Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

WANASHERIA WATAKIWA KWENDA MAHAKAMANI

TATIZO SI SHERIA AU MAHAKAMA. NI INTEGRITY NA CREDIBILITY


Mabandiko ya mwanzo tumezungumzia sana kuhusu integrity (yaani kuamin katika uadilifu na maadili ya juu kabisa) na credibility (ubora katika imani ya kushawishi na kuaminika).

Haya mawili ni sehemu ya mambo kama uchaguzi. Uchguzi kuwa free and fair haimaanishi una integrity au credibility.

Tukahoji, wale wanaosema uchaguzi wetu ulikuwa huru na haki, je ulikuwa na credibility na integrity?

Tatizo la kukosa credibility na integrity ndilo linataka kutumiwa na baadhi ya wanasheria kupindisha mambo

Mwanasheria wa zamani wa ZNZ anataka uchaguzi urudiwe, la sivyo wanaolalamika waende mahakamani.

Hoja yake ingekuwa na maanaa kama tu , kwanza, kuna sheria inayoruhusu matokeo kuhojiwa mahakamani

Hata hivyo, katika hali ya giza, tufikirie kuwa kwenda mahakamani ingetoa suluhu,CUF wana sababu ya kukataa

Mahakama zina majengo, wanasheria na sheria zinazowaongoza na ni huru kabisa.

Hata hivyo, Uhuru wa mahakama hautoshi bila imani na kuaminika. Hapa ndipo tunarudi katika credibility na integrity

Tunajua, aliyekuwa Jaji mkuu wa JMT, aliyeshika nyadhifa mbali mbali bara/visiwani, alichukua fomu za Urais CCM.

Utata uliuibuka lini alianza kuwa mwanachama wa CCM na kimaadili hilo linaruhusiwa kwa nyadhifa alizowahi kushika?

Kujitokeza kwa Jaji kuwa mgombea kuliondolea mhimili wa mahakama credibility na integrity katika masuala ya uchaguzi

Watu wanajiuliza, kama hiyo ndiyo hali, haki inawezaje kupatikana katika utata kama uliojitokeza?

Nani anayejua watakaongoza kesi na mapenzi yao iwe kwa CUF au CCM hata kama hawana mapenzi yoyote?

Tunarudi kusema, uhalali wa jambo haukamiliki kwa uhalali tu bali kuaminika, kuaminiwa na kushawishi uhalali huo.

Integrity na credibility ni vitu muhimu,CUF wana duku duku la mahakaman, kimantiki tu linaweza kuwapa advantage.

Mwisho tusistize hatuna maana yoyote ya kuhoji uadilifu na maadili ya mahakama.

Tunachokifanya ni kuonyesha tu wasi wasi na kumjibu mwanasheria aliyetaka watu waende mahakamani kwa mifano.

Kwamba, wanaokataa si kuwa wanakataa bali wana hoja zao.

Je, hoja zao zina mantiki au la, hilo kila mmoja ataamua. Tunachojaribu ni kuieleza hali ilivyo

Tusemezane
 
Home

Baada ya kudonoa donoa kuhusu uchaguzi kutoka pande zote, tutaendelea kudonoa na habari tuliyowahi kuieleza

Tumesema mara nyingi, Rais wa JMT aanakabiliwa na changamoto nyingi, kubwa sana ni kukosa mass support
Kwamba Taifa limeduwaa, watu hawana raha na kuna manung'uniko yaliyojaa vifuani si hadharani

Pitia hiyp link hapo juu halafu tutajadili kwa kina.

Itaendelea.....
 
''WANATUPA VITAMBULISHO, HAWATAKI KUPIGA KURA TENA''

Gazeti la The Guardian katika link hapo juu linaonyesha hasira za wananchi kufikia kutupa vitambulisho vya kura

Hoja kubwa ni kutokana na jinsi wanavyoliona zoezi la kura lilivyoendeshwa

Tunasema, ni makosa wananchi kutupa hati zao za kupiga kura.

Uchaguzi ni zoezi endelevu na makosa ya uchaguzi mmoja yasitumike kuathiri uchaguzi mwingine

Hata hivyo, ni muhimu kusikiliza kwanini wananchi wanatupa vitambulisho vyao

Ipo hoja nzito wengi wasiyotaka kuisikia au kuiona baadhi ya viongozi na wapambe wao

Kwamba uchaguzi haukuwa na integrity na credibility. Hilo hasa ndilo linalowasukuma wananchi watupe vitambulisho

Tumesema mara nyingi kuwa kushinda au kushindwa si hoja, hoja ni utaratibu mzima kuonekana ukiwa na uaminifu, maadili na unaoshawishi kuwa kilichotokea ndicho kilichofanyika katika sanduku la kura

Kunapokuwa na mchakato unaoacha wananchi katika hali iliyopo, lipo tatizo kubwa.

Tatizo si kutupa vitambulisho tu na kuidharau hatua nzima ya demokrasia, bali kuonyesha jinsi ambayo sehemu ya Taifa ilivyo na manung'uniko na isivyo na raha

Inaweza kuwa ni asilimia 40 au 50 lakini ni sehemu muhimu sana ya jamii isiyoweza kupuuzwa

Matokeo yanaweza kuwa ya haki na sahihi, lakini je, mchakato mzima umeweza kuondoa hofu hiyo ya wananchi?

Endapo tutakubaliana umma una mashaka, basi zoezi zima lina mashaka kwa kukosa kuaminika hata kama kilichofanyika ji kweli. Kukosa imani na zoezi ni jambo kubwa lisiloweza kupuuzwa

Ni muhimu kuwepo na hatua za mkusudi za kuliunganisha Taifa bila kujali matokeo ya nani kashinda nani kashindwa

Hatua hizo kwa mtazamo na maoni yetu zitasaidia serikali kuungwa mkono na Taifa badala ya kuwa Taifa lenye rangi rangi

Amani na utulivu wetu ni pamoja na kuwa wamoja, kusimama pamoja kama Taifa

Tunashauri haya

TUME YA UCHAGUZI IJIUZULU

Tume kujiuzulu kuna maana moja kubwa, kurudisha imani kwa wananchi kuwa sisi ni taifa moja na kwamba hakukuwepo na namna nyingine tofauti kama inavyodhaniwa au kuhisiwa

Kujiuzulu hakuhalalishi malalamiko dhidi yao, ni njia ya kujenga umoja na serikali kuungwa mkono na wananchi wote

Bado tunaweza kuwa na tume ya mpito kwa chaguzi za dharura, hata hivyo suala la Katiba halina budi kurudi mezani

Ukisoma maoni ya watu katika gazeti hilo, wengi wanasema hawatapiga kura chini ya Tume ya uchaguzi iliyopo

Hii maana yake ni kuwa hawana imani na tume kusimamiza chaguzi.

