Miujiza ya mafanikio ya Kiuchumi ya China yaliyowezeshwa na chama cha CPC

Miujiza ya mafanikio ya Kiuchumi ya China yaliyowezeshwa na chama cha CPC

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
gdfgdsg.jpg
Tarehe mosi Julai 2021, Chama cha Kikomunisti Cha China CPC kiliadhimisha miaka 100 tangu kianzishwe.

Katika hafla kubwa ya kuadhimisha karne moja, Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu wa Kamati Kuu ya CPC alitangaza kuwa China imetimiza lengo la kwanza la karne la kujenga jamii yenye ustawi wa wastani katika pande zote.

Kupitia kwa uongozi mahiri wa CPC, ndani ya miaka hiyo mia moja China sasa imekuwa nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, mpokeaji mkubwa wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, na moja ya soko kubwa zaidi la watumiaji duniani.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa Pato lake la taifa yaani GDP limezidi yuan trilioni 100- (sawa na dola za kimarekani trilioni 15.47).

Kwa watu waliozaliwa katika miaka ya 60 na wale waliozaliwa kwenye miaka ya 90 nchini China, wote wana hadithi tofauti kuhusu mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.


Waliozaliwa katika miaka ya 60 walishuhudia hali ngumu ya maisha na udhaifu wa Uchumi wa China, lakini ndani ya kizazi kimoja tu, yaani tangu kuanza kutekelezwa kwa sera ya mageuzi ya kiuchumi na kufungua milango mwaka 1978, China imebadilika na kuwa nchi yenye nguvu, na imefanikiwa kushughulikia changamoto kubwa, pamoja na kukidhi mahitaji ya kimsingi ya idadi kubwa ya watu wake.

Kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia, mwaka 1960 China ilikuwa maskini kuliko baadhi ya nchi barani Afrika. Kwa mfano mwaka 1960, mgao wa pato la kitaifa kwa China ulikuwa dola 89 tu, wakati DR. Congo ulikuwa dola 220, Kenya dola 97, Afrika Kusini 433 na Ghana 183. Lakini ilipofika mwaka 2017 mgao huo kwa China ulikuwa umefikia dola 8,827, huku Kenya ikiwa na dola 1,507, Ghana 1,641, Afrika Kusini 1,615.

Abbas Zaki, mwanachama wa kamati kuu ya chama cha Palestina cha Fatah anayesimamia uhusiano na China na nchi za Kiarabu, ametembelea China kwa zaidi ya mara 10 tangu safari ya kwanza mnamo 1974, alibaini kuwa katika kizazi kimoja tu, China imefanikiwa kuwaondoa watu wote kutoka kwa umaskini uliokithiri.

Anasema vijiji vilivyokuwa maskini vimebadilishwa na kuwa na tija, na maeneo mengi ambayo yalikuwa nyuma kimaendeleo sasa yamefurika viwanda.

Naye katibu mkuu wa Jumuiya ya muungano wa Urafiki wa Wabunge wa China na Japan yaani Sino-Japan Shoichi Kondo, anasema alienda kusomea China mwaka 1981 na sasa miaka 40 baadaye anaona China imekua kwa kasi ya kushangaza na kufanya miujiza chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China.

gfdsgtyreuyt.jpg

Muujiza wa Kiuchumi umefanikishwa na mipango kababe ya miaka mitano

Mpango wa maendeleo wa miaka mitano ni moja ya sababu kuu ya kufanikisha muujiza wa ukuaji wa kiuchumi wa China. Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Afrika na China katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, David Monyae anautaja mfumo huo kuwa wa kuaminika katika kuzingatia na kutabiri jinsi uchumi unavyokua na ni marekebisho gani muhimu ambayo yanahitajika kufanywa.

Tangu kuanzishwa kwake katika miaka ya 1950, kumekuwa na mipango 14 ya miaka mitano (FYP) – na kila moja inaashiria mabadiliko makubwa katika sera za uchumi za China na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Siku hizi mfumo huo wa China umekuwa sera inayofuatiliwa kwa karibu ulimwenguni kote kwani inatoa mwangaza wa sera za uchumi na malengo ya maendeleo ya China.

