Mitego ya Rais ya kununua Magoli iwakamate wajinga wa hili Taifa tu. Mimi siwezi kamatwa kamwe

Nyie mnaosema pesa cjui ijengewe hospital au shule .kwani kuna mwaka hivi vitu havijengwi?
Kila cku shule zinajengwa hospital nazo pia
 
Kama unajua jinsi ya kuinua anzia mtaani kwako tuone mfano .vinginevyo wacha pesa itumike
Nipeni hizo fedha muone. Zipo njia sahihi za kukuza michezo na si hizo, hebu niambie ununuzi wa hayo magoli unakuzaje michezo!? Nipeni hizo kodi niwaoneshe kwa mfano
 
Kumbe maneno yoote nkajua mzalendo kumbe izo ela naww unazitaka ?
Wenzako wanatoka jasho uwanjani ndio wanapata
Ebu weka number ya mpesa nkutumie nauli uje uchukue pesa nyingi sawa eeh
 
Kwa kweli ni ujinga wa hali ya juu kufurahia utapanyaji wa fedha kwenye starehe zisizo na tija wakati mambo muhimu kabisa, yanayohitaji sana pesa yashindwa kupata fedha.

Nina mfano unaoishi ambao sitausahau maishani, tuliwapeleka watu waliokuwa kwenye hali mbaya sana baada ya kupata ajali ya agari, na mmoja alifariki, lakini majeruhi wale baada ya kuwafikisha hospitali ya wilaya walikaa kwa masaa 7 bila ya huduma ya daktari kwa sababu hospitali nzima ina madaktari watatu tu walioajiriwa, na mmoja ni daktari mfawidhi, anashughulika zaidi na masuala ya utawala, mmoja yupo likizo, na aliyebakia azunguke wodini kuwahudumia wagonjwa wote. Tulipolalamika kwa huduma dhaifu, patron wa hospitali alitujibu kwa hasira kuwa, 'msitusumbue, hata mngekuwa ninyi msingeweza. Rais wenu anagawa hovyo pesa kwenye magoli lakini sisi hapa tumeandika barua za kuomba kuajiri madaktari na wauguzi mpaka tumechoka. Jibu kila mara ni kuwa Serikali haina pesa. LAKINI hela ya kununulia magoli na kusafiri na wasanii nje ya nchi ipo nyingi sana'. Tulipatwa na simanzi kubwa. Ikabidi tuliokuwepo pale hospitali tuchangishane pesa haraka ili majeruhi wale wakimbizwe hospitali ya rufaa. Maana tuliambiwa ambulance ipo ila hela ya mafuta hakuna, hela ya dereva na nurse hakuna.

Hapo ndipo ilipofikia nchi hii!! Mambo ya kijinga yanafanywa ni muhimu, na mambo ya muhimu yamepuuzwa kabisa. Inakera sana. Watawala wanatafuta sifa za kijinga kabisa!!
 
Kuna mipuuzi haina akili na elimu inashabikia huu upuuzi.
 
Sijui mantiki au logic ya kununua magoli ni ipi, ila ninacho jua kuna makumi kwa maelefu ya Watanzania wanataabika sana mtaani unaweza zania nchi haijapata uhuru, Raia wanaaugulia majumbani hawana pesa ya vipumo vya hospitali, ambako unakuta kipimo kimoja ni zaidi ya laki na mtu hana kwa sababu ya umasikini mkubwa sana na ambao walio sababisha ni hao hao wanao nunua Magoli ya Yanga na Simba.

Mpira wa miguu hasa haya mambo ya Yanga na Simmba yanatumika kisiasa kuhafaa wajinga wa hili Taifa, hadi too much.

Huwezu Raisi ukawa unanunua starehe ilihali raia wako wana hali mbaya sana mtaani, Raia wanatembeza fomu za michango ya kutibiwa Raisi anagawa bulungutu za pesa za Magoli na wajinga sisi tunashangilia kwa sababu tu wanao teseka watajijua wenyewe.