Wanapokosa imani maana yake zoezi zima linaweza kuwa huru na la haki lakini likakosa integrity na credibility.

Hilo ni tatizo kubwa maana kutakuwa na mivutano kila mara, na wananchi kuacha kushiriki katika kuchagua na kuongoza nchi kama wadau wa mihimili miwili ya nchi( Serikali na Bunge)

Hivyo ni wakati sasa tume ya uchaguzi ijiuzulu katika kurudisha imani na kuponya makovu makubwa yanayoligawa Taifa

Hatuwezi kwenda mbele tukiwa katika mfungu fungu, tunatakiwa tuwe kitu kimoja na hapo ndipo NEC inapotakiwa kujitazama kama ina aminiwa tena kusimama zoezi zima

Pamoja na yote hayo, Wapinzani wanatakiwa kusoma na kuelewa kuwa hoja za wananchi kwasababu ni zile tulizosema
Kwamba, watangaze kutoshiriki chaguzi nyingine chini ya tume iliyopo na mfumo uliopo

Warudishe agenda ya Taifa kujiandikia nyaraka yao(Katiba) itakayokuwa na maboresho ya Tume ya uchaguzi

Wachague viongozi wanaoweza kuelewa hoja za wananchi na kuzisimamia.

Na hapo ndipo wanatakiwa waongeze mabadiliko kuanzia kwao wenyewe na si kunyooshea watu vidole.

Uongozi uliopo umefanya haya haya kwa miaka kadhaa, ni wakati wa kutafuta uelekeo mpya

Tusemezane
 
RAIS MAGUFULI NA BUNGE LA JMT

NINI TUTARAJIE

Awali ya yote kuna video hii inayotoa maelezo ya kina kama tulivyowahi kuyaeleza, kuhoji au kuuliza kuhusiana na sakata la uchaguzi wa visiwani (Kwa hisaini ya Mzalendo.net na Channel 10)
Ukweli unapodhihiri - Mzalendo.net

SUALA LA ZNZ

Hoja zote zimetolewa,ni dhahiri kuwa CCM pamoja na kushiniliza uchaguzi urudiwe, kifundi wamekwama

M/kiti wa ZEC iwe yeye au washauri wake, walifanya makosa ya kifundi katika barua ya madai 9 uchaguzi ZNZ kufutwa

1. Tulieleza hapa duru, uchaguzi haufutwi ni takwa la kikatiba.
Uchaguzi unaarihishwa hata kama ni miaka 3 au 4. M/kiti wa ZEC katika taarifa alisema amefuta .
Taarifa ya msemaji wa serikali imesema tume imefuta matokeo.
Hilo lilikuwa kosa la kwanza kiufundi pengine kutokana na haraka au shinikizo

2. Mwnyekiti wa ZEC alitangaza kama yeye, na hakuna kifungu kinachompa malaka hayo.
Tume ni timu si mtu, yeye ni kiongozi tu wa tume si tume kamili. Kosa la kifundi

3. Mwenyekiti wa ZEC hakuanisha kifungu kinachompa mamlaka ya kufuta uchaguzi.
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana kifundi linalohitimisha tatizo zima la mgogoro wa ZNZ

Madai mengine yaliyotolewa hayakuwa na maana au uhusiano na uchaguzi.

Kwamba, mgombe wa CUF kajitangaza, hilo ni kosa la jinai na tume haina mamlaka ya kumshtaki.
Inachoweza kufanya ni kuwa shahidi upande wa mashtaka.

Kwa maneno mengine ni kosa la kisheria linalohusishwa na uchaguzi lakini si kosa la uchaguzi.
Hivyo mkondo wa sheria ndio unaotumika bila kuathhiri matokeo ya uchaguzi

Hoja za wajumbe wa tume kupigana hazina ushahidi wa maeneo wala wahusika.
Hoja za kuibiwa masanduku hazina ushahidi kwasababu hakuna msimamizi wa jimbo aliyelalamika.

Na hoja kuwa vyama vimelalamika, hakuna isipkuwa CCM bila ushahidi,mashahidi wa CCM ni mawakala walio sain matokeo

Na kosa lingine la kifundi ni kutokuwa na malalamikaji kama tulivyo wahi kueleza.
Yule aliyopo hakulalamika katika kituo au jimbo, na alisubiri masaa zaidi ya 48.

Hoja inayozika suala la ZNZ na kuilazimu ZEC kutangaza matokeo ni moja tu.

Mamlaka ya kufuta uchaguzi yamepatikana wapi na kwa njia gani na sababu zipi ndani ya sheria. Jibu ni hakuna, hivyo hakuna budi kutangaza matokeo.

Hili ndilo kosa kiufundi linalozika hoja ya CCM katika mtindo wa 'technical knockout'

Tumekumbusha haya kwasababu Rais atakapofungua bunge hoja ya ZNZ lazima iwe mezani.

Hakuna namna hilo linaweza kukwepeka. Hivyo, tuna angalia hotuba yake katika mtizamo ufuatao

Inaendelea....
 
RAIS NA HOJA YA ZNZ

Rais aliyeondoka alimwachia ajaye suala la ZNZ bila ufumbuzi.

Pengine alijaribu kujiweka mbali kwani tatizo ni pana linaloweza kuathiri muungano wa nchi hizi

JK alionja joto la muungano kukaribia kusambaratika mikononi mwake.Hakutaka historia ijirudie mikononi mwake

Rais hana budi kuingilia kati ili kumjengea taswira kama Rais wa muungano

Huenda kimya chake kikawa na sababu, hata hivyo kuna hali hizi mbele yake

Kwanza, Rais anaweza kutoliongea na kulirudisha kwa wznz waamue hatma yao.

