Mjadala: Benki nzuri kwa mikopo ya wafanyabiashara (15m-500m)

Mjadala: Benki nzuri kwa mikopo ya wafanyabiashara (15m-500m)

Masikini ni mentality!! You become what you think!!
Mfano una biashara inakuingizia faida ya 4M kwa mwezi kwa mwaka ni 48M
Unahitaji kupanua wigo wa biashara, kwanini usifanye Hivyo? Au unataka asset mpya? Au umepata tender kubwa?
Nimekupa challenge nitajie Tajiri unayemfahamu ambaye hajawahi kukopa, MMOJA TU
aisee we ni kiazi...tajiri unayemuona amekopa ni hao unaowafamamu wewe na kunatrick watu hufanya kuonyesha wanamikopo kupunguza ukubwa wa kodi....tajiri unayemuona kakopa itakuwa amepata kandarasi kubwa kuliko uwezo wa mtaji wake hivyo ni kama anahamisha fedha abakie na fedha zaidi...wewe mtaji na mzunguko wako ni milioni 20 kwa mwaka...unakwenda kukopa m30 unafungwa mota urejeshe fedha na riba juu baada ya miaka miwili au mitatu unakuta ushapotea kabisa....watu hukopa pale anapozidiwa na wateja yaani demand imezidi supply yake anakwenda kuboost supply kwafedha zilizowekwa benk na wasio na mishe zao ennki wanachukua chao na yeye anabaki na chake...sasa wewe unapambana kupata wateja supply ipo chiini demand ipo chhini unaenda kukopa utakunya mavi ya blue...unashindwa kulipa ada unakwenda kukopa biashara ngumu unakwenda kukopa...watu wanakopa kuanzisha project ambazo demand ipo wazi yaani baada ya kukamilisha anapata fedha ya kurejesha na kubaki na faida...sio tena anaanza kukuza biashara ama nini...
 
HAKUNA TAJIRI ASIYEKOPA! Umewahi kuwasikia watu wakisema hawakopi au kujisifia kwamba hawakopi kwenye biashara zao? Ukweli ni kwamba matajiri wote unaowajua wanakopa, ELON MUSK, alikopa kuinunua Twitter (sasa X), Mohammed Dewji MO alikopa benki ya First Rand Afrika kusini. Sasa Kama Elon Musk anakopa itakuwa wewe George wa Uyole? Mikopo ni ushahidi kwamba unaaminika na taasisi Kama Benki.

Je ni Benki ipi, (mtushauri kwa uzoefu) ina masharti nafuu ya mikopo. Kati ya Benki hizi za Tanzania kubwa (NBC, CRDB, NMB) au ndogo (MKOMBOZI, MAENDELEO, AKIBA, AZANIA, DCB, AMANA)au za kimataifa (EQUITY, KCB, ABSA, NCBA, STANBIC, STANDARD CHARTERED, EXIM, BOA, DTB,) ipi ina masharti nafuu kwa wafanyabiashara wanaokopa kiwango cha 15M -500M .

Benki nyingi hazina shida kutoa mikopo ya wafanyakazi hasa wa Serikali! Lakini kwenye wafanyabiashara sarakasi zinakuwa nyingi utasikia lete "audited financial reports " za miaka mitatu iliyopita.

TOFAUTI ya matajiri na wafanyabiashara wa kawaida wao wanaaminika hivyo wanapewa mikopo nafuu, yenye masharti nafuu. Wewe ukienda kukopa jiandae riba ya 20% na hati ya nyumba mkononi 😂,bado hongo za hapa na pale kwa maafisa wa benki.

Kwenye benki tajwa hapo juu, ni ipi inawasaidia Sana wafanyabiashara wa kati na wadogo SMEs kukua? Hapa tuongelee mikopo ya 10M-500M

Natamani kusikia testimonials, kuhusu mtu aliyekuwa anakopa 10M na amepanda hadi 100M

Karibuni mshauri ,kwa mliokopa ni challenge zipi mlikutana nazo kwenye marejesho?
Swali zuri ila naona hapa si pahala pake. Muone kama Covax anabwabwaja tu
 
Biashara zenye audited financial report ni 2% ya biashara zote Tanzania, na tayari ni kubwa hata kulipa mkopo sio issue kwao, ila nyingi zinazo hitaji mkopo ni informal hazina documents za biashara zaidi ya leseni tu.
Mkuu watu wanapenda kukopa hawajui mlolongo wa payment ,unatakiwa kabla hujasaini omba mpangilio wa malipo na ujue hadi mwisho unalipa shiling ngapi iterms of interest . Kuhusu hizo za informal bank hasa za hapa zinahuduma ya vikundi wanaweza kopa, tatizo watu sio waaminifu kulipa hiyo ni characters za watu.
 