Ukiachana na Wagonjwa kuna shule kibao za Serikali yaani unaweza zania ni magofu ya kambi za maaskari wa vita ya Veitnam. Madarasa kama mabanda ya kufugia mbuzi na mkuu wa nchi anagawa pesa uwanjani

Magari ya Kubeba wagonjwa ni hadi raia ndugu jamaa na marafiki wajichange kumbuka gari ni STK na zimenunuluwa kwa kodi na stilli raia wanakamuliwa kwa kisingizio hakuna bajeti ya mafuta huku Raisi akinunua Magoli.

Nenda Police Gari za police unaambiwa hazina mafuta toa pesa ya mafuta mtuhumiwa wako akakamatwe yaani Raia ndio inabidi atoe pesa ya mafuta kuwezesha Police kwenda kukamata mtuhumiwa,Raisi ananunua Magoli ya Yanga na Simba.

Mimi ni Yanga na sisapoti huu ujinga na hakuna hata siku moja nitaingia kwenye huu mtego wa kutega wajinga wa hili Taifa kwa kununua Magoli ilihali Raia wanataabika sana mitaani.

Mitego hii ya kununua magoli iwakamate wajinga wa hili Taifa tu.
Washauri Watanzania wafanye kazi, Rais hawezi kupita majumbani akigawa pesa. Magufuli alisaidia baadhi ya watu akiwapa pesa mkachonga, oooh Rais anagawa pesa anazitoa wapi. Wacha tupate burudani ya maisha siyo kila siku tufikirie ujenzi tu, kuna maisha baada ya kazi na maisha yenyewe ndo kama hayo ya michezo.
 
Unazungumzia mashabiki tena kwani hizo hela zinagawiwa kwa mashabiki?
Kugawa hela kwa kwa simba na yanga inachangia nini kwenye soka la Bongo? Bora hizo hela angezitumia katika kufanya mambo ambayo yatasaidia kukuza soka au michezo kwa ujumla kuliko hivyo anavyofanya ambavyo ni kwa sababu za kisiasa zaidi.
Mkuu Simba na Yanga hazikwepeki ushawishi wake kwa namna yoyote ile.

Huko kwingine ambako unadhani pesa zingefaa kwenda zinakwenda na kufanya kazi. Hiyo ni motisha kwa hizo timu ili ziweze kushinda katika uwanja wa nyumbani, na ni njia ambayo imesaidia katika kuhakikisha uwanja wa Taifa hatoki mtu kutoka nje ya Tanzania.

Hawezi SSH kumridhisha kila mtu inabidi tu tuwe wapole.
 
Washauri Watanzania wafanye kazi, Rais hawezi kupita majumbani akigawa pesa. Magufuli alisaidia baadhi ya watu akiwapa pesa mkachonga, oooh Rais anagawa pesa anazitoa wapi. Wacha tupate burudani ya maisha siyo kila siku tufikirie ujenzi tu, kuna maisha baada ya kazi na maisha yenyewe ndo kama hayo ya michezo.
Watanzania wanapenda mno kulialia kama watoto wadogo, Hiyo pesa ni motisha ya ushindi kama hapendi mpira aanzishe tu mada nyingine za kisiasa wachangiaji tupo.
 
Mkuu unaongea kama hii nchi ni katika nchi zilizoendelea kumbe bado tunaangaika na mashimo ya vyoo.
Maendeleo ni mchakato wa miaka mingi mkuu Tz mbongo. Lakini haimnyimi Rais SSH kutumia kodi zetu katika kuwapa motisha Yanga na Simba. Asingefanya hivyo wangekuja na uzi mwingine wenye kulalamika kwamba hayupo karibu na michezo kwa ujumla.

Huwa hatuna dogo wabongo.
 
Mkuu Simba na Yanga hazikwepeki ushawishi wake kwa namna yoyote ile.

Huko kwingine ambako unadhani pesa zingefaa kwenda zinakwenda na kufanya kazi. Hiyo ni motisha kwa hizo timu ili ziweze kushinda katika uwanja wa nyumbani, na ni njia ambayo imesaidia katika kuhakikisha uwanja wa Taifa hatoki mtu kutoka nje ya Tanzania.

Hawezi SSH kumridhisha kila mtu inabidi tu tuwe wapole.
Kwanini asitumie hizo pesa kusaidia kukuza soka au michezo kiujumla kuliko kuzigawa kwa simba na yanga tu et ili kuwapa motisha? Ina maana akija Rais mwengine na akawa hatoi hizo pesa za motisha ndio itakuwaje?
 