Akifanya hivyo, atakuwa ameuingiza muungano katika wakati mgumu.

Kwa maneno mengine atakuwa amejiondolea dhamana ya Rais wa JMT na hadi hapo anakuwa Rais wa Tanganyika.

Pili, akisisitiza msimamo wa CCM kurudiwa uchaguzi, atakuwa amepoteza taswira yake na ya nchi mbele ya dunia

Wageni na waangalizi wakiwemo wa nchi za Afrika wametoa maoni hakuna tatizo bali limetengenezwa.

Kwenda kinyume na matakwa ya wananchi kunaweza kuzua balaa tusiloombea

Rais atahusishwa kama kiongozi wa nchi mbele ya sura ya kimataifa

Tatu, kwavile CCM na hasa wahafidhina hawana hoja tena za kisheria, suala la kutangaza matokeo kama yalivyo halikwepeki.

Rais anaweza kuchukua maamuzi magumu yatakayomjengea heshima na taifa kwa ujumla kama atatoa tamko la matokeo kutangazwa

Hapa duru tunasema, kwa hali ilivyo ya nchi kwa ujumla, tunategemea Rais ataitumia fursa hiyo kufanya yafutayo

-Kwanza, kuonyesha yupo tayari kufanya kazi na kufanyia kazi maamuzi ya wananchi.

Hilo impact yake itagusa bara ambako uungwaji mkono una walakini, hali ya kisiasa bado inahitaji maridhiano na umoja

- Ataweza kutangaza kumalizika mgogoro ili ku score politicala point kutoka visiwani

- Ataweza kutangaza kumalizwa kwa shauri ili kuepuka matatizo makubwa yanayoweza kuibuka visiwani

- Anatambua uenyekiti-CCM ni madaraka yanayokuja, lazima adhibiti wahafidhina kwa mustakabali wa Taifa kwa ujumla

Kwa mtazamo wetu, tunaweza kusema (predictions) kuwa baada ya kumaliza hotuba suala la ZNZ litakuwa kimefikia mwisho.

Hotuba inaweza 'kuwafubgua' wahafidhina CCM ZNZ wasiotaka mshindi atangazwe kwa hofu ya kupoteza nguvu za kisiasa visiwani

Kwa mtazamo wa kisheria, kimantiki, hekma,na mtazamo wa jamii nzima,CCM hawana hoja na inaonekana wameshakubaliana na hali.

Kinachotakiwa ni mtu wa kuwafungua kamba, na hilo linaweza kutokea Ddodoma

Tusemezane
 
LA ZNZ SASA LATUA MUUNGANO. RAIS KUANZA NA MTIHANI WA DIPLOMASIA

SPIKA KUWEKA 'MSINGI' WA UENDESHAJI WA BUNGE KWA MIAKA 5 IJAYO

UKAWA WAMWEKA RAIS NA SPIKA NJIA PANDA

Mara kadhaa tumesisitiza kuhusu tatizo la ZNZ na jinsi linavyoweza kuathiri Muungano

Leo UKAWA wamemwandikia Spika kutaka kujua hatma ya hotba ya Rais bungeni bila wabunge wa ZNZ

Walichokifanya UKAWA ni timing, sasa wana mtu wa kujibu hoja zao(Spika) na kuweka shinikizo kwa JMT kumaliza tatizo

RAIS

Ikumbukwe 'hatukumuona' Rais wa ZNZ wakati wa kuapishwa Rais-JMT. Busara zilizesema hivyo mbele ya nchi na dunia
Pengine alikuwepo, tunachosema hakuonekana na tunasimama kusahihishwa

Katika hali iliyopo, uwepo wa Rais wa ZNZ unahojiwa na UKAWA kwa mantiki na vifungu vya sheria.
Wapo wanaosema uwepo wa Rais wa ZNZ madarakani ni kisheria, UKAWA wanasema keshamaliza muda wake

Kwa Rais hili ni changamoto ya kwanza ya kidiplomasia na kisheria.
Kwamba, madai yanakuja akielekea kuweka agenda kadhaa ikiwemo urudisha umoja na uzalendo

Endapo itaamuliwa tu Rais wa ZNZ awepo, hilo litamuondolea Rais wa JMT imani
Lipo kundi litakaoona nchi inaongozwa kwa nguvu na sheria inafuata badala ya kinyume chake

Kwa maneno mengine, Rais wa JMT wa wote atakuwa amechukua upande tayari, na hilo linaweza kuchochea hali tusiyoitaka itokee visiwani. Yaani litaondoa watu kutoka meza ya majadiliano

SPIKA

Mzigo mkubwa na mzito upo kwa Spika. Tuliona bunge la 10 lilivyokosa umoja na kupoteza maana yake halisi

Udhaifu wa Spika ulichangia, Kwamba, kuendesha bunge kwa nguvu na si kanuni kulishusha hadhi ya kiti na bunge

Tulishuhudia jinsi bunge la katiba lilivyoendeshwa kibabe, likafanya aibu kukidhi haja za wasiotaka muafaka wa kitaifa

Hili la kesho ndilo linaloandika mtazamo wa Spika kwa miaka 5 ijayo

Kama likiwa handled vema na kwa ustaarabu Spika atapata heshima za makundi yote na kazi yake kuwa rahisi sana.

Kama Spika atafuata uchama na kuacha kufuata kanuni, sheriao, miongozo au busara, kwa maneno machache atakuwa amejitangazia mgogoro na ukosefu wa ushirikiano

Naye anaweza kujikuta katika hali iliyowakumba Spika wa bunge la 10 na mwenyekti wa bunge maalum la katiba

Tumkumbushe Spika kuwa,mwenyekiti wa bunge maalum la katiba , pamoja na jitihada zake kusaidia matokeo ya kazi ile yamehitimisha safari yake ya siasa katika hali ya dhalili

Spika wa bunge la 10 aliamua kustaafu, kama angerudi asingepata ridhaa ya kuongoza kutoka ndani ya chama chake

Ni vema Spika wa bunge la 11 akatumia busara zake kuhakikisha majibu yake yanatosheleza kiu si ya wapinzani bali ya umma kwa ujumla.

