Mitandao ya Twitter na YouTube haipatikani Tanzania bila VPN | Septemba 07, 2021

Mitandao ya Twitter na YouTube haipatikani Tanzania bila VPN | Septemba 07, 2021

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Katika hali ya kushtusha Leo 7/9/2021 majira ya kuanzia saa 5 na nusu, mitandao maarufu ya kijamii Twitter na YouTube haipatikani bila VPN.

Mtumiaji atalazimika kuwasha VPN ili kuendelea kufurahia kutumia mitandao hiyo. Mitandao hiyo siku za karibuni imekuwa ikitumika kama platform ya chama upinzani(CHADEMA) kujadili ajenda zake, mfano CHADEMA wamekuwa wakitumia jukwaa maarufu la Twitter lijulikanalo kama SPACE na Pia imekuwa iktumia mtandao wa YouTube kushea matukio yake mbalimbali.

Chama kikuu cha upinzani kimelazimika kutumia zaidi mitandao ya kijamii kwa shughuli zake za ukuzaji chama baada ya mazingira ya kukutana ana kwa ana ndani ya nchi yao kutokua rafiki.
 
Au ndio mambo ya Tozo yanaanza kupikwa ?

Huyu Mshauri Mwigulu ni mshauri mzuri sana ningependekeza apelekwe kwenye wizara nyingine (ambayo haina impact sana ) akashauri huko..., sababu tukiendelea na ushauri wake kesho yetu huenda ikawa ngumu kuliko leo
 
yule bwana wa kule twitter hana lolote siku hizi ,labda wanataka kufanya maamuzi mazito kuhusu Mbowe kwahiyo wanapima upepo
Yule jamaa amechoka ndembendembe, Sijui hata siku hizi atakua anapost Nini.
 
Back
Top Bottom