MJADALA: Je, ni kwa namna gani YouTube humlipa mmiliki wa account?

MJADALA: Je, ni kwa namna gani YouTube humlipa mmiliki wa account?

Umeeleweka ila ungewagusia waliokufanya kuandika uzi huu..!!
Nilianzisha uzi huu baada ya kusoma article fulani kwenye mojawapo ya magazeti yaliyoko online. Mwandishi alikuwa akipima mavazi na video effects za wimbo mmoja dhidi ya wimbo mwingine na ku-conclude kuwa wimbo mzuri unahitaji investment kubwa katika video kwa kuwekeza katika mavazi na video effects ili kuvutia watazamaji. VYote hayo hayakuingia akilini mwangu kwa kuangalia video hizo tatu za juu sana hapo Youtube.
 
7c6159539d44b92a23c4b64e65aa3113.jpg


Angalia hapo palipozungushiwa duara jekundu, hiyo ndiyo hali halisi ambapo views wa halali
Hata mimi nimekiona hii kitu huko you tube sasa sijajua ina maana gani hasa
 
Kwa video namba mbili:sababu ya kuwa na views nyingi ni ukiachilia nyimbo ni Kali ila sababu nyingine ni baada ya kifo cha muigizaji Paul walker ambae alifariki ghafla kwa ajali ya gari wakati yuko kwenye "peak" na muendelezo wa movie yao ya fast n furious ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kweli...na hiyo nyimbo ilitumika kama soundtrack ya hiyo movie.

Video namba 3:ni kwamba huyo mjamaa anatokea China kama ameweza kupenya Europe,America na hata huku Africa kwa ngoma yake ya gangman style...huko kwao ndo habari ya mjini...population ya China tu ni kama bara zima la Africa..wachina wenzake walichangia kwa kiasi kikubwa kumpa views nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati nakumbuka methali isemayo "ukipenda chongo uita kengeza"

Jiulize mara mbili mbili mtu kukaa mwaka mzima na kuja kuibuka na SEDUCE ME imekidhi haja yako ya kumsubiria king mwaka mzima?

Jiulize maudhui ya hiyo nyimbo, mashairi yake n.k n.k

Je umevutiwa na nini? uchezaji, uvaaji, mdundo, ujumbe uliokuwemo n.k n.k
Angalia upande wa pili,

Nyimbo za seduce na ziipendwa zimepishana siku moja au mbili kutoka, je wcb walitunga saa ngapi nyimbo, walirekodi muda gani, walishoot muda gani

kwa uharaka wa kusema wamemjibu king
 
Atubela,
Hujamsikiliza kiba leo?
Hyo nyimbo alirecord 2yrs ago, kaitoa kama starter, yani ukienda hotel kubwa ukaagiza chakula wakati wanakiandaa unapewa vi bites ili vikupunguzie njaa wakati unasubiri oda yko, so kiba hyo ni starter, nyimbo yenyewe inakuja soon
 
So fans wa Kiba wameangalia wimbo ili kumkomoa tu Dayamondi sio sababu wimbo wa Kiba mzuri! Wabongo bana
 
Watanzania inaonekana tumezowea muziki tempo fulani tu, kwa hiyo ukija muziki wa tempo nyingine tuanona si mzuri.
 
Je unafanyaje hadi ufikie kulipwa? na ni viewers wangap wanahitajika ili ulipwe? na kwanini unalipwa? Na ninani anaekulipa tafadhalini ndugu zangu nisaidieni kwa hilo nahitaji kufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unalipwa kwa kutumia AdSense ili uweze kupata matangazo ya adsense videos zako. Zinatakiwa kuwa na viewers angalau 10000 na ujitahidi kuweka video ambazo haziviolet mambo ya copyrights. Ili kuweza kutoa pesa unapaswa ufikishe angalau $100 na utachagua njia ya kulipwa
 
Back
Top Bottom