Akiamua kwenda kwa mwendo tofauti, atakuwa amejenga msingi uwe imara au mbovu wa shughuli zake kwa miaka 5

Tuone ubabe na hasara zake

Inaendelea...
 
UBABE

Miongoni mwa mambo yaliyowaudhi wananchi ni ubabe uliotumika katika mabunge yote mawili.
Hilo lilikiweka CCM katika wakati mgumu wa kampeni. Na pia, tumeona ubabe ulivyoshindwa katika masuala ya kitaifa

Kushindwa kwa katiba mpya kulianza mwenyekiti alipotumia kila nguvu kuhakikisha Rais anahutubia baada ya Tume ya ya Warioba,kinyume na taratibu na kanuni.

Huo ukawa mwanzo wa uhasama uliozaa UKAWA

CCM wakabaki wenyewe, wakashindwa kuandika katiba na kutia wananchi hasira zilizowagharimu sana katika uchaguzi

Na tunaona tena bunge la 10 na la katiba lilivyoleta ufa katika umoja wetu.

Bado tuna makovu yasiyosemwa ya uchaguzi. Huu si wakati wa kuongeza majeraha, ni wakati wa kukazani dawa yapone

Nchi haifanikiwi kwa mtu au kikundi cha watu. Na wala Taifa halifanikiwi kwa kuendeshwa kwa maguvu bali sheria

Hakuna mshindi wa katiba mpya, lazima tujifunze kuanzia hapo.

Sote tifanye kazi kwa pamoja, na njia rahisi ni kufuata sheria tulizojiwekea, kanuni na ikibidi busara zetu

Hili la kesho, ni mtego na mzigo mzito kwa Rais na Spika wake

Tusemezane
 
KAULI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JMT

Akihojiwa na kitu cha TV , mwanasheria mkuu wa JMT amejibu hoja za wapinzani kuhusu uhalali wa Rais wa SMZ kuhudhuria uzinduzi wa bunge

Kwanza, kama ilivyoriporiwa , wapinzani walimwandikia Spika wa bunge. Kwa maana nyingine waliwasiliana na mkuu wa mhimili mmoja wa dola kujua hatma ya hoja zao. Hivyo, ni dhima ya Spika kuwajibika wapinzani kama mkuu wa mhimili huo

Inapobidi, mwanasheria wa serikali anatoa ufafanuzi na pengine ingekuwa vema Spika angenukuu ushauri au kuwa pamoja na mwanasheria wa serikali wakati wa kutoa kauli. Kitendo cha mwanasheria kuzungumza akiwa ni mwakilishi wa mhimili ''unaolalamikiwa'' kinachanganya umma

Hata hivyo, kauli ya mwanasheria imejikita katika kunukuu katiba ya ZNZ na ile ya JMT ili kujenga hoja
Tukumbuke kuwa tangu tatizo limetokea , mwanasheria mkuu wa JMT hakuwahi kutoa ufafanuzi wa kisheria
Anapojitokeza sasa hivi, ni sawa na kuzungumzia jambo likiwa limeshasonga mbele

Iwapo amenukuu katiba ya ZNZ na kukubaliana na hoja kuwa uchaguzi umefutwa kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ZEC huru, swali, uchaguzi huo umefutwa kwa kifungu gani cha sheria cha katiba hiyo anayoizungumzia

Haitoshi kusema ZEC imeona kuna matatizo ikafuta uchaguzi.
Alipaswa kusema, baada ya kuona kuna tatizo ZEC ilifuta uchaguzi kwa kutumia kifungu namba kadha wa kadha.

Na anaponukuu kauli ya ZEC kufutwa uchaguzi, huku kukiwa na kauli ya SMZ ya kufuta matokeo kuna walakini
Uchaguzi ukifutwa ina maana wabunge wa ZNZ nao wanafutwa kutoka bunge la JMT

Hatuna uhakika ni kipi kinazungumziwa, kufta uchaguzi au matokeo. Na kama ni matokeo ni yapi, ya wabunge waliopewa vyeti vyao vya ushindi na Urais au ni matokeo ya Urais?

Hapa haina maana anaingilia uhuru wa ZNZ bali ananukuu kifungu kama alivyonukuu vingine.
Kwa mfano, alinukuu katiba ya ZNZ inayotoa nafasi kwa Rais kuendelea na Kutoa kifungu kujenga hoja

Vivyo hivyo alipaswa kunukuu kifungu kutoka katiba ya ZNZ kinachotoa uhalali wa ZEC kufuta uchaguzi

Pamoja na hayo, bado hakuangalia jambo hili kwa mtazamo mpana. Anaposema ZEC imefuta wakati umma unajua aliyefuta si ZEC kwa vile hakuna kumbu kumbu za kikao chochote cha ZEC, anajichanganya

Hii maana yake,mwanasheria amekubali kuwa mwenyekiti wa ZEC ndiye ZEC kamili.
Kisheria angetuonyesha wapi ZEC inakuwa mtu mmoja. Ikiwa wajumbe 2 walijiyokeza na kusema hakukuwa na kikao, na ikiwa hakuna aliyekanusha, wapi mwanasheria anapata hoja ya kutuma vifungu kwa baadhi ya hoja, huku akijiuzuia kutumia katika hoja zingine?

Lakini pia tujiulize, iweje Rais wa ZNZ hakuhudhuria (tunasimama kusahihishwa) kuapishwa kwa Rais wa JMT katika msingi ule ule wa kutokuwa na ombwe, na kwamba Rais mwingine hajaapishwa?

Hii inaleta picha gani kimantiki, kisheria au kitaratibu?
Kwanini sheria zinatumika tukiwa 'wenyewe' wakiwepo ''wageni' tunasita kutumia sheria zile zile?

