Mitambo yashindwa kuondoa mti wa asili Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Mitambo yashindwa kuondoa mti wa asili Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Dodoma Mjini kabisa karibia na St Gasper Hotel kuna mbuyu upo pembeni kabisa ya rami, barabara ya rami imepita pembeni yake kabisa. Umeshindikana mpaka leo. Aise dunia ina mambo.

Kumbuka ule mti ulikatwa kule Tabora asubuhi wakaukuta umesimama tena, wanume wakachukua magome yake wakaenda chemsha wakanywa wakawa na nguvu za kupitiza. Hahahaha!
Yes, ni 2015 hiyo, Kijiji kinaitwa Nkrurusi Wilaya ya Tabora
 
Huko Shinyanga Kuna kajumba ka bibi fulani, kila wakikiondoa kesho yake kipo vilevile. Wakaachana na kijumba na kupindisha barabara. Hayo ni mambo yetu ya Afrika, tulidharau mila zetu na kukumbatia utamaduni wa kizungu.
Mila zenyewe ndio hizo unataka kukata mti ufanye maendeleo mti hautaki, lini utaondoka haijulikani, sasa ni mila gani hizo??? aacha mzungu aitwe mzungu.
 
SIBISHI [emoji817]
Chang'ombe walishaiondoa ilibidi nasikia wamtumia mjukuu wa bibi, yule bibi alikua na mjukuu wake anampenda sana ndo akipika bibi anakula la sivyo hali, wakamseti dogo na kumpatia nyumba sijui wapi?

Bibi akapikiwa chakula na mjukuu kisha mjukuu akamchanganyia na dawa za usingizii, bibi anazinduka yuko kwingine uko ndo kufanikiwa kuivunja ile nyumba pale.

Ila Makulu pale karibu na sheli GP88 ndo imeshindikana kila wakija wanaona bahari nyumba haionekani. SGR imepita pembeni yake aisee![emoji28]
 
Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika mikoa ya Morogoro na Pwani imelazimika kuuhifadhi mti wa asili jamii ya Marula uliokuwa ukitumiwa na watu mbalimbali wa zamani kufanya matambiko ya asili kuwa kama sehemu ya kivutio ndani ya hifadhi hiyo baada ya kushindwa kukatika kwa zana na mitambo mbalimbali ya kisasa ili upishe upanuzi na matengenezo ya barabara kuu inayokatiza hifadhini hapo.

Huo sio mti tu km unavyouona!
Ni madhabahu ya Giza!
 
Kifikra let say ukauona mti fulani ukaunyenyekea ukaanza kuweka mchele unga maziwa ukazidi ukaunyenyekea ukauchinjia mnyama kama ngombe,mkaueshimu mkautamkia maneno ya kuutukuza,hayo maneno yanakwenda kuumba DEMON,that mean circuit completed Demon must born there.
Ni nguvu za Giza tu ! Lucifer ktk ubora wake! Demon ni mapepo
 
Mbona wachina sijui wajapani wakati wa ujenzi wa morogoro road pale manzese waliukata mti ,ulikuwa na imani kama hizi walikuja usiku wa manane wakaukata aubuh hakuna stori kama hii.
Unafikiri walikata tu?
 
Kijiji cha Mfuto, Ilolanguru wilaya ya Uyui. Kijiji hiki kina mti ambao ulianguka kwa miaka 3 na ukasimama ghafla tu. Watu wakachukua magome kwa ajili ya dawa. Wanaume 19 waliokunywa magome ya mti huo, nguvu zao za kiume zikaongezeka sana, ikawa tabu kwao[emoji28]. Tabora kuna mambo unaweza kudhani ni movie kumbe ni Live, hii ilitokea mwaka 2014.
Ni nguvu za Giza,unakuta ni madhabahu hizo.
Tabora hukohuo pia,kuna mtumishi alikuwa anaombea eneo,vunja madhabahu za giza na kusimamisha madhabahu ya Mungu!
Weee kuna mti wa miaka ulikuwa unaogopwa,ulianguka wenyewe mpk mizizi ikang'oka ,ukiwa mbichi kabisa kipindi km cha masika!

Kesho yake asubuhi wakakuta moto unawaka ndani ya mti km vile mti mkavu ,na mtu kawasha moto humo ndani,uliwaka zaidi ya siku 2 mpk uliteketea!
 
Hayo mauza uza yapo ni lzm uongee na wazee wakupe ruhusa.Maeneo mengine ni kambi za kutunzia misukule, matambiko,madhabau za kichawi,milango ya kuzimu,nk.
Ila unatakiwa watumishi wa Mungu wa kweli tu wenye nguvu za Mungu kumaliza hivyo vitu na inaisha sio tens kwenda kwenye nguvu za giza.
 
Back
Top Bottom