Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Maafisa mikopo wamezoea kupewa rushwa ili kutowa mikopo fasta na ndio maana mikopo yao hailipiki nyumba zinapigwa mnada.Equity tawi la Dodoma nimeomba kimkopo kidogo tu m10 zaidi ya miezi 3 sasa wako kimya.
Documents muhimu zoote nime provide...hii nayo ni bank kweli?!.
We hebu acha kuwasumbua watu, hebu nenda benki kakope hela ufanye kazi.....masharti nafuu yapi unataka, sharti ni kukopa hela na kurejesha kila mwisho wa mwezi basi.....Nimeuliza kwa 10-100M ipi ina masharti nafuu, na 100M-500M ,Aina ya mkopo ni mkopo wa biashara kuongeza asset (asset financing)
Mkuu hujalazimishwa kuchangia uzi huu Kama hauna cha kusema pita kimyakimya. AhsanteWe hebu acha kuwasumbua watu, hebu nenda benki kakope hela ufanye kazi.....masharti nafuu yapi unataka, sharti ni kukopa hela na kurejesha kila mwisho wa mwezi basi.....
Hilo endelea nalo utapata majibu.. Nilikuwa naweka maoni.. Kuna mmoja alisema mikopo ni kutafuta kufilisikaHii inajulikana, swali langu umesoma lakini? Nauliza benki ipi nzuri (masharti nafuu) kwa mikopo ya 15-100M na 100-500M
Hapa lazima uende benki husika ... Range ya mkopo ni kubwa sana .. Mikopo kama 15 - 30 milioni, inashughulikiwa kwa urahisi na saccos na vikoba..... Masharti ya benki kukopa inategemea , unakopa kama mfanyabiashara au mfanyakazi watakuwa na masharti yao. Ambayo si rahisi kuyaweka hapa... Benki zote za biashara zinaweza kutoa mkopo huo.. Swala ni wewe , una qualify vipi, track record yako ya kipesa na unataka kukopa kwa kitu gani, kilimo, biashara mbalimbali.. Ukipitia benki mojamoja utapata picha.... Experience ya mtu mmoja wa hapa jukwani sidhani ni kipimo sahihiHii inajulikana, swali langu umesoma lakini? Nauliza benki ipi nzuri (masharti nafuu) kwa mikopo ya 15-100M na 100-500M
Kabla hatujaenda huko benki tunataka kusikia testimonials? Kuna mtu amekopa sehemu na hatamani kurudi akishare hapa tunajifunza au nimekosea wapi ndugu?Hapa lazima uende benki husika ... Range ya mkopo ni kubwa sana .. Mikopo kama 15 - 30 milioni, inashughulikiwa kwa urahisi na saccos na vikoba..... Masharti ya benki kukopa inategemea , unakopa kama mfanyabiashara au mfanyakazi watakuwa na masharti yao. Ambayo si rahisi kuyaweka hapa... Benki zote za biashara zinaweza kutoa mkopo huo.. Swala ni wewe , una qualify vipi, track record yako ya kipesa na unataka kukopa kwa kitu gani, kilimo, biashara mbalimbali.. Ukipitia benki mojamoja utapata picha.... Experience ya mtu mmoja wa hapa jukwani sidhani ni kipimo sahihi
Mbaya zaidi unawakopa bank halafu ukifault mkopo unakuja kudaiwa deni na vibaka wengine kampuni za udalali utakoma ubishi.Unakwenda kukopa na kununua matatizo!
Uwe tayari kupima suksri, pressure na hutakaa kuwa na amani huki nyumbani kwako
Humu kila mtu mjuaji mkuu! Utasikia anajitapa kwamba hawezi kukopa swali ni je atafika utajiri kwa kudunduliza?Yaani hivi vi take home ndio tuvitegemee kujenga, kuwekeza, kusomesha nk? Mikopo haikwepeki, muhimu ni kufanyia kazi kile ulichokusuda kabla ya kuingia hiyo mikopo.
Hongera, mkuu uko kwenye biashara au ajira? hao ABSA masharti yao yapojeSuala la mikopo lipo subjective kwa sababu kila mtu ana elimu na uzoefu wake na kwa kuongezea ni kuwa benki kama ABSA inakopesha vizuri as long as umecomply vizuri. Hizi benki kubwa kama CRDB, NMB, NBC nazo nipo vizuri ila tatizo ni kwamba zinazidiwa na demand ya huduma na wateja. Nimewahi kwenda kufanya application ya mkopo mdogo tu wa 36m ila process ya masaa 24 ilichukua zaidi ya wiki 3 mpaka pesa inasoma kwenye account.
haya subiria hizo testimony...Kabla hatujaenda huko benki tunataka kusikia testimonials? Kuna mtu amekopa sehemu na hatamani kurudi akishare hapa tunajifunza au nimekosea wapi ndugu?
Asante mkuu, nipo kwenye biashara full-time. Huko ABSA mashaeti yao kwa biashara ni lazima uwe na collateral, documents zote ziwe sawa na pia mkopo uwe ni wa kuendeleza biashara. Nilichopenda kwa hiyo benki ni kwamba hakuna adha ya mafoleni na pia customer service ipo vizuri. Isingekuwa mkopo wa awali nigekuwa na akaunti huko.Hongera, mkuu uko kwenye biashara au ajira? hao ABSA masharti yao yapoje