KAULI NI YA SERIKALI
Akiwa mshauri mkuuwa serikali, kauli yake ndio msimamo wa serikali.
Pengine serikali imekubali hoja za ZEC kufuta uchaguzi. Kama itakuwa ni hivyo, kauli ya mwanasheria itazua utata

Kwamba, Rais sasa itabidi azungumzie suala la ZNZ katika mtazamo wa mwanasheria mkuu ili kuepuka kuchanganyana

Tunadhani ipo diplomasia inayoendelea kuhusiana na mazungumzo ya ZNZ.
Hatujui ushiriki wa JMT katika hilo, tunachojua ni kuwa JMT ni mdau muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo.

Rais wa JMT ameelezwa kikatiba, hivyo ZNZ inaangukia katika eneo la utawala. Udau wa JMT ni wa asili, ni wa kikatiba
 
MSINGI WA HOJA SI RAIS WA ZNZ

NI HATMA YA WABUNGE WA ZNZ, NA MUSTAKABALI MZIMA WA MUUNGANO

Hoja ya mwanasheria mkuu wa JMT ni kuhusu uwepo wa Rais wa ZNZ ndani ya bunge
Huo si msingi wa hoja iliyotolewa na wapinzani.

Hoja iliyopo ni kutokuwepo kwa wabunge kutoka Baraza la wawakilishi

Wabunge hao watano wametajwa katika katiba ya 1977 kifungu kama kiungo cha mamlaka mbili

Wabunge wa ZNZ wanaoingia bunge la muungano hawana tatizo kwa uwepo au kutokuwepo kwao
Ni sawa na wabunge wa majimbo yaliyo ahirisha uchaguzi

Ukisoma katiba(nasimama kusahihishwa) haijawataja wabunge wa ZNZ bunge la muungano kwa upekee kama wa BLW

Wale 5 wana tatizo, kutokuwepo kwao kunaashiria kutoshiriki ZNZ kupitia wawakilishi wao ambao nao huchagua wabunge hao 5

Mwanasheria wa serikali alitakiwa aeleze kama hilo si tatizo.

Kutokuwepo na uwakilishi wa BLW, chombo kinachofanya na SMZ na mahakama kunadhoofisha muungano

Hilo litajenga hoja ya BLW kutoa maamuzi yao siku za mbeleni hata kama ni kukiuka katiba kama ilivyowahi kutokea

Ingalikuwa busara na vema kama mwanasheria angezingatia hoja za wapinzani.

Hoja za wapinzani haizkuta maelezo kuhusu uchaguzi wa ZNZ bali maelezo kuhusu hali ya baadaye ya Taifa

Ni hoja rahisi lakini yenye mantiki siku za mbeleni. Ni hoja itakayozua utata mwingine kwa jinsi inavyochukuliwa

Katiba ni mwongozo ulioandikwa kwa mtiririko na ufundi. Vifungu vyake vinajieleza na hufungamana.

Tatizo la katiba ni pale vifungu vinapochezewa au kufumbiwa macho.

Hilo linafungua nafasi ya ukiukwaji kadri muda unavyosonga mbele

Tusemezane
 
YAMETIMIA

MGOGORO WA ZNZ WATUA RASMI JMT

ILIKUWA SUALA LA MUDA TU


Mabandiko ya nyuma tuliasa sana kuhusu suala la ZNZ. Tulieleza, hilo ni tatizo la nchi na si ZNZ
Wakati utakapofika na busara zisipotumika, tatizo liatkuzwa kuliko lilipo kwa sasa

Tuliendelea kusema, katika mazingira yaliyopo, busara, sheria na kanuni zinatakiwa zitumike.
Kinyume chake, ubabe na maguvu yanaweza kutufikisha mahali pa gumu zaidi

Hayo ndiyo yaliyotokea leo. Rais wa ZNZ kazomewa akiingia bungeni.

Kuzomewa si tatizo, tatizo ni wabunge kumzomea kiongozi wa ngazi ile umma, ni jambo la kufikiria

Kwa mfano, hali ipo tete visiwani, na watu wapo katika tension kubwa.
Leo wanapoona wawakilishi wao wakizogoana wengine wakisema CCM na wengine Maalim Seif, hali mitaani ni tete

Kilichotokea ni ujumbe kwa makundi mawili.
Kwamba walioimba CCM walikuwa wanathibitisha kuwa Shein ndiye Rais

Huku mitaani inatafsiriwa kwa njia mbili
Kwamba, ndiye Rais wa ZNZ wa sasa au ndiye Rais wa ZNZ anayetakiwa

Pili, wale wanaoimba Maalimu Seifa nao wanatoa ujumbe
Kwamba, Maalimu ndiye alipaswa kuwepo pale au kukazia kuwa ndiye Rais

Hili linazidisha ufa, kwa wananchi wa kawaida tafsiri yoyote inaweza kutua vichwani mwao.
Tatizo ni wale wenye 'pre meditated thought' wanaweza kukosa ustahamilivu

Ndani ya bunge kulikuwa na viongozi waalikwa, nao wameona yaliyotokea.
Hii ni aibu kwa Taifa kwani wakichimba na tunajua wanajua, wataona zaidi walichojua kuhusu mtazamo wa wananchi

Picha iliyoonekana ni kugawanyika kwa Taifa. Hilo ni tatizo kubwa sana viongozi wetu hawalioni


Hotuba ya Rais

Katika jambo aliloongelea kwa undani ni kuimarisha muungano kwa kuulinda. Hapa alikuwa anapeleka ujumbe ulio na utata

Kwanza, kwamba, kila njia itatumika kulinda muungano.
Kwa kujua wapinzani ZNZ 'wanatuhumiwa' kutaka kuuvunja, ujumbe kutoka kwa Rais una utata mkubwa sana

Kwamba, muungano utalindwa , sasa haijulikani ni kwa njia zipi

Lakini pia una maana tofauti, kwamba yupo tayari kufanya kazi na wapinzani ilimradi kulinda muungano

Tutaendelea zaidi kuangalia hotuba kwa kina

Itaendelea....
 
