Katika hali ya kushtusha Leo 7/9/2021 majira ya kuanzia saa 5 na nusu, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) imefungia matumizi ya mitandao maarufu ya kijamii Twitter na YouTube.
Mtumiaji atalazimika kuwasha VPN ili kuendelea kufurahia kutumia mitandao hiyo.Mitandao hiyo siku za karibuni imekua ikitumika kama platform ya chama upinzani(CHADEMA) kujadili ajenda zake, mfano CDM wamekua wakitumia jukwaa maarufu la twitter lijulikanalo kama SPACE na Pia imekua iktumia mtandao wa YouTube kushea matukio yake mbalimbali.
Chama kikuu cha upinzani kimelazimika kutumia zaidi mitandao ya kijamii kwa shughuli zake za ukuzaji chama baada ya mazingira ya kukutana ana kwa ana ndani ya nchi yao kutokua rafiki.