Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
- #81
Hakika mkuu...kama unataka aje asomee vyuo vyetu hapa nchini na aajiriwe hapa nchini...angalia uwezo wa mfuko wako unakuruhusu kumsomesha shule za aina gani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika mkuu...kama unataka aje asomee vyuo vyetu hapa nchini na aajiriwe hapa nchini...angalia uwezo wa mfuko wako unakuruhusu kumsomesha shule za aina gani.
Wengine wanaingia gharama kwa ajili ya fasheni tu,wekeza pale mfuko wako unapokuruhusu; kama unataka mwanao aje kuwa Director wa World bank pambania huko upande wa pili, mwanzo mpaka mwisho; na akasome mojawapo ya vyuo (top 10 ) vinavyotambulika huko duniani.Hakika mkuu...
Upo sahihi mkuu. Japo mtaala ni ule ule kuna tofauti kubwa sana.Shule ya msingi asome private. Ukiangalia syllabus za primary private zinacover secondary Kwa asilimia zaidi ya 70. Mtafute alie darasa la sita mpe paper za form 2, civics,geography, English, biology uone atakachotenda. Pia secondary hapambani kukariri, lugha anaijua hivyo masomo hayawi magumu sana kwake
Watoto wa namna hii wanakabiliwa na yafuatayo ambayo mwisho wa siku hujikuta wameumia :-Option nionazo ni mbili kwa upande wangu.
1.Mpeleke primary shule ya government Ila hakikisha unamsimamia kila nukta huku unawekeza ktk tuition, secondary mpeleke private maana ndo life linaanzia hapo.
2.Aanzie darasa la awali mpaka class 3 private Kisha mrudishe government aingie la4 mpaka la7.
Secondary mpeleke private.
Darasa la3 kwa shule nzuri ya English medium inatosha kabisa kwa mtoto kuwa vizur ktk lugha.
Kwa government tatzo la watoto wetu wanajisahau na mwisho wa siku wanaangukia pua hasa kidato Cha nne.
Na Kama ukimuanzisha primary ya private basi hata secondary ni private.
Nina ushahidi wa watoto wengi walokua private kwa primary Kisha wakafaulu government,ndani ya muda mfupi walipotea mazima.Nina wadogo zangu watatu walisoma private kwa primary na tena huyo mmoja alikua kipanga hasaaa na kufaulu shule kubwa ya government,Ila lastly alikuja kuumia.
Nafikir hakuna ufuatiliaji wa kimasomo na uangalizi ni mdogo Sana huku watoto wengi wakiwa hawana morali yakusoma.Labda advanced government ndo hua na spirit kubwa ya usomaji.
Umeandika kwa umakini na ufafanuzi wa kina sanaWatoto wa namna hii wanakabiliwa na yafuatayo ambayo mwisho wa siku hujikuta wameumia :-
1. Ni kipindi cha kupevuka (Adolescent stage) ambacho huambatana na mambo mengi hasa much know for everything. Mlezi ama mzazi usipomfuatilia mtoto kwa karibu hesabu umeumia no matter amesoma shule gani ya msingi.
2. Kubweteka wakati wa kidato cha kwanza na cha pili baada ya kuona wanafanya vizuri kwa sababu ya kujua lugha ya kufundishia kuliko wenzao waliotoka shule za serikali bila kujua baadhi ya wanafunzi waliotoka shule za serikali ni wazuri kuliko wao Ila lugha ndo tatizo. Wakijakuelewa kidogo tu kiingereza, huwapoteza hawa wa private mazima, then hawa wa waliotoka private schools hukata tamaa na kuharibu kabisa future zao.
3. Makundi. (Pear groups) Hapa mzazi/ mlezi kuna kazi ya ziada. Kuna magroup ya aina nyingi . Moja tu ndiyo salama la kujisomea, mengine ni majanga.
Wazazi / walezi jukumu la kuwafuatilia wanafunzi ni 50% na walimu 50%. Shirikianeni na walimu mjue tabia na mabadiliko ya watoto wanu ili muweze kuwarekebisha ipasavyo mapema. Kuwajengea msingi mzuri haijalishi km mtajitoa kwenye malezi. Wazazi/ Walezi peke yenu hamuwezi na walimu peke yao hawawezi. Students are very tricky nowadays when they get to know that parents are not Collaborating with their teachers.
Mfano mdogo tu wakati wa breakdown ya Corona, miezi 3 tu, wazazi / Walezi hawakuwa na hamu ya kuendelea kukaa na watoto wao kwa tabia na mienendo yao. Sasa tujiulize km hali ni hii, jukumu zito la malezi wanaachiwa walimu, je peke yao wanaweza ? Nao wanachangamoto zao lukuki !
Ni hayo tu.