Maendeleo ni mchakato wa miaka mingi mkuu Tz mbongo. Lakini haimnyimi Rais SSH kutumia kodi zetu katika kuwapa motisha Yanga na Simba. Asingefanya hivyo wangekuja na uzi mwingine wenye kulalamika kwamba hayupo karibu na michezo kwa ujumla.

Huwa hatuna dogo wabongo.
Wewe unaona motisha ya kugawa hizo hela kwa simba na yanga ni bora kuliko angefanya kitu kwenye soka letu ambacho kingebaki kuwa na manufaa na kukumbukwa hata akiondoka madarakani? Anachokifanya ni siasa tu na kwa mtazamo wako amefanikiwa kuonekana anajali hadi michezo.
 
Kwanini asitumie hizo pesa kusaidia kukuza soka au michezo kiujumla kuliko kuzigawa kwa simba na yanga tu et ili kuwapa motisha? Ina maana akija Rais mwengine na akawa hatoi hizo pesa za motisha ndio itakuwaje?
FIFA wanatuma Tanzania shilingi bilioni moja kila baada ya miaka miwili, unajua zinatumikaje hizo pesa?.

Akija Rais mwingine tutajua mbele ya safari ataamua kufanya vipi kuhusu michezo.

JPM alikuwa anagawa maburungutu ya pesa kwa wapita njia huko mitaani, ulishawahi kuhoji juu ya tabia yake hiyo kipindi kile akiwa bado yupo hai?.

Acheni nongwa za kitoto hizi.
 
Wewe unaona motisha ya kugawa hizo hela kwa simba na yanga ni bora kuliko angefanya kitu kwenye soka letu ambacho kingebaki kuwa na manufaa na kukumbukwa hata akiondoka madarakani? Anachokifanya ni siasa tu na kwa mtazamo wako amefanikiwa kuonekana anajali hadi michezo.
Pesa hizo milioni 20 ni kodi zetu, mimi na wewe ni pesa zetu hizi. Mimi sina pingamizi lolote na maamuzi ya serikali yake japo ninao mchango katika hizo pesa anazowapa Yanga na Simba.

Punguzeni akili za kitoto hizi, yapo masuala mengi muhimu yenye kuhitaji mjadala wa kina.
 
Kwa kweli ni ujinga wa hali ya juu kufurahia utapanyaji wa fedha kwenye starehe zisizo na tija wakati mambo muhimu kabisa, yanayohitaji sana pesa yashindwa kupata fedha.

Nina mfano unaoishi ambao sitausahau maishani, tuliwapeleka watu waliokuwa kwenye hali mbaya sana baada ya kupata ajali ya agari, na mmoja alifariki, lakini majeruhi wale baada ya kuwafikisha hospitali ya wilaya walikaa kwa masaa 7 bila ya huduma ya daktari kwa sababu hospitali nzima ina madaktari watatu tu walioajiriwa, na mmoja ni daktari mfawidhi, anashughulika zaidi na masuala ya utawala, mmoja yupo likizo, na aliyebakia azunguke wodini kuwahudumia wagonjwa wote. Tulipolalamika kwa huduma dhaifu, patron wa hospitali alitujibu kwa hasira kuwa, 'msitusumbue, hata mngekuwa ninyi msingeweza. Rais wenu anagawa hovyo pesa kwenye magoli lakini sisi hapa tumeandika barua za kuomba kuajiri madaktari na wauguzi mpaka tumechoka. Jibu kila mara ni kuwa Serikali haina pesa. LAKINI hela ya kununulia magoli na kusafiri na wasanii nje ya nchi ipo nyingi sana'. Tulipatwa na simanzi kubwa. Ikabidi tuliokuwepo pale hospitali tuchangishane pesa haraka ili majeruhi wale wakimbizwe hospitali ya rufaa. Maana tuliambiwa ambulance ipo ila hela ya mafuta hakuna, hela ya dereva na nurse hakuna.

