battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Allah ndio alikuja Kuweka wazi
Msome Allah na Yesu Allah anasema Kuna Mungu na Yesu anajitaja mwenyewe
Koran 57:3. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho,
Rev 22:12.“Sikiliza!” Asema Yesu..... 13Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.”
Koran 24:35. Mwenyezi Mungu ni Mwanga wa Mbingu na Ardhi....
John 8:12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu.
Koran 20:114. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki....
Itim 6:15 Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao uliopangwa na Mungu mwenye heri na aliye Mtawala pekee, Mfalme wa wafalme,
Koran 22:62. Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Wa Kweli,....
John 14: 6Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai.
102. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu...
John1: 3 Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
Koran 3:135.....na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu?........
Math 9:6Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.”....
Koran 22:69. Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu...
Math25:32 Mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
Koran 59:23. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, ....
Luke 4:34“Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”
Ndugu Mokiti
Naona unaruka ruka ,mara umeshika mada hii mara ile,Kwanini Humuamini yesu na mafundisho yake?