Sawa kaka mkubwa yote kheri...Mimi nataka niende shamba na wanangu wanajua kusoma na kuandika Inatosha wanajua kutumia computer na other electronic devices inatosha
Asante nitakupa mrejesho hela kdg iliyobaki inatosha kununua MBUZI 200NA NGOMBE 50 NA KUKU 100 KIBANDA NILISHAJENGA WAKISHAJUA KUZISIMAMAIA mali zao HATA NIKIFI NITAKUWA SINA HOFU WANAWEZA JIENEDELEZA... mamilioni niliyoipoteza ili wajue kuandika na kusoma zinaniuma sanaSawa kaka mkubwa yote kheri...
Pole sana ndugu yangu...nimepoteza hela (5m×1×4)+(5×5)+(3m×2×11) ningeziweka kwenye architecture na mashamba ya miti na mifugo wanangu wangekuwa mabilionea by the age of 20yrs .....
Sawa kaka mkubwa...Brother peleka dogo katika shule za government kuanzia primary mpaka chuo kikuu
Ndio umeandika nini sasa hapa? Una hata mtoto kweli?Brother peleka dogo katika shule za government kuanzia primary mpaka chuo kikuu kingereza sio ishu kama dogo yupo vizuri, kwanza asikuambie mtu zipo shule za serikali nyingi ziko vizuri kuanzia walimu, mazingira, learning materials na watoto wanafanya vizuri achana na mambo za private brother fanya utafiti utaniambia mm kuna madogo wengi wanasoma shule za serikali wapo nondo kuliko wa private school. Labda kama unataka mwanao awe vizuri kwenye DEBATE za maoney is better than education.
Poa poa mkuu...kingereza sio ishu kama dogo yupo vizuri
Unaweza ukaweka vigezo/ushahidi ili kuendana na ulichoandika?Brother peleka dogo katika shule za government kuanzia primary mpaka chuo kikuu kingereza sio ishu kama dogo yupo vizuri, kwanza asikuambie mtu zipo shule za serikali nyingi ziko vizuri kuanzia walimu, mazingira, learning materials na watoto wanafanya vizuri achana na mambo za private brother fanya utafiti utaniambia mm kuna madogo wengi wanasoma shule za serikali wapo nondo kuliko wa private school. Labda kama unataka mwanao awe vizuri kwenye DEBATE za maoney is better than education.
Ushauri wa kibaba sana huuMkuu nashauri uwaanzishe private kwanza ili wajue kutumia lugha ya English, kiingereza ni lazima kwa kizazi kijacho, kwani tech inavyozidi kukua ndivyo English inavyozidi kutumika katika kila nyanja.
Pia ukitaka wanao wafike mbali zaidi lazima waijue English ipasavyo kwani ndio lugha ya dunia.
Secondary hakuna kigumu cha kukesha ukisoma isipokuwa lugha ni tatizo, jiulize kwanini private zifanye vizuri kuliko za kawaida.
shule za serikali ukielewa English utawaburuza mpaka basi,
kwani wenzako wanakalili lakini wewe unaelewa hivyo swali ukiliona na jibu lipo kichwani siyo yule aliyekalili.
Mababa ya form4 yalikuwa yananiogopa sababu ya English, peleka mtoto private.
Sawa kiongozi wangu...Mkuu nashauri uwaanzishe private kwanza ili wajue kutumia lugha ya English
Mkuu, hivi unajua CCM ndio baba lao?Mkuu nashauri uwaanzishe private kwanza ili wajue kutumia lugha ya English, kiingereza ni lazima kwa kizazi kijacho, kwani tech inavyozidi kukua ndivyo English inavyozidi kutumika katika kila nyanja.
Pia ukitaka wanao wafike mbali zaidi lazima waijue English ipasavyo kwani ndio lugha ya dunia.
Secondary hakuna kigumu cha kukesha ukisoma isipokuwa lugha ni tatizo, jiulize kwanini private zifanye vizuri kuliko za kawaida.
shule za serikali ukielewa English utawaburuza mpaka basi,
kwani wenzako wanakalili lakini wewe unaelewa hivyo swali ukiliona na jibu lipo kichwani siyo yule aliyekalili.
Mababa ya form4 yalikuwa yananiogopa sababu ya English, peleka mtoto private.
Wadau mpaka sasa nasikia CCM imeshachukua majimbo naneMtu mwenye kipato cha chini lengo lake ni mtoto afaulu ili aje kupata ajiri ya take home 470,000/= Kwa maana hiyo ni bora mtoto wake Primary asome government school akifaulu na kuchaguliwa shule mzuri aendelee na government school,akipata shule ya hovyo peleka private secondary school maana cheti cha form four ndiyo kila kitu kwenye mustakabali wa mtoto wake kielimu.
Kama mpunga upo somesha mtoto private kuanzia Primary mpaka University apate elimu bora ili aje kusimamia biashara zaka au aajiriwe kwenye International organization, government and private institute zenye kulipa mishahara mikubwa.