
Kijiji cha Mfuto, Ilolanguru wilaya ya Uyui. Kijiji hiki kina mti ambao ulianguka kwa miaka 3 na ukasimama ghafla tu. Watu wakachukua magome kwa ajili ya dawa. Wanaume 19 waliokunywa magome ya mti huo, nguvu zao za kiume zikaongezeka sana, ikawa tabu kwao[emoji28]. Tabora kuna mambo unaweza kudhani ni movie kumbe ni Live, hii ilitokea mwaka 2014.
Nakumbuka hata kuna sehem mbali na tabora ilitokea hiyo mti ulikatwa kesho wakaukuta kama ulivyokua[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mbona wachina sijui wajapani wakati wa ujenzi wa morogoro road pale manzese waliukata mti ,ulikuwa na imani kama hizi walikuja usiku wa manane wakaukata aubuh hakuna stori kama hii.
Kwanini usiku wa manane kama hakukuwa na stori kama hizo? Hayakufanyika matambiko usiku huo na wazee wa eneo hilo?
Dini zisitusahaulishe mambo ya mababu zetu
 
Huko Shinyanga Kuna kajumba ka bibi fulani, kila wakikiondoa kesho yake kipo vilevile. Wakaachana na kijumba na kupindisha barabara. Hayo ni mambo yetu ya Afrika, tulidharau mila zetu na kukumbatia utamaduni wa kizungu.
Hii siyo Shinyanga ni Mwanza barabara inayooandisha Bugando.
 
Umeshaharibiwa na imani za Wazungu
Na hii ndo shida kubwa inayotukabili waAfrika, unakuta mlango ukiusogelea unajigungua ukipita unajifunga, ukimwambia mtu ni uchawi atasema sayansi ya sensa. Ila fanya nyumbani kwako usiweke izo sensa za wazungu utaambiwa ni mchawi ww. Aliyetuloga sisi aisee
 
Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika mikoa ya Morogoro na Pwani imelazimika kuuhifadhi mti wa asili jamii ya Marula uliokuwa ukitumiwa na watu mbalimbali wa zamani kufanya matambiko ya asili kuwa kama sehemu ya kivutio ndani ya hifadhi hiyo baada ya kushindwa kukatika kwa zana na mitambo mbalimbali ya kisasa ili upishe upanuzi na matengenezo ya barabara kuu inayokatiza hifadhini hapo.

Hii kazi wawape wachina, wataenda saa 8 usiku kufanya kazi alafu asubuhi yake muje kuedit hii habari..

Kulikuwapo maeneo korofi hususani yanayopitiwa na barabara miti, milima, madaraja, mito, misitu, mapori lakini leo hii yamebakiza history tu baada ya tender kupewa wachina na kushughulikia.
 
Kwanini usiku wa manane kama hakukuwa na stori kama hizo? Hayakufanyika matambiko usiku huo na wazee wa eneo hilo?
Dini zisitusahaulishe mambo ya mababu zetu
Wasichokijua ..hata hao wachina na vigagula mbaya...

Walijenga huku..wanaweka vibarua mchana tu usiku wanaingia peke yao..asubuhi utakuta ukuta umejengwa kiasi ambacho kikawaida muwe 60 na zaidi ..ndio mjenge kwa usiku mmoja ..!
 
"Uokovu"tulioletewa umetufanya tukipuuze kila kilicho imani ya kishirikina. Wenzetu wa rangi zingine ushirikina huufanya kwa manufaa makubwa kimaendeleo
 
Back
Top Bottom