Mitungi 100 ya gesi ya January Makamba kwa ufafanuzi wa Spika Tulia ilikuwa siri, Salma Kikwete karopoka bila kujua?

 
Yale mauchawi yenu ya kupumbaza Watanzania yanaendelea kumaliziwa na Mungu. Katika siku isiyokuwa na jina wa Tz watainuka!
Watainuka waende wapi kulima mahindi na maharage au kuinuka kivipi....mpo tu mnagonga hela za wanyonge za join the chain hamtaki kutoa hata hesabu🤣🤣 Mungu hataki utapeli
 
Takrima vs Rushwa. Only in TZ.
 
Huku wafanyakazi waliopo chin ya wizara yake wanaenda likizo hawalipi hii nchi ngumu sana,
Yaan mtu akishiba kumkumbuka mwenye njaa ni shida sana!
 
CCM isije ikarudia tena kilichofanyika 2020 kuingiza bungeni watu wenye akili ndogo. Kuna mbunge Babu Tale naye huwa anaongea utumbo mtupu. Mbunge Shigongo pia huwa haeleweki. Kuna siku kaleta hoja kwanini UDSM wamemnyima admission ya kusoma masters kisa hana cheti cha form four? Yaani ushuzi mtupu. Uchaguzi wa 2020 ulikuwa maumivu kwa wapinzani hadi CCM kwasababu kuna majina mengi sana ya wagombea yalikatwa kibabe na kuwekwa wasio na sifa.
 
Sio Takrima kweli hii?
ILitolewa kabla au baada ya bajeti ya wizara?
 
Hiyo mitungi 100 ni yakuanzia kamanda si sawa na kukosa kabisa
Huu ni ukatuni.
Yeye alisema umeme wa 27000 ni gharama ndogo, watu wanaweza kumudu 320000 hivyo irudi 320000. Alafu hapo hapo anaenda kutoa msaada wa mtungi wa sh 50000.
 
Bado hata hao ambao hawakupita hamna kitu,maana wengine ndio wameteuliwa ukuu wa wilaya. Mfano Babu tale mshindani wake alikua omary mgumba, huyu baada ya kukosa ubunge alipata uteuzi lakini baadae mama samia alimtengua na mlishangilia kwa kusema kweli hafai.

Wala tusitafute mchawi, hao waliopita ndio cream ya CCM. Ukitaka kutafuta nje ya hapo ni sawa na kwenda kutafuta bikra kwenye wodi ya wazazi
 
Hapana. CCM ina hazina ya watu wengi wenye uwezo kiuongozi. Tatizo linakuja kwenye kukata majina yakifika Dodoma kama ilivyokuwa 2020. Kumbuka Dr Slaa alikuwa mwanaCCM aliyeshinda kura za maoni wilaya ya Karatu ila jina lilivyoenda Dodoma likakatwa. Ni jambo lilitugharimu hadi leo. Upinzani ndo hauna watu kabisa wenye uwezo. Lema anayetukana Boda? Mdude Chadema?
 
Kwa hiyo Dr slaa angekuwa kiongozi ccm angefanya vizuri? Acha utani

Hao unaowaona kila baada ya miaka mitano karibu 25% huwa ni wapya toka miaka hiyo. Hakuna jipya, sijui unasubiri miujiza gani

Unasema CCM Ina hazina ya viongozi wazuri? Kwenye nafasi za uongozi CCM si wangeonekana, kaangalie makatibu wa CCM mkoa, wilaya, na kwingine alafu niambie kama kuna kiongozi mzuri hata mmoja.
 
Huko CHADEMA ndo kuna viongozi wazuri?
 
Huko CHADEMA ndo kuna viongozi wazuri?
Sipo chadema, Mimi nazungumzia ccm kwa kuwa ndio chama dola na tumekiona toka tunazaliwa hadi leo. Hivyo nakataa uongo eti waliokosa ubunge wapo vizuri kuliko waliopata
 
Sipo chadema, Mimi nazungumzia ccm kwa kuwa ndio chama dola na tumekiona toka tunazaliwa hadi leo. Hivyo nakataa uongo eti waliokosa ubunge wapo vizuri kuliko waliopata
Kuna sehemu nimesema waliokosa ubunge wote ni wazuri? Halafu mtu ambaye hana upande huwa daima ni MNAFIKI.
 

Kimsingi tuseme to Makamba aligawa rushwa ya 5,000,000 kwa kila mbunge maana siamini kama kuna aliyechukua hata mtungi moja. ( Mtungi Tzs.50,000*100)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…