Wanajamvi, Bandiko mbili hapo nyuma tulieleza kwanini Wapinzani wanahoji kuhusu bunge kuhutubiwa kukiwa hakuna wabunge kutoka Baraza la wawakilishi

Tumesoma habari inayoonekana chini tukabaki na maswali mengi. Tutaahirisha mazungumzo kuhusu hotuba ya Rais Bungeni na Tangazo la NEC kuhusu kusitisha shughuli za waangalizi

Tunafanya hivyo ili kuonyesha jinsi ambavyo kuna namna watu wanavyotaka umma uelewe ima kwa ukweli au upotoshaji
Soma habari hii kwanza halafu tutafanua. Tunaomba usome kwa bidi kile kifungu JUKATA inachosema kinampa Rais mamlaka ya kuhutubia bunge hata kama wabunge au wawakilishi hawapo kwa mujibu wa katiba ya 1977!!! Kwa mujibu wa katiba!


Kwa hisani ya gazeti la habari leo

Jukwa la Katiba wakunwa uteuzi wa Majaliwa

JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA) limepongeza uteuzi wa Waziri Mkuu uliofanywa na Rais John Magufuli kwa kumteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa.


Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema Rais amefanya uteuzi sahihi kwani waziri huyo ni miongoni mwa watu wasiokuwa na makandokando ya ufisadi na wala rushwa. Kibamba alisema wanaamini kuwa Majaliwa atasaidia katika kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa aliwahi kuwa mwalimu na kwamba anajua matatizo yanayowakabili wananchi.


??Haya ni mageuzi makubwa aliyoyaahidi kwa kuanza na kuunda kikosi cha miavuli kwa kuanzia na Waziri Mkuu makini na mchapakazi,?? alisema Kibamba akimzungumzia Majaliwa ambaye katika Serikali ya Awamu ya Nne, alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akishughulikia Elimu.


Aidha, Kibamba alisema suala la Rais kuhutubia Bunge pasipo kuwepo kwa wawakilishi kutoka Zanzibar, haliwezi kuwa kikwazo kwani Katiba ya mwaka 1977 inaweka wazi kwamba Rais anaweza kuhutubia Bunge hilo pasipo wabunge na wawakilishi wengine kuwepo.


Alisema Rais hawezi kuahirisha kuhutubia Bunge kutokana na majimbo machache kutofanya uchaguzi au wawakilishi kutokuwepo. Aidha, Jukata ilimuomba Rais Magufuli kumteua aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwakilisha wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

?Kwanza tunampongeza Mghwira kuwa ni mwanamke pekee ambaye aliendesha kampeni zake kwa hoja na sera bila ya kutumia lugha ya uchochezi, hivyo tunamuomba Rais amchague (kupitia nafasi zake 10) ili akawakilishe wananchi,?? alisema Kibamba.

Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, Jukwaa limemwomba Dk Magufuli kutangaza rasmi namna ya kurejea kwenye mchakato huo na kwamba atumie mamlaka yake kuonesha jinsi ya kutoka kwenye mkwamo huo.

Jukwaa hilo pia limemuomba Rais kuongoza jitihada za kuinusuru Zanzibar kwa kutambua kuwa hatua ya Umoja wa Serikali ya Kitaifa iliyokuwa imefikiwa na Wazanzibari inapaswa kulindwa na kuheshimiwa.
 
Wanajamvi, Bandiko mbili hapo nyuma tulieleza kwanini Wapinzani wanahoji kuhusu bunge kuhutubiwa kukiwa hakuna wabunge kutoka Baraza la wawakilishi

Tumesoma habari inayoonekana chini tukabaki na maswali mengi. Tutaahirisha mazungumzo kuhusu hotuba ya Rais Bungeni na Tangazo la NEC kuhusu kusitisha shughuli za waangalizi
Tunafanya hivyo ili kuonyesha jinsi ambavyo kuna namna watu wanavyotaka umma uelewe ima kwa ukweli au upotoshaji
Soma habari hii kwanza halafu tutafanua. Tunaomba usome kwa bidi kile kifungu JUKATA inachosema kinampa Rais mamlaka ya kuhutubia bunge hata kama wabunge au wawakilishi hawapo kwa mujibu wa katiba ya 1977!!! Kwa mujibu wa katiba!


Kwa hisani ya gazeti la habari leo

Jukwa la Katiba wakunwa uteuzi wa Majaliwa


JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA) limepongeza uteuzi wa Waziri Mkuu uliofanywa na Rais John Magufuli kwa kumteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa.


Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema Rais amefanya uteuzi sahihi kwani waziri huyo ni miongoni mwa watu wasiokuwa na makandokando ya ufisadi na wala rushwa. Kibamba alisema wanaamini kuwa Majaliwa atasaidia katika kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa aliwahi kuwa mwalimu na kwamba anajua matatizo yanayowakabili wananchi.


??Haya ni mageuzi makubwa aliyoyaahidi kwa kuanza na kuunda kikosi cha miavuli kwa kuanzia na Waziri Mkuu makini na mchapakazi,?? alisema Kibamba akimzungumzia Majaliwa ambaye katika Serikali ya Awamu ya Nne, alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akishughulikia Elimu.


Aidha, Kibamba alisema suala la Rais kuhutubia Bunge pasipo kuwepo kwa wawakilishi kutoka Zanzibar, haliwezi kuwa kikwazo kwani Katiba ya mwaka 1977 inaweka wazi kwamba Rais anaweza kuhutubia Bunge hilo pasipo wabunge na wawakilishi wengine kuwepo.


Alisema Rais hawezi kuahirisha kuhutubia Bunge kutokana na majimbo machache kutofanya uchaguzi au wawakilishi kutokuwepo. Aidha, Jukata ilimuomba Rais Magufuli kumteua aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwakilisha wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

?Kwanza tunampongeza Mghwira kuwa ni mwanamke pekee ambaye aliendesha kampeni zake kwa hoja na sera bila ya kutumia lugha ya uchochezi, hivyo tunamuomba Rais amchague (kupitia nafasi zake 10) ili akawakilishe wananchi,?? alisema Kibamba.

Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, Jukwaa limemwomba Dk Magufuli kutangaza rasmi namna ya kurejea kwenye mchakato huo na kwamba atumie mamlaka yake kuonesha jinsi ya kutoka kwenye mkwamo huo.

