Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Hafai....muongo muongo sana naye hasa kwenye hili dubwana na Richmond mbona anapigapiga chenga tu..kama kweli yeye ni PM si apeleke goma hilo bungeni na aliweke wazi...In short Pinda hafai na hata U PM aliupata basi tu.....


Wewe unaonyesha una chuki binafsi. Huyu ndiye kiongozi muadilifu kuliko wote tulionao kwa sasa. Zaidi ya yote, ni msomi, ana confidence na ana uchungu na nchi yake. Tunataka viongozi wasio na tamaa ya utajiri bali wenye kiu ya maendeleo ya nchi yetu. Anafaa kuwa RAIS!
 
BILA SHAKA ANATUFAA JAPO KWAMIAKA MITANO TU. NAPENDA KUMKUMBUSHA TUMAIN KUWA RAIS MSTAAFU WA URUS AMBAYE SASA NI WAZIR MKUU YEYE HAJAWAH KUTUMIA COMPUTER WALA PIA KUPOKEA SIM YAN HANA SIM NA KAMA ATAKUMBUKA MWAKA FULAN ALIKUWA PERSON OF THE YEAR VIRADMIN PUTIN. NILAZIMA UJUWE UJANJA SIO KUWA NA SIM AU KUJUWA COMPUTER NILAZIMA UJUWE KUNA KAZ WATU HATA LAPTOP HAWARUHUSIW KUWA NAYO NILAZIMA UJUWE PINDA AME KUWA KATK IDARA ZA USALAMA KWA KIPINDI KIREFU HVYO ANAJUWA UBAYA WAKUTUMIA LAPTOP AU COMPUTER, WEL NAWEZA SEMA KAMA SISI WENYEWE HATUJAJUWA KUTENGENEZA LAPTOP AU COMPUTER HAIFAI VIONGOZ WETU KUZITUMIA MAANA USALAMA WA NCH NA MAL ZAKE UNAKUWA HATARIN NADHAN NISISEME SANA KTK HILI ILA NIKIWA KAMA MWANA HARAKAT NA MPIGANIA HAKI NA UHURU WA WATANZANIA NA MAL ZAO PINDA ANAFA KUWA RAIS AU MAGUFUL BILA SHAKA TAIFA LINGE PAA KIMAENDELEO. SHIME PINDA. God bless Tanzania and God bless Tanzanian. Thank u! Thank u.

No way to Pinda hatuhitaji mtu wa usalama wa taifa hapa watu wa aina hii ni hatari sana vilevile waoga wanajua wanachoapa.Tunataka mtu mwenye vision potential figure kama Mkapa anayeweza kusema kitu na kukisimamia kitekelezwe, Mkapa aliangushwa na kibri tu lakini alikuwa na vision nzuri, hadi sasa Pinda amefanya nini kwenye kilimo kwanza zaidi ya kuwapa tenda mafisadi tena walio na kesi mahakamani.

Vision ya Pinda iko focused zaidi kwenye ujamaa ambao umetushinda kwa hiyo ataturudisha kulekule kwenye ujima mtu kuwa na mali ni uhaini kuwa na TV laptop unaonekana wa maana watu wasivae suti kubana matumizi what nonsense idea is this, kama tukiamua kuirudisha CCM madarakani ni mara kumi ya EL awe presida kuliko Pinda.
 
Amechoka sana ukifika wakati huo, kiafya na kiakili

Besides uwezo wake ni mdogo kiakili na hata kiuchambuzi choka mbaya amesoma sheria hajui sheria, anabaki analia bungeni (anataka symphathy), swala makoti na matumizi ya serikali ..sentesi hizo tu zinaonyesha uwezo wake ni mdogo..therefore ni below standard

Hatuhitaji 2015 mtu ambaye computer hajawahi kutumia.

wakati mwingine waweza dhani una ufahamu kuliko wengine. huna tofauti na shabiki anayetazama mpira wa miguu na kuanza kukosoa uchezaji. kwako standard ni kumeza machungu na kuvaa tabasamu la mamba. kwa maoni yako, Obama ni below standars kwani alishalia hadharani. watu tusitumie hisia kutoa maamuzi, bali akili
 
Pinda abaki kuwa PM, Magufuli achukue nchi,tumeshachelewa sana,na mambo mengi yako ICU tunahitaji raisi atakae kuwa chachu ya maendeleo na kuiondoa nchi toka ICU
 
Makinda: Kitendo cha Pinda si cha ajabu

  • ASEMA HATA MKAPA NA SUMAYE WALITANGAZA MALI ZAO
Exuper Kachenje na Mahija Mpera

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda aliona kuna umuhimu kwa kiongozi wa serikali kutangaza mali zake na akafanya hivyo juzi, lakini naibu spika wa Bunge, Anna Makinda haoni kama kitendo hicho ni muhimu.

"Sikuona ajabu; sikuona kitu cha ajabu kabisa kwa yeye (Pinda) kufanya hivyo (kutangaza mali)," alisema Makinda baada ya kuulizwa na Mwananchi maoni yake kuhusu kitendo hicho cha Waziri Pinda.

Pinda, mmoja wa viongozi wanaoonekana kuwa ni wasafi, alitangaza mali zake juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari akisema kuwa ana nyumba za kawaida jijini Dar na Dodoma, gari moja la mkopo wa ubunge na akiba ya Sh25 milioni benki.

Lakini Makinda aliiambia Mwananchi jana kuwa hakuona kitu cha ajabu na kwamba kitendo cha Pinda hakimshtui kwa kuwa ni uamuzi wake.