Mwaka huu, FYP ya 14 inayoishia 2025 imewekwa kwa kuzingatia kufikia malengo ya miaka mingine 100 ijayo ikiwemo kujenga nguvu ya kisasa ya ujamaa ifikapo 2049 wakati Jamhuri ya watu wa China itakapotimiza miaka 100.

Sera ya Ufunguzi
Nguzo nyingine muhimu kwenye uongozi wa CPC katika kufanikisha malengo yake ya kiuchumi ni kutekeleza sera za ufunguzi.
Mkutano wa tatu muhimu wa Kamati Kuu ya 11 ya CPC mnamo Desemba 1978 ulikuwa mwanzo wa safari ya kiuchumi ya China ya miaka 40 na zaidi ya mabadiliko na ufunguzi, na pia ulikuwa ni mwanzo mpya wa kazi za Chama ambazo ni ujenzi wa uchumi.

Sera ya kufungua milango kimsingi inamaanisha kukaribisha wawezekaji wa kigeni nchini China na ilitangazwa na kiongozi wa CPC wa wakati huo Deng Xiaoping. Matunda yake yameonekana ndani ya miaka 40 iliopita na mwaka 2020 China iliipiku Marekani na kuwa nchi inayovutia zaidi uwekezaji wa wa moja kwa moja wa kigeni.
 
Tunaiishia kujadili tu ila kuchukua hatua tunashindwa.China ni mfano bora wa kubaxili uchimi kws mda mfupi.
Zingine ni korea,Japan, Singapoor,Iran, Islaek, Brazil, Taiwan, Hong kong. Botswana,mouritious, Catar nk.
Usiweke wenye mafuta,unaharibu radha
 
Mi nlishawahi sema uwoga wetu ndio umaskini wetu.

Yaan bado tunakumbatia misaada na fadhila za wazungu tukijua ndio njiaa ya kutoboa.

Lakini uchumi wa nchi husika hujengwa na wananchi wake pekee na sikinginee.

Lakini sisi tumekosa njia za kujiongoza wenyewe tukitegemea misaada na fadhila ndo tukajenge bara bara....?

Sasa sijui siku mafuriko na vimbunga vikabomoa hiyo bara bara sijui ndo tutafanyaje....?

Any way pongezi kwa wachina walio amua kujitoa kimaso maso.

Mchina ni sawa na nzi ni nyuki alie amua kuwa serous na maisha yake.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Tunaiishia kujadili tu ila kuchukua hatua tunashindwa.China ni mfano bora wa kubaxili uchimi kws mda mfupi.
Zingine ni korea,Japan, Singapoor,Iran, Islaek, Brazil, Taiwan, Hong kong. Botswana,mouritious, Catar nk.
Fuatilia dhana ya ASIAN TIGERS uelewe zaidi. Pia suala la UONGOZI BORA utaelewa .
 
China walibahatika kumpata Rais mjanja aliyeitwa Deng Xiaoping. 100% ya yaliyofanyika na yatakayofanyika China ni Mipango ya huyo mzee. Marais wote wanafata Mipango ya huyo mzee.
 
Mwaka 1961 Tanganyika inapata uhuru uchumi wa Tanganyika na China ulikuwa unalingana Nyerere alifeli wapi?
Kama hayo ni kweli, mbona hatukwenda kuwajengea reli au kiwanda cha nguo kama wao walivyofanya kwa urafiki na tazara?
 
Bongo akipatikana huyo Deng Xiaoping watanzania watamchukia mara 100 ya walivyokuwa wanamchukia Magufuli[emoji28]
Tatizo wabongo wavivu sana, tunaongea sana vitendo kidogo. Kila kitu tunakosoa... Natamani tungepata rais mbabe zaidi ya alivyokuwa Uncle Magu angalau tungepiga hatua kidogo kiuchumi.
 
Tatizo wabongo wavivu sana, tunaongea sana vitendo kidogo. Kila kitu tunakosoa... Natamani tungepata rais mbabe zaidi ya alivyokuwa Uncle Magu angalau tungepiga hatua kidogo kiuchumi.
Wabongo tumezoea janja janja na shortcut za maisha! Wengi wamejikita kwenye rushwa na ufisadi tu maisha yaende..,Ukimtengenezea ugumu hapo tayari wewe ni adui namba moja😅 tegemea kutukanwa matusi yote!

