Ni upumbavu wa hali ya juu unachotetea ni ujinga.
Jana mimi nimemtumia mtu 20000 nimekatwa mimi kama mtumaji 1560, yeye anaenda kukatwa zaidi ya 2000 atakapotoa hiyo pesa. Hebu fikiria muamala unakatwa zaidi ya 25% ya kiasi ulichotuma kama gharama.
Na watumiaji wengi wa hizi huduma ni watu wa chini wanaotuma na kupokea 5000, 10,000, 20000, 30000 kama mtu ana pesa nyingi kuanzia milioni mara nyingi ataenda benki au kwa wakala wa benki tu kudeposite.
Sasa mtu kama huyu anayetuma na kupokea 20,000 eti umkate almost 5,000 ni upuuzi.
Nchi hii ina kila aina ya neema,kuanzia madini mpaka ardhi, yani ni upuuuzi serikali kumkamua mwananchi eti kujenga barabara sijui kufanya nini kama vile nchi haina rasilimali.
Yani serikali imeshindwa kusimamia rasilimali zetu kuanzia dhahabu, ruby, chuma,gas, ardhi, bahari, tanzanite, bandari tukaweza kujenga nchi mpaka imkamue mwananchi hadi pumzi ya mwisho.