Hapo ndipo ilipofikia nchi hii!! Mambo ya kijinga yanafanywa ni muhimu, na mambo ya muhimu yamepuuzwa kabisa. Inakera sana. Watawala wanatafuta sifa za kijinga kabisa!!
Hayo ni matatizo yenye kutakiwa kutatuliwa na waziri wa Afya, tunalipa kodi zetu na hatuoni dhambi yoyote kwa Rais kuwapa Yanga kama motisha ya ushindi.

Pia serikali inafanya shughuli nyingi mno na nyingi kati ya hizo hazijalala mpaka muda huu zinasonga mbele kama kawaida.

Michezo ni sekta mojawapo katika nyingi zinazoendeshwa kwa kodi zetu, kama nyinyi hamuipendi michezo tupo wengine tunazeeka na mahaba yetu ya Yanga na Simba.
 
Mkuu ni kutofautiana mitazamo tu wewe unona Rais kutoa pesa na kuzipeleka kwa wasio wahitaji kwamba ni jambo la furaha kwa wapenzi wa soka tu ila mwengine yeye kaona si sahihi Rais kutoa pesa badala ya kuzipeleka kwenye uhitaji tena wa msingi ambao utawafaa wananchi wote yeye anaenda kuzipeleka kusiko na uhitaji ili tu kuwafurahisha wapenzi wa mpira.
Huko kwa wahitaji mbalimbali peleka pendekezo kwa Waziri Ridhiwani Kikwete ndio mhusika mkuu, kwenye michezo kuna Mwana FA hawa ni mawaziri wawili wenye bajeti mbili tofauti.
 
Sijui mantiki au logic ya kununua magoli ni ipi, ila ninacho jua kuna makumi kwa maelefu ya Watanzania wanataabika sana mtaani unaweza zania nchi haijapata uhuru, Raia wanaaugulia majumbani hawana pesa ya vipumo vya hospitali, ambako unakuta kipimo kimoja ni zaidi ya laki na mtu hana kwa sababu ya umasikini mkubwa sana na ambao walio sababisha ni hao hao wanao nunua Magoli ya Yanga na Simba.

Mpira wa miguu hasa haya mambo ya Yanga na Simmba yanatumika kisiasa kuhafaa wajinga wa hili Taifa, hadi too much.

Huwezu Raisi ukawa unanunua starehe ilihali raia wako wana hali mbaya sana mtaani, Raia wanatembeza fomu za michango ya kutibiwa Raisi anagawa bulungutu za pesa za Magoli na wajinga sisi tunashangilia kwa sababu tu wanao teseka watajijua wenyewe.

Ukiachana na Wagonjwa kuna shule kibao za Serikali yaani unaweza zania ni magofu ya kambi za maaskari wa vita ya Veitnam. Madarasa kama mabanda ya kufugia mbuzi na mkuu wa nchi anagawa pesa uwanjani

Magari ya Kubeba wagonjwa ni hadi raia ndugu jamaa na marafiki wajichange kumbuka gari ni STK na zimenunuluwa kwa kodi na stilli raia wanakamuliwa kwa kisingizio hakuna bajeti ya mafuta huku Raisi akinunua Magoli.

Nenda Police Gari za police unaambiwa hazina mafuta toa pesa ya mafuta mtuhumiwa wako akakamatwe yaani Raia ndio inabidi atoe pesa ya mafuta kuwezesha Police kwenda kukamata mtuhumiwa,Raisi ananunua Magoli ya Yanga na Simba.

Mimi ni Yanga na sisapoti huu ujinga na hakuna hata siku moja nitaingia kwenye huu mtego wa kutega wajinga wa hili Taifa kwa kununua Magoli ilihali Raia wanataabika sana mitaani.

Mitego hii ya kununua magoli iwakamate wajinga wa hili Taifa tu.
Kwa magoli ya Samia kweli huwezi ila kwa upuuzi wa CHADEMA unanaswa kama mbwa na chatu
 
Kumbe maneno yoote nkajua mzalendo kumbe izo ela naww unazitaka ?
Wenzako wanatoka jasho uwanjani ndio wanapata
Ebu weka number ya mpesa nkutumie nauli uje uchukue pesa nyingi sawa eeh
Sawa Bosa
 
Back
Top Bottom