Jukwaa hilo pia limemuomba Rais kuongoza jitihada za kuinusuru Zanzibar kwa kutambua kuwa hatua ya Umoja wa Serikali ya Kitaifa iliyokuwa imefikiwa na Wazanzibari inapaswa kulindwa na kuheshimiwa.
...........
 

UFAFANUZI WA HOJA YA JUKATA
Tunaanza kuiangalia hoja ya JUKATA kwa kutazama aina yawabunge
Katiba 1977 inataja aina za wabunge
66.-(1) Bila yakuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge,yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanziaasilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d),itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwakatika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais,
watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwaBungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wauwakilishi baina ya vyama hivyo;
(c) Wabunge watanowaliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
(d) MwanasheriaMkuu;
(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutokamiongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifailiyotajwa katika ibara ya 67(1)(b)
UFAFANUZI: Wabunge waliochaguliwakuwakilisha majimbo ya uchaguzi kama ilivyp hapo juu 66(1)(a) ni hawa kutokabara na wale kutoka ZNZ wanaochaguliwa na wananchi
66(1)(c) Inataja makusudikabisa wabunge 5 kutoka baraza lawawakilishi
Kumbuka makundi mengine yaliyotajwa mahususi ni wanawake namwanasheria mkuu
Soma sehemu hii ya katiba ya 1977 tena
91.-(1) Rais atalihurubia Bunge Jipya katika Mkutano wake wa Kwanzana kulifungua rasmi Bunge hilo.
(2) Bila ya kuathirimasharti ya ibara ndogo ya (1); Rais aweza wakati wowote kulihutubia Bunge aukupeleka kwenye Bunge taarifa ambayo itasomwa na Waziri
Hadi hapa tunaona hakuna kifungu chochote cha katiba ya 1977kinachosema?Rais anaweza kuhutubia bunge bila wabunge au wawakilishi kamailivyodaiwa na JUKATA
Kifungu 91(1) Kinaeleza tu Rais kufungu bunge la kwanza.Hakuna maelezo mengine ya jinsi gani atahutubia na akidi au aina ya washiriki
JUKATA wamechakachua kifungu cha katiba ili kujenga hoja zao
Inaendelea..



 
=Nguruvi3;14670671]
JUKATA wametumia kifungu kifuatacho kujenga hoja yao ya Rais anaweza kuhutubia bila wabunge au wawakilishi kutoka BWL

Kifungu hiki ni kutokana na sheria Na 15 ya 1984 ya katibaya 1977

95. Bunge laweza kutekelezashughuli wakati wa vikao vyake bila ya kujali kwamba kuna kiti kilicho wazimiongoni mwa viti vya Wabunge (iwe kiti hicho kimekuwa wazi tangu Bungelilipokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au kimekuwa wazi baadaya Mkutano huo wa kwanza) na iwapo katika shughuli hizo atashiriki mtu yeyoteambaye hana haki ya kushiriki au kama wakati wa shughuli hizo atakuwapo mtuyeyote ambaye hana haki ya kuwapo, basi kushiriki kwa mtu huyo au kuwapo kwakehakutabatilisha shughuli hizo.

Hapa kinachoelezwa ni shughuli za Bunge na uwepo wazi waviti.

Kama JUKATA wanasema bunge lina haki ya kuendelea nashughuli, hiyo ina sawa.

Na kama JUKATA inasema uwepo wa Rais wa ZNZ ni sehemu yakifungu hiki, hilo ni sawa maana kifungu kinasema ..mtu yoyote ambaye hana haki ya kushiriki kuwapo, basi ushiriki wake wa mtu huyo au kuwepo kwakehakutabadilisha shughuli

Hivyo Shein anaweza kuwepo tu kama mgeni bila kuathiri taratibu, lakini anapotajwa kuwa ni Rais wa ZNZ na wala si Rais mstaafu, hilo linaturudisha katika kifungu 66(1)(c) kuwa wajumbe kutoka BLW walipaswa kuwepo

Kifungu hicho kimetoa uwakilishi maalumu uliopo kikatiba


Tunachojaribu kueleza hapa ni kuwa, kumezuka makundi ambayo

kwasababu zisizojulikana yanataka kupotosha umma.


Hakuna kifungu kinachosem Rais anaweza kuhutubia bunge la kwanza hata kama hakuna wabunge auwawakilishi katika katiba ya 1977 kama JUKATA wanavyosema

Hawa ndio Jukwaa la katiba! Tunatoa nafasi kwa mtu kutoka JUKATA kufika hapa tujadiliane

Miezi takribani miwili , Jukata(Kama kumbu kumbu zetu ziposahihi, na tunasimama kusahihishwa) waliomba Rais aweke msimamo juu ya katiba mpya kabla hajaondoka.

Tunapoweka yote katika kapu moja, tuna maswali ya kujiulizasana !

Tusemezane

Tutarudi hotuba ya Rais na kauli ya NEC
[/QUOTE]
 
ETI Rais wa Zanzibar hakuwepo siku ya kuapishwa Dr Magufuli.. Mzee wangu umekusudia au ulikosea..stori zako zinapoteza mulekeo..jaribu kuwa KATI sio kuchagua upande..yaani wewe ndio uwe sahihi wenzako wote hawako sahihi
 
Adharusi huwa sipendikukukujibu kwasababu siku zote huna hoja.
Unachotafuta ni mneno neno tu yasiyokuwa na maana.
Nashauri ujifnze kusoma, si herufi tu bali ni jinsi ganimaneno yamewekwa, yameelezwa, yamelindwa, yamefunguliwa, alama gani zimetumikan,k,
Siku zote huji na hoja bali personal attack popotenitakapoandika. Kule jukwaa la siasa umetukana uliogundua sikujibu ukaonaunifuate kwingine.
Hata siku moja sijasoma mahali ulipoandika kitu nikahisiumesaidia uelewa.
Ni kutafuta mabishano ya kipuuzi kwa hoja za kipuuzi
Hulazimishwi kusoma hapa, lakini ukisoma basi ukubali ziposababu na usome kwa uelewa ukitumia akili. Kusoma si kuimba, ni weledi na akiliukitafakari
Ungekuwa na ufahamu ungeshatambua kwanini huwa unakuwaigored.
Napata tabu sana kushiriki mjadala nawe na naomba unisaidiekwa hili
Nimefunga mjadala nawe, nawataka radihi wanajamvi kwausumbufu