Uchumi wa china umejengwa na uwajibikaji wa raia wote kwa usawa! Bila kulalamika japo iliwaumiza ila ndio ilikuwa namna pekee ya kufika walipo sasa na imewajengea spirit ya uwajibikaji vizazi kwa vizazi. Kiongozi mzembe anakula shaba tu. Raia mzembe kitanzi kinamuhusu hamna mambo ya kijinga!
 
Mwaka 1961 Tanganyika inapata uhuru uchumi wa Tanganyika na China ulikuwa unalingana Nyerere alifeli wapi?
Nyerere aliangushwa na Vita ya Kagera. Nchi ilitumia zaidi ya dola million 400 kwenye Vita hiyo.

Baada ya Vita Hali ya nchi ikawa mbaya sana.

Ila CCM ya kuanzia utawala Mwinyi tulidokezwa TU kuwa CCM haina dira wala uelekeo.

Alipoingia Mkapa ndipo tukaona dhamira ya dhati ya CCM ni kujaza matumbo na kuwaneemesha watu waliopo kwenye nafasi nono.

CCM ya Leo bado ni ileile ISIYO na dira, ambayo haijui inatupeleka wapi. Inasikitisha, miaka sitini ya Uhuru bado tunambwelambwela jangwani.

Narudia kuwaasa, CCM ndiye adui yetu mkubwa, yeye na ndugu yake KATIBA ya mwaka 1977
 
Bongo akipatikana huyo Deng Xiaoping watanzania watamchukia mara 100 ya walivyokuwa wanamchukia Magufuli😅
😂
Ila huyo mzee Deng na uongozi wake ndio umefanya China iwe hivyo, wanamuita The General Architect. Ndie aliyekuja na wazo la Special Economic Zones, Duty free zones, Muanzilishi wa Mabenki Makubwa China, Pia wachina wengi walipewa mikopo na mabenki kwa Dhamana ya CPC na roho yako. Yaani ukila hasara wanakuua. Hiki ndio chanzo cha utajiri wa ma tech giants wa china kama Jack Ma, Huawei, Xiaomi. Masuala ya kupiga hela ya ukandarasi. Kuvutia wawekezaji kwa kufuta kodi china. Huyu mzee ndie alilazimisha wachina wawe wanakopi utengenezaji wa vitu. Yaani huyu mzee ni Balaa. Mpaka wachina huwa wanaficha historia yake na vitabu vyake vya mipango ya uchumi vinafichwa na kulindwa ili watu wengine wasigeze. Huyu Deng alikuwa balaa na nusu.
 
😂
Ila huyo mzee Deng na uongozi wake ndio umefanya China iwe hivyo, wanamuita The General Architect. Ndie aliyekuja na wazo la Special Economic Zones, Duty free zones, Muanzilishi wa Mabenki Makubwa China, Pia wachina wengi walipewa mikopo na mabenki kwa Dhamana ya CPC na roho yako. Yaani ukila hasara wanakuua. Hiki ndio chanzo cha utajiri wa ma tech giants wa china kama Jack Ma, Huawei, Xiaomi. Masuala ya kupiga hela ya ukandarasi. Kuvutia wawekezaji kwa kufuta kodi china. Huyu mzee ndie alilazimisha wachina wawe wanakopi utengenezaji wa vitu. Yaani huyu mzee ni Balaa. Mpaka wachina huwa wanaficha historia yake na vitabu vyake vya mipango ya uchumi vinafichwa na kulindwa ili watu wengine wasigeze. Huyu Deng alikuwa balaa na nusu.

Mzee alidhamiria kuwapeleka uchumi wa juu kwa jasho na damu
 
Mzee alidhamiria kuwapeleka uchumi wa juu kwa jasho na damu
😂
Nawaza kama Deng angekuwa rais wa bongo yaani kibongobongo mtu upewe mkopo kwa dhamana ya roho yako. Najua hakuna kitu tungefanya zaidi ya starehe na kula misambwanda.
 
Back
Top Bottom