battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Nyongeza.Muhammad ukimsoma Wikipedia ni bonge moja la jamaa mstaarabu ila dini yake aliyoanzisha imekuwa na changamoto sana duniani baada ya kuweka mafundisho ya violence.
Kwasababu umetumia biblia tena kitabu cha Yohana, mimi nakupeleka sura ya kwanza:
1. Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
3. Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.
4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.
5. Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda.
14. Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utukufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba.
Mimi nilivyo mfahamu Yesu ni kuwa Katumwa na MUNGU awafundishe watu wapate kumjua MUNGU na wamtumikie Mungu.
Kazi hii Yesu Kaitimiza.
''Yoh.17; 8 kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma.
Hata Mimi naamini pia kuwa Yesu kweli alitumwa na MUNGU,
halikadhalika naamini Kuwa Muhammad naye Katumwa na MUNGU tena yule yule kwa ulimwengu.
Sasa hizi stori za Yohana hazikutoka kinywani mwa Yesu, na si sehemu ya Ujumbe wa Yesu. Bali ni Maono yake .
Yesu alisema
Mimi nawaambia maneno yatokayo kwa Baba aliye nituma hamuyaamini, lakini akija mwingine na maneno yake huyo mutamuamini.
Hili ndio tatizo lako wewe.
Naomba Zikanushe hizo kauli za Yesu kwanza kuwa ni Muongo? na yohana ndiye mkweli