 
HOTUBA YA MAGUFULI

NEC YAWAAMBIA WASIMAMIZI MUDA UMEKWISHA

Tumeona yaliyotokea Bungeni. Hapa duru tulisema si suala lasheria tu, bali busara zitumike

Busara zilizotumika ni kulazimisha waliolalamikiwa kama Rais wa ZNZ kuwemo Bungeni

Fedheha iliyotokea ni kubwa . Hakukuwepo ulazima katika mazingira tatanishi kama yaliyopo

'Uharibifu' si wa heshima ya viongozi tu, umeleta ‘hamasa'kwa wanaodhani haki haijatendwa.

Kwa maneno mengine Bunge/serikali zimefanya ‘promotion' yatatizo kwa kushindwa busara

HOTUBA YA RAIS

Imegusia kwa uchache ZNZ. Hoja kubwa ilikuwa kulinda muungano.
Viongozi wengi duniani huamini katika nguvu badala ya umma.

Urusi na mataifa mengine yalisambaratika licha ya kuwa na nguvu za kilinzi
UK walifanya kura ya maoni kuhusu Scotland ku pre empty umma kuja juu.

Kitendo hicho kimetuliza hali .Scotland inaendelea kuwa UK Washirika wakipewa fursa maamuzi kama Scotland

Ndivyo ilivyokuwa kwa Canda na Quebec. Kura ya maoni ilihitimisha kujitenga kwa Quebec.
Ingawa suala halijafikia mwisho, nguvu imepoteakuliko ilivyokuwa miaka 20 au 30 iliyopita


Marekani na Puerto Rico ilikuwa hivyo Na kwingine.

Si kuungana kuachanani njia mojawapo.Dunia ya leo kuachana kunahitaji fikra na suala zito

Muungano haulindwi kwa kauli au vitisho na maguvu. Utalindwa na umma wenyewe maridhiano.

Kauli ya Rais ilikuwa muafaka lakini ilitakiwa iwe ‘comprehensive'ikionyesha ushiriki wa wananchi.
Si suala la mtu bali watu kulinda muungano


MGOGORO WA ZNZ

Rais amesema amemtuma Makamu wa Rais kwenda kurafuta suluhu.
Ndivyo Rais aliyepita aliyetuma wakuu wa vyombo vya ulinzi kwenda kuongea na wanasiasa


Kinachoonekana ni wenye mamalaka kukaa mbali na tatizo.

Hatuelewi hili tatizo ni baina ya wagombea Urais au vyama.

Kama ni baina ya Wagombea, majadiliano yahusishe na upandewa tatu usiochukua sehemu

Kama ni miongoni mwa vyama, wenyeviti au wakuu wa vyama wasimamie mazungumzo hayo
Makamu wa Rais ni CCM,anayekwenda kusuluhisha ugomvi wa CCM na CUF!!!

Hatuelewi ni suluhu ipi inayotafutwa ikiwa vifungu vya sheria vipo na havitumiki

Iweje mambo ya kura yaamuliwe na vikao? Wapi haki za wananchi kuipitia sanduku la kura?

Wapi upande neutral unaosimama mazungumzo hayo?

Utamaduni wakuongea badala ya kura umeanza lini?

Ilikuwaje miaka ya nyuma maongezi yalifanyika baada ya matokeo?


Inandelea
 
TUME YA UCHAGUZI NEC
Tume imeeleza muda wa waangalizi kutoka nje umekwisha tarehe10 Novemba

Kama yupo anayehitaji aombe kibali kuangalia chaguzi nyingine Kauli imekuja siku 10 baada ya muda kwisha.

Katika hali ya kawaida, katazo hutolewa au kusisitizwa katika muda husika.


Imechukua siku 10 kwa NEC kufanya hivyo na tangazo hilo limegongana na Hotuba ya Rais

Tume ina haki ya kusema kwa muda wao. Hata hivyo, mtiririko na busara unazua hisia

Watu hutafuta namna ya kuunganisha matukio hata kwa kuungaunga.


Inapotokea kuungaunga huko kuna mantiki, manti husika hupewa nguvu kuliko dhamira ya kweli

Kwanini tamko limetokewa siku 10 baada ya muda kwisha ?


Tusemezane
 
MATUKIO YA KUFIKIRISHA BUNGENI

Tunaendelea kuangalia hali ya mambo kuanzia nyuma hadi siku bungelilipogeuka gulio
Busara hazikutumika, laiti zingetumika yasingejitokezatuliyo yaona.

Baraza la wawakilishi lilikataa makamu wa kwanzakuhudhuria kuvunjwa kwake.
Makamu wa kwanza wa Rais alikataliwa.


Si Rais wala makamuwa pili aliyeona tatizo.
Wote waliona ni la ‘maana' kwasababu liliwanufaisha kisiasa na kumdhalilisha mwenzao


Yaliyomkuta Rais waZNZ ndani ya bunge la JMT yanaeleza viwango tofauti vya busara ‘double standard'. Makamu wa kwanza hakuhudhuria BLW kwasababubusara zilitawala

Imeshangaza Rais wa ZNZ akihudhuria wakati busara zinasema haikuwa vema.

Spika wa BLW na Makamu wa pili wa Rais walihudhuria. Endapo walikuwa wageni wa bunge hakuna tatizo. Kama walikuwa wageni kwa nyadhifa zao lipo tatizo.

BLW limevunjwa, uspika wa BLW unapatikana kwa misingi gani?


Serikali ilishamaliza muda wake, Umakamu wa pili wa Rais unatoka wapi?

Haya ni mambo ya kupindisha ‘taratibu' yanaoonekana kutawala busara , hekima nasheria.


Tuangalie tukio la pili la bunge na ''conflict of interest''

Inaendelea..

 
Back
Top Bottom