Mitandao ya simu kazi yake ni mawasiliano, si kutoa huduma za kibenki

Umesahau hata swala la mawasiliano
Ni kazi ya shirika la posta sio wao 😁😁
Tuendelee na barua tu
 
Mitandao ya simu hawajalalamika kwa kuwa kwanza hiyo tozo wao haiwahusu.Ndio maana ukituma pesa wanakwambia kabisa kwamba makato yao ni kiasi kadhaa na tozo ya serikali kiasi kadhaa.Kwa hiyo mantiki yako haieleweki.
 
IMEANDIKWA WAPI?
 
mim nashaur.wasiwe wanasema tozo yetu kias kadhaa. cha serikal kias kadhaa
inakua kama wanawachongea
 
eti huyu nae ni msomi hii nchi ime logwa kwa kweli
sio kwa huu umbumbu wa mtoa mada
[emoji706][emoji706]
 
Bado tuna safari ndefu sana ya kupiga hatua ktk maendeleo yetu sisi wenyewe.
nilishuhudia nikiwa kijiji kwetu kundi moja la wakazi wakitaka zahanati ijengwe eneo fulani pia kukajitokeza kundi jingine wakipinga zahanati isijengwe.
naaamini mifano hii ipo ktk kila maeneo yetu.
Pia siwezi kushangaa hili la tozo ya miamala, wapo wanao furahia kulipa wakitarajia mambo mazuri lkn wapo wengine pia kwa roho zao zilizo jaa "ushetani" hawataki kabisa kuona mafanikio yanatokea ktk nchi, watu wa aina hiyo kwa lugha rahisi tunawaita "wachawi" wa maendeleo.
Tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu.
kama kunahitajika marekebisho yanaweza kufanyiwa kazi mbele ya safari lkn tusiwakatishe tamaa na kuwababaisha watanzania.
 
Serikali kamwe isijaribu kurudi nyuma,
ikibidi basi, irekebishe tu viwango viwe reasonable. lkn tozo iwepo pale pale, kila mtanzania achangie maendeleo yake.
 
Hapa ndio tunapopaswa kuishi kwa uhalisia wa hali yetu. Kwamba huduma za kifedha au mabenki kama taasisi, yameshindwa kuwafikia na kuwahudumia watu wote kutokana na ubovu wa mifumo ya miundombinu na pia kukosekana kwa shughuli za kueleweka na kuaminika za kiuchumi za hao watu, kiasi kwamba hizi taasisi hazioni au hazitapata faida ya kuwepo huko wakilinganisha na gharama za uendeshaji. Bado tunaamini tuko uchumi wa kati?
 
ndo kodi iwe mara mbili kwa transaction mkuu?kuna vat si ya serikali pia unazani na makato ya mitandao serikali hawachukui?
 
Serikali inaweza kufanya adjustment lkn pia Serikali isisahau kuwa wananchi hao hao wanataka pia Huduma bora za barabara, hispotali, elimu n.k, na endapo wananchi watakosa barabara bora, huduma za afya bora na elimu bora lazima tutalalamika.
Hivyo serikali kazi kwao.
 
Kumbe wanga wa maendeleo bado wapo? aisee!! Tz hatari?
 
Bandiko lako ni nzuri sana, japo ni fupi na kuna baadhi naamini umewaacha.

Ila upande wangu naunga mkono, kitu kinachojitokeza nikuw makampuni yasimu yanafanya biashara za kifedha nje ya taratibu za lesen zao (hata kama wanalipia) wao wanatazam zaid faida kwa upande wao.

Serikari kwa kuliona hilo imewawekea kizingiti ila kwa jeuri zao na wao wanajimwamba fai.

Kifup lengo la serikari ni kupata mapato zaid, ila ubaya nikuw aneumizwa ni mwananchi maana makampun hayataki kuguswa.

Pendekezo langu serikari itazame upya hizi kodi hata kama wanalengo zuri ila limekuwa mzigo sana, lakini haya makampun yaache upuuzi wao tunajua wanapenda upigaji sana na wanapenda tukosane na serikari............ hakuna marefu yakakosa nchaa
 
Huyu TAGA aliyeanzisha huu uzi hata hajui anataka kuwaaminisha watu kitu gani, inamaana hajui umuhimu wa simu hasa kwenye suala la fedha huko kijijiji kwao ambako hata umeme haupo? kuna mijitu wakati mwingine unajiuliza kwanini ilizaliwa. Stupid Fellow
 
Umechanganya mambo hapo. Kwamba wateja tukubali yaishe na tuendelee kulipa tozo hii isiyo rafiki. Pili makampuni ya simu yakubali yaishe kwa vile yamekwishavuna sana katika biashara hii. Waionaje hali ilivyo sasa baada ya wahusika kukiri mapungufu yaliyomo katika kanuni zao kandamizi?
 
Maendeleo yanapotokea vitu vingi hubadilika, siku hizi unaweza fanya chochote na simu, saaa, kalenda, tochi, calculator,camera vyote vipo kwenye simu hivyo kazi ya mpiga picha, muuza saa, muuza calendor vilichukuliwa na simu za kisasa, kwa makampuni kufanya kazi za kibenk hakuna cha ajabu kabisa.
 
Kutuma SMS sio KAZI ya simu ni KAZI ya shirika la posta lenye wajibu wa kutoa huduma za kupeleka barua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…