"Are you serious (uko makini?); unataka nizungumzie hilo; Kwanza I don't know what's the point (sioni hapo hoja nini nini)," alisema Makinda.

"Kutangaza mali ni hiari ya mtu, wala sheria haiku-demand (haikulazimishi) kutangaza mali. Sikuona ajabu; sikuona kitu cha ajabu kabisa kwa yeye (Pinda) kufanya hivyo. Yeye ni waziri mkuu amependa kufanya hivyo Okay! (sawa)."

Alifafanua kuwa Pinda si wa kwanza kutangaza mali kwa kuwa kitendo kama hicho kiliwahi kufanywa na rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na waziri mkuu wake, Frederick Sumaye.

"Sio kitu cha ajabu kabisa, Mkapa aliwahi kutangaza mali hata Sumaye alifanya hivyo," alisema Makinda. Alipoulizwa iwapo ana mpango wa kufanya hivyo, Makinda ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini alisema: "Sheria hainilazimishi kufanya hivyo, hiyo ni hiari na wewe huwezi kuniambia nifanye hivyo kwa sababu utakuwa umenilazimisha."
 
Huyu mama amechoka kweli ndio wale wale wa miaka 40 bungeni kung'atuka hawataki mabadiliko hawataki kutangaza mali zao hawataki, yaani wizi mtupu
 
Re: Kauli ya Anna Makinda si ya kiungwana!



1. "Kutangaza mali ni hiari ya mtu, wala sheria haiku-demand (haikulazimishi) kutangaza mali. Sikuona ajabu; sikuona kitu cha ajabu kabisa kwa yeye (Pinda) kufanya hivyo. Yeye ni waziri mkuu amependa kufanya hivyo Okay! (sawa)."

2. Makinda ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini alisema: "Sheria hainilazimishi kufanya hivyo, hiyo ni hiari na wewe huwezi kuniambia nifanye hivyo kwa sababu utakuwa umenilazimisha."

- Mkuu mbona sijaelewa, eti hapa kwenye maneno ya Mama Makinda tatizo lipo wapi? Sijaona huo ukosefu wa uungwana uliousema au?

es!
 
Alichosema Anna kina maana na ndio tuanze kutafakari,je ni kweli sheria haiwalazimishi viongozi kutaja mali zao?na kama nimemuelewa Anna anaposema hata Mkapa na Sumaye nao walitangaza mali zao lakini hilo halikuwazui kukwiba na hawakuwajibika kutangaza mali zao wakati wanaondoka ,kwa hiyo hiyo sheria ni Ze Comedy wajameni,asante Anna kwa kutufungua macho ila sasa inabidi ung'atuke maana kuufanya ubunge ni ajira mbadala ni makosa inabidi mupumzike muweze kukaa na wajukuu zenu ili muwafunze maadili mema kwa kuwa tunakoelekea ubunge umeingiliwa na ufisadi wabunge wetu mmetugeuka
 
Anna Makinda hajakosea, pinda hajafanya jipya na sisi watanzania tunasubiri siku atakapoondoka ata-declare nini!!

Tatizo ni namna ambavyo kichwa cha ile habari kilivyoandikwa kwenye gazeti, imekaa kuwachonganisha kuliko kubeba maudhui ya ujumbe wa mama makinda
 
Mkapa alisema hivyo,baadae aliondoka na ufisadi wa hali ya juu.so pinda anaweza kusema hivyo ,tusubiri akiondoka madarakani
 
wakati mwingine waweza dhani una ufahamu kuliko wengine. huna tofauti na shabiki anayetazama mpira wa miguu na kuanza kukosoa uchezaji. kwako standard ni kumeza machungu na kuvaa tabasamu la mamba. kwa maoni yako, Obama ni below standars kwani alishalia hadharani. watu tusitumie hisia kutoa maamuzi, bali akili

Na wewe acha kulialia nimetumia akili, jibu hoja kwa hoja siyo ushabiki

Pinda ni below standard kwa vigezo vyote

Tangu awe PM kitu gani amefanya kinachoonekana zaidi ya "status quo" siyo creative, hakuna innovatios zozote, amebaki anaongelea habari za kuvaa suti, etc very boring..

He cannot will not command the higher office...very weak PM in our history.
 
Sasa kama sheria ipo lakini ni non binding kuna umuhimu gani wa kuwa na hiyo sheria? Ni kama vile mtu aseme kuna sheria ya "usiibe" lakini hainilazimishi kutoiba. Yaani hiyo sheria ilitungwa kufurahisha tu baraza?
 
Sasa kama sheria ipo lakini ni non binding kuna umuhimu gani wa kuwa na hiyo sheria? Ni kama vile mtu aseme kuna sheria ya "usiibe" lakini hainilazimishi kutoiba. Yaani hiyo sheria ilitungwa kufurahisha tu baraza?

Halafu nani aliyetunga sheria hiyo?
 
mpaka sasa hivi siamini kuwa hata % kubwa yp JF wanakubali kuwa Pinda ana gari moja. its imposible ina maana pinda ni mzembe kiasi hicho? sio mjasiriamali? huyu ataiba au ni mwizi.
 
Anna kapungukiwa na uadilifu kujaribu kumuunganisha Pinda na kina mkapa ambao imethibitika kujilimbikizia mali chafu. Sasa kwa pinda haijawa hivyo kwani kudhani ni kumhukumu prime minister isivyostahili. Nasi tunaweza kumhukumu Anna kwa dhana kwamba kitendo cha Pinda kinamhukumu hatia maana yeye ni fisadi na anaogopa kujulikana na umma ikiwa atataja mali zake.
 
Back
Top Bottom