Biashara ya pharmacy ni kuuza dawa, unaamini anaweza kujenga hotel au kuna dawa za kulevya pia.

Elewa hapa duniani kuna biashara za watu ni cover tu kuhaada watu source of income yake lakini income yake halisi siyo hiyo unayoiona wewe kwa macho.

Hata Rummy naye alikuwa anazuga na Pharmacy kumbe alikuwa anauza "BWIMBWI".
 
aisee we ni kiazi...tajiri unayemuona amekopa ni hao unaowafamamu wewe na kunatrick watu hufanya kuonyesha wanamikopo kupunguza ukubwa wa kodi....tajiri unayemuona kakopa itakuwa amepata kandarasi kubwa kuliko uwezo wa mtaji wake hivyo ni kama anahamisha fedha abakie na fedha zaidi...wewe mtaji na mzunguko wako ni milioni 20 kwa mwaka...unakwenda kukopa m30 unafungwa mota urejeshe fedha na riba juu baada ya miaka miwili au mitatu unakuta ushapotea kabisa....watu hukopa pale anapozidiwa na wateja yaani demand imezidi supply yake anakwenda kuboost supply kwafedha zilizowekwa benk na wasio na mishe zao ennki wanachukua chao na yeye anabaki na chake...sasa wewe unapambana kupata wateja supply ipo chiini demand ipo chhini unaenda kukopa utakunya mavi ya blue...unashindwa kulipa ada unakwenda kukopa biashara ngumu unakwenda kukopa...watu wanakopa kuanzisha project ambazo demand ipo wazi yaani baada ya kukamilisha anapata fedha ya kurejesha na kubaki na faida...sio tena anaanza kukuza biashara ama nini...
Hapa umeandika vizuri kabisa, hapo kwenye kuangalia mzunguko wako kuna kitu wanaita debt to income ratio yaani kiwango cha Deni unagawa kwa kipato chako cha mwezi (rejesho unagawa kwa mapato ya mwezi)
 
Jumamosi niliona kipindi kimoja StarTV, walikuwa wanamuhoji mwanafamilia/ afisa wa GSM kama ni vyema kuchukua mkopo au la.. Alichojibu kama mkopo ni kwa ajili ya kuendeleza biashara hilo ni jambo jema..Lakini kama mkopo ni kwa ajili ya matumizi ya maisha hilo si jambo jema.. Nafikiri hii ni loud and clear
 
Ashakum si matusi hakuwa mke ni gumalaya gwa mjini ambaye nilidhani nitaoa kumbe alifuata kibunda .
Nilikopa ili aanzishe biashara ya vipodozi duka kuuuubwa Kama naliona ,Ila ikawa vile akaolewa huko Tabora na jamaa mmoja muuza asali ,.Kuhusu makato ni Siri yangu maana nikisema hapa mtanicheka mbwembwe zangu za hapa na kamshahara ninakopokea hakaendani na hadhi yangu ,hivyo kwenye suala la makato naomba miwe nje ya box .
Ahsante dada umeniumiza moyo sana
Unapiga ulanzi Tu hapo Mzee wangu😂 kummake Malaya
 
Jumamosi niliona kipindi kimoja StarTV, walikuwa wanamuhoji mwanafamilia/ afisa wa GSM kama ni vyema kuchukua mkopo au la.. Alichojibu kama mkopo ni kwa ajili ya kuendeleza biashara hilo ni jambo jema..Lakini kama mkopo ni kwa ajili ya matumizi ya maisha hilo si jambo jema.. Nafikiri hii ni loud and clear
Hii inajulikana, swali langu umesoma lakini? Nauliza benki ipi nzuri (masharti nafuu) kwa mikopo ya 15-100M na 100-500M
 
Back
Top Bottom