Mtandao wa Youtube unajulikana kuwalipa watu kutokana na views za video zao. Kitu kigumu kwa wanao-upload video zao pale youtube ni kujua kama zitapata views za kutosha.
Ni kweli kuwa unaweza kulipa watu wawe wanafungua video yako mara nyingi ili kuongeza views, na vile vile kuna robots za kutumika kufungua video yako hata kama haingaliwi lakini hizi hukwama mara nyingi kutokana na security ya youtube. Sasa swali linarudi pale pale, kuwa ni nini kinachotakiwa kwa video kutazamwa sana. Jibu lake lina sehemu tatu:
(1) Sehemu ya kwanza ni maudhui ya video yenyewe. Video za Muziki ndizo hufunguliwa sana kwa sababu ni fupi, halafu binadamu wote hupenda muziki.
(2) Sehemu ya pili ni wigo wake ( yaani reach). Video inayofikia watu wenye background mbalimbali hupata views nyingi sana kuliko video inayofikia watu wa aina fulani tu.
(3) Sehemu ya tatu, ambayo inaweza kuwa na uhusiano wa karibu na hiyo sehemu ya pili hapo juu ni kuhusu umaarufu wa mtoa video na promotion ya video yenyewe. Mtu anayetoa video akiwa mtu maarufu mwenye wafuasi wengi akitangaza kuwa ametoa video yake, basi wafuasi wake karibu wote watakuwa wa kwanza kuiangalia hata kama ni mbaya. Sasa iwapo mtu huyo ana wafuasi milioni 20, ni wazi kuwa video hiyo inaweza kupata views milioni kumi kwa siku moja tu hata kama siyo nzuri.
Nimejaribu kuangalia kwa makini hizi video tatu ambazo zina views bilioni tatu na zaidi nikashindwa kabisa kujua ni vigezo gani vilivyotumika kuvuta watazamaji namna hiyo zaidi ya content ya muziki wenyewe.
Video ya kwanza
Video hii ina zaidi ya views 3.4 billions katika muda wa miezi sita tu. Video hii imepigiwa mitaani kwa kawaida tu, ila ina muzuki mzito sana ambao nadhani ndio unaovuta watazamaji. Ni kweli kuwa inapata advantage kubwa sana ya kupendwa na watu wote wanaouzungumza spanish lakini nadhani content ya muziki wake ndiyo inayovuta watazamaji. Hakuna cha mavazi au video effects hapo.
Video ya pili
Video hii ina zaidi ya views 3.0 billions katika miwili iliyopita. Video hii ina muziki wa nguvu sana ambao nadhani ndio unaovutia watazamaji kuliko hata majina ya waimbaji wenyewe. Kibaya ni kuwa Muziki huo unajitokeza kwa muda mfupi sana na kutoweka, kwa hiyo mtazamaji anajikuta akirudia rudia. Characters wote katika muziki huu wamevaa mavazi ya kawaida tu kama ilivyo kwenye mitaa ya miji mbalimbali ya Marekani na wala muziki haukutumia video effects zozote.
Video ya tatu ni
Video hii ina karibu ya views 3.0 billions katika miaka mitano iliyopita. Huyu jamaa Psy hakuwa anajulikana kabisa duniani kabla ya kutoa video hiyo, lakini video yake ilikuwa maarufu sana duniani kote. Amevaa na kutumia mazingira ya kawaida ya jijini Seol na hata video effects alizotumia ni minimal sana. Utaona kuwa hapa kilichovuta watazamaji ni creativity zake katika mziki wenyewe na katika uchezaji wake.
Outlook hiyo fupi inaonyesha kuwa video za muziki hazivuti watazamaji kwa sababu ya video effects au mavazi ya characters bali uzito wa muziki ulio embedded kwenye video zenyewe. Music producers wa kitanzania wanatakiwa kufanya kazi za ziada kupaisha video za wanamuziki wetu kuliko kutumia njia za mkatomkato kama